Katibu mkuu wa CHADEMA John Mnyika ateta na mabalozi walipowasili mahakamani 10-9-2021 katika kesi ya Mbowe

LAZIMA NISEME

JF-Expert Member
Apr 5, 2015
232
260
Kumekuwepo na maswali mengi juu ya Wanadiplomasia hawa kujihusisha na Mambo ya Ndani ya Nchi na kwamba wanakiuka mkataba wa Viena waliotia saini mwaka 1961 juu ya maswala ya kuingilia shughuli za ndani za dola nyingine, kuonekana leo kwa Mnyika akitoa maelezo ya mwenendo wa Kesi ya mwenyekiti wa Chadema vinatoa Taswila gani kwa Mamlaka za Tanzania?



Screen Shot 2021-09-10 at 11.08.52.png


Screen Shot 2021-09-10 at 11.09.11.png


Screen Shot 2021-09-10 at 11.10.00.png
 
Hapo ndipo nchi ilipofikia. Rais mwenye mamlaka kamili hawezi kuachia hili hao ni wa kupewa masaa 24 tu.
Wote?Akimaliza kutoa notisi hiyo na Mabalozi wake pia wanarudishwa nyumbani na ndiyo inakuwa mwisho wa misaada,Uwekezaji na Utalii.Mtakuwa tayari?
Pengine ni vema wanapohudhuria wanajithibitishia ugaidi ili watusaidie kuutokomeza,bado utataka wafukuzwe?
Akili za CCM wanazifahamu wenyewe.
 
Hapo ndipo nchi ilipofikia. Rais mwenye mamlaka kamili hawezi kuachia hili hao ni wa kupewa masaa 24 tu.
Mabalozi swala la ugaidi ni muhimu sana kwao kwa ajili ya usalama wa wao na raia wao. Hukumu ndiyo itawafanya waendelee kuwapo au waondoke. Unapoitangazia dunia kuwa nchini mwako kuna ugaidi ujue huo si bongo muvi hivyo lazima ukubaliane na wasiwasi wa wale uliowalenga, unaweza ukachukua njia ya mkato ukawafukuza nawe ukaendelea na ugaidi wako.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom