Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
Tunasema tuzae bila kikomo, kuzaa ni jambo jema, hakuna anayepinga kuzaana lakini tuzae kwa mpango, mpangop wa taifa umeelekeza zitengwe fedha kwa ajili ya kutoa elimu ya uzazi wa mpango ili tupate taifa la wazalishaji kwa maendeleo ya taifa hili
Kila ongezeko la watoto linasababisha kuongezeka kwa msongamano darasani, tamko la kuzaana bila kikomo limetolewa Simiyu mkoa ambao watu wake wanazaliana kuliko eneo lolote nchini, ni mkoa uliyo na wananchi wengi wasiojua kusoma na kuandika
Hivi ni nani kati yenu alikwenda kufundishwa jinsi ya kuweka mimba kwa mwanamke au kupokea mimba kutoka kwa mwanamme?
Tusipowafundisha hawa watoto tutegemee ongezeko la mimba za utotoni, Ni jukumu letu kuendelea kuwafundisha kuhusu uzazi wa mpango kwa ajili ya maeneleo ya taifa letu
Kwa mwanamme ni rahisi sana kusema abebe mimba tu, lakini mwanamke anafahamu kichefuchefu anachokipata, madhara wakati wa kujifungua, wanaume wote tunaowajali wanawake tuungane kuhakikisha tunaimarisha uzazi wa mpango na kupeleka wake zetu kliniki
Nyie mnataka wake zetu wawe wanakufa tu hospitalini kwa sababu mnaweza kuoa wake wengine? Hii haikubaliki
Msimamo wa Chadema ni kwamba, watoto wote katika Taifa hili wenye umri wa kwenda shule wapelekwe bila kujali jinsia wala jinsi yake
Tunaambiwa hawa mabinti waliopewa mimba wasirudi shule kusoma, kama unazuia uzazi wa mpango unadhani wataachaje kupata mimba?
Wananchi hivi sasa badala ya kuona kiza, sasa wanapaswa kuwasha mshumaa kuleta nuru
Itakua ni fedheha na aibu kwa mtumishi kukaa na Ilani katika utekelezaji wa maendeleo, ni aibu kubwa
Katika ziara ya Rais tumeshuhudia viongozi wakiwekwa ndani bila sababu za msingi, viongozi wanakaripiwa hii haileti taswira nzuri katika Taifa na hata kwa kiongozi
Taasisi ya urais inapwaya na kama haipwai basi Rais anazungumza maoni yake ambayo sisi wananchi hatuyahitaji, huwezi kumpangia mtu utaratibu wa kuishi
Sio swala la Ng'ombe kuzaa wala kuwa na chakula, kila ongezeko la watu ambalo halina kwenye mpango linaweza kusababisha ongezeko la hali mbaya ya maisha
Ifike wakati tuanze kufungiana "Speed Govener" kiongozi wa nchi anapoanza kuzungumza mawazo yake binafsi tena yasiyokubalika inaleta ukakasi mkubwa katika nchi
"Kuna tatizo la mimba za utotoni, mfano kule alikokuwa anahutubia kuna mabinti wadogo na ukiwaangalia utadhani wana umri mkubwa sasa asipopata elimu ya uzazi tunatengeneza nini?"
Dk. Mashinji amesema, kwa wanaume wanaojali na wanaume wote Tanzania niwaombe tushikane kwa pamoja kuimarisha afya ya uzazi na tuwapeleke wake zetu tukapate elimu ya uzazi wa mpango kwa maendeleo yetu
"Waliopata kadhia katika ziara ya Rais, waelewe ndio hali ya mawasiliano katika Taifa letu na badala ya kulalamika gizani sasa wawashe mshumaa kwenye giza"
Kuhusu suala la CHADEMA kujiimarisha kwa kutumia CUF Zanzibar kama alivyosema Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Hashim Juma Issa Dk. Mashinji amesema kama chama bado hawajajadili suala hilo huenda ni matamanio ya wanachama