Katibu Mkuu wa CUF - Lipumba, Magdalena Sakaya: Mimi kama mwanaye, Maalim Seif akihamia CHADEMA hawezi kushinda Urais Zanzibar

Daimler

JF-Expert Member
Sep 11, 2018
556
973
IMG_8270.JPG

Katibu Mkuu wa CUF -Lipumba, Magdalena Sakaya, akiongea na Mwananchi amemshauri Maalim Seif kuachana na mpango wake wa kuhamia CHADEMA na badala yake atulie kulinda heshima yake. Alisema ingawa ni hiari ya mtu, itakuwa jambo la ajabu kama Maalim atahamia CHADEMA kisha kugombea Urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2020. "Akienda CHADEMA hawezi kushinda nafasi hiyo .... kwa sababu Chama hiki hakina nguvu Zanzibar."
Sakaya aliongezea kuwa, "Mimi kama mwanaye na yeye ni baba, ninamshauri atulie tu ili ajenge heshima yake kwa sababu alishawahi kuwa kiongozi mkubwa katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar."

IMG_8269.JPG
 
Sakaya anajua fika Maalim kuhamia CDM ndiyo kifo cha CUF bara na visiwani. Kwa maana nyingine CUF itakuwa kama TLP chama kisicho na mbunge kabisa. Kwa hiyo ni lazima wamsihi asihame. Dawa ni moja tu Lipumba kuacha kutumika kwake, vinginevyo wapende wasipende CUF Maalim na CDM wataungana tu.
 
CUF imekua ikishinda chaguzi Zote Zanzibar, Ushahidi upo..Ila Nchi hawapewi au Ushindi gani anamaanisha huyu Bibie.
 
View attachment 865741

Katibu Mkuu wa CUF -Lipumba, Magdalena Sakaya, akiongea na Mwananchi amemshauri Maalim Seif kuachana na mpango wake wa kuhamia CHADEMA na badala yake atulie kulinda heshima yake. Alisema ingawa ni hiari ya mtu, itakuwa jambo la ajabu kama Maalim atahamia CHADEMA kisha kugombea Urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2020. "Akienda CHADEMA hawezi kushinda nafasi hiyo .... kwa sababu Chama hiki hakina nguvu Zanzibar."
Sakaya aliongezea kuwa, "Mimi kama mwanaye na yeye ni baba, ninamshauri atulie tu ili ajenge heshima yake kwa sababu alishawahi kuwa kiongozi mkubwa katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar."

View attachment 865740
Maalim seif sio mwanasiasa wa kubabaisha,ni bingwa wa siasa za zanzibar pia ni taasisi ya kisiasa huko zenji,kwa wanaccm na wasio wana ccm wote kwa umoja wao wanamkubali na kumtegemea,subira ya vuta kheri mtasikia siku moja,akitangazwa kuwa rasi wa zanzibar
 
Back
Top Bottom