Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK) mbaroni kwa kuomba rushwa ya Tsh. Milioni 50

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,402
1643351028948.png

Picha: Renatus Muabhi

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) inamshikilia Katibu Mkuu wa Chama cha Siasa kiitwacho Chama Cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi kwa kujifanya Mtumishi wa Taasisi hiyo

Anadaiwa pia kuomba rushwa ya Tsh. Milioni 50 kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Bharya Engineering & Contracting Company Limited (BECCO), Manraj Bharya

TAKUKURU imeeleza kuwa imebaini Renatus aliomba rushwa hiyo akidai kutaka kumsaidia Bharya katika tuhuma zake zinazomkabili kuhusu IPTL

Mtuhumiwa alikamatwa Desemba 10, 2019 jioni katika ofisi za BECCO akiwa amepokea fedha za mtego Tsh. Milioni 1 zilizokuwa zimeandaliwa na kuchanganywa na nyingine kufikia Milioni 50.

Pia soma:

- Aliyekuwa Katibu Mkuu CCK mbaroni kwa kujifanya ‘usalama’ (28/01/2022)
 
Mmh! Atakuwa kachezeshewa mchongo labda. Katibu wa chama anaweza kufanya haya?!! Ngoja niweke akiba ya maneno
 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) inamshikilia Katibu Mkuu wa Chama cha Siasa kiitwacho Chama Cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi kwa kujifanya Mtumishi wa Taasisi hiyo....
Halafu Mweyekiti cha mama hicho anakuja kujinasibu anataka kugombea U RAIS jaman MUNGU awe nasi tu
 
Chama cha siasa kilichobaki nchi hii ni CCM..Hivi vingine ni vikundi vya vigodoro
 
Kwahiyo kama na ushahidi wa pesa za moto ulikuepo imekuwaje ametoka mpaka leo 2022 ana kesi nyingine ya utapeli?

Mahakama zetu zimeoza? Au nini kilitokea?

Anyway, bongo movie wanahitaji kutengeneza muvi za stori za matukio kama haya.
 
Kwahiyo kama na ushahidi wa pesa za moto ulikuepo imekuwaje ametoka mpaka leo 2022 ana kesi nyingine ya utapeli?

Mahakama zetu zimeoza? Au nini kilitokea?

Anyway, bongo movie wanahitaji kutengeneza muvi za stori za matukio kama haya.
Kuna makosa nadhani, jamaa alikamatwa kwa makosa ya kujifanya afisa wa Takukuru decemba 10, alafu tarehe 24/12 akafanya kosa kama hilo akiwa Bado na kesi kama hiyo!
 
Back
Top Bottom