eliesikia
JF-Expert Member
- Oct 29, 2010
- 787
- 755
Habari,
Katika hali ya kawaida kabisa inafahamika Katibu mkuu ndio msimamizi na msemaji mkuu wa chama. Lakini kwa CUF ni tofauti sana hasa wanapotoa kazi hii kwa naibu au mwenyekiti. Mi siijui katiba "vizuri" ya CUF lakini nimeona kwenye katiba yao hayo maelezo ndio yapo.
Kwa kuwa hivi karibuni chama cha CUF na CHADEMA wanagombana sana haswa kwenye swali la nani mtawala na nani ni mpinzani. Basi huu ni wakati muafaka kwa Katibu Mkuu Mhe. Maalim Seif kueleza umma kuwa chama chake ni cha mlengo gani na nia gani na nadhani mabishano yoote haya yataisha.
Pia, CUF wanasema CHADEMA ina "kebehi" serikali ya umoja wa kitaifa ya Zanzibar na kudai kuwa wanataka kuulazimisha UMMA uamini kuwa CUF na CCM ni anko na shangazi wote shuka moja. Lakini kiukweli anaujua huyu katibu mkuu ambaye ndiye msimamizi mkuu wa chama hiki na ndie mshiriki katika hii serikali. JuziJuzi alilalamika kazi za kichama zimekuwa nyingi na anataka msaidizi lakini nadhani kwenye maswala haya ya msingi ni wakati muafaka akajibu kwa umma kuwa wao CUF ni chama tawala au upinzani. Na jee serikali ya kitaifa ina maana gani kama si kushirikiana na CCM???!!
Hapa kuna "mkanganyiko" mkubwa wa mambo haswa:
1. Je wakiunda serikali kivuli pamoja na CHADEMA ni wabunge wapi waingie wale waliotoka kwenye serikali ya umoja Zanzibar au bara?
2. Je hao CUF wanatekeleza sera ipi na ilani ipi ya chama kipi katika serikali ya umoja wa kitaifa?
3. Je hao CHADEMA wakikubali kuungana na CUF ni sera au ilani ya chama gani watakubaliana kuifuata? Eg. CCM wanadai kilimo kwanza lakini CUF wao wanaweza wakataka elimu kwanza na CHADEMA wao wakataka ajira kwanza kwa wananchi. sasa ni sera gani wanaweza kuweka sawa maana naaamini sera ni kama dini ukiamini yabidi kufuata na kabla yahitaji kujitayarisha.
4. Je katika kutekeleza hayo yote CHADEMA hawakuwa na sera ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na yeyote hata kama wangeshinda uchaguzi? Kuna hasara na faida ya kufanya hivi. Moja yawezekana "PLANS" zako ukafanikiwa au usifanikiwe kwa hiyo hutaki kumwingiza mwenzako mkaangukia pua pamoja.
Baada ya hizo hoja za msingi na madalizo mbalimbali naamini Mhe. Maalim Seif mwanaCCM wa zamani na MwanaCUF kindakindaki akayaeleza kinaga ubaga ili ubishi woote uishe. Na CUF itakuwa huru kuchagua njia ipi ya kupita kuliko kurukia njia mbili "mtaka mawili moja humponyoka".
MYTAKE:
Mimi nimeona ukimya wa huyu bwana na wenzake kama mgombea mwenza wa Lipumba, Mhe. Duni waziri wa afya na wengine wanaoshiriki serikali ya Umoja wa kitaifa ndio yaliyoleta manung'uniko kwa CHADEMA kupelekea kuwashuku "vibaya" wenzao. Na bado naamini hii siri iliyojificha hapa ndio kisa chenyewe kwa kuwa CHADEMA wanaamini hawa jamaa ndio CUF halisi toka enzi ikianzishwa.
Baadae
Nawasilisha hoja