Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon Kugombea Urais,Korea Kusini.

Kazetela

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
1,714
1,618
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon
amedokeza kuwa huenda akawania urais nchini
mwake, Korea Kusini.

Muhula wake Ban kama katibu mkuu wa Umoja wa
Mataifa unakamilika mwisho wa mwezi huu wa
Disemba
Wakati wa mkutano wake wa mwisho na waandishi
wa habari, Ban alisema kuwa baada ya kupata
mapumziko anarudi nchini mwake Korea Kusini
kuona vile ataisaidia nchi yake.

Uchaguzi wa uraia nchini Korea Kusini unatarajiwa
kufanyika Desemba mwaka 2017
Ban Ki-Moon amfuta kazi kamanda wa jeshi
Sudan Kusini
Ban Ki-moon aisihi Afrika Kusini kutojiondoa
ICC
Lakini huenda uchaguzi huo ukafanyika katika muda
wa miezi miwili baada ya bunge la nchi hiyo kupiga
kura ya kumuondoa madarakani Rais Park Geun-hye,
kutokana na sakata, ambapo analaumiwa kwa
kumruhusu rafiki wake wa karibu kunufaika kifedha.

Ikiwa mahakama ya katiba itadumisha kura hiyo ya
kumuondoa, atakuwa rais wa kwanza wa Korea
Kusini aliye madarakani kuondelwa katika kipindi
cha uhuru wa nchi hiyo.

Mahakama ya katiba ina siku 180 kutoa uamuzi wa
mwisho.

Matamshi ya Ban yanakuja huku yakishuhudiwa
maandamano kwenye mji mkuu wa Korea Kusini,
Seol.
 

Attachments

  • 1481977671509.jpg
    1481977671509.jpg
    10.5 KB · Views: 67
Back
Top Bottom