Katibu mkuu wa UN asema siku ya Jumanne kuwa kuna umuhimu kuwajumuisha watu walio na ulemavu katika ajenda yamaendeleo ulimwenguni

Dunia yakoo

Senior Member
Nov 23, 2019
139
214
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa (UN),Antonio Guterres, alisema siku ya Jumanne kuwa kuna umuhimu kuwajumuisha watu walio na ulemavu katika ajenda ya maendeleo ulimwenguni.

Akizingumza wakati wa kongamano la siku ya walemavu ulimwenguni, Guterres alisema tunapolinda haki za watu walemavu, tunakiribia kufanikisha malengo ya mwaka 2030 ya kutomwacha yeyote nyuma.

''Siku hii ya kimataifa nasisitiza kuwa umoja wa mataifa iko tayari kufanya kazi na watu walemavu ili kuleta mabadiliko siku za usoni ambayo yatafurahiwa na kila mtu wakiwemo wanawake, wanaume, wasichana na wavulana ili kuwawezesha kutimiza ndoto zao.'' Alisema Guterres.

ULAYA.jpg
 
Kumbe walikuwa hawajumishwi,tuanze sasa hatua makanisani na misikitini tuwe na wakalimani wa lugha za alama
 
Back
Top Bottom