figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
KATIBU MKUU DKT. MASHINJI AONYA; NI HATARI RAIS ASIPOZINGATIA SHERIA, KUTOKUBALI KUKOSOLEWA
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Vincent Mashinji ameitaka Serikali iliyoko madarakani kutambua kuwa kuheshimu na kuzingatia sheria za nchi si jambo la hiari, kwani kinyume chake ni kuiweka nchi katika sintofahamu kubwa na kurudisha nyuma dhana nzima ya maendeleo ya watu.
Katibu Mkuu Mashinji amesema hayo leo alipokuwa akizungumzia hotuba ya Rais John Magufuli aliyoitoa leo Ikulu, jijini Dar es Salaam, alipokuwa akiwahutubia wakurugenzi wateule wa wilaya, miji na majiji, aliowateua hivi karibuni.
Amesema kuwa kwa muda mfupi tangu Serikali ya CCM chini ya Rais Magufuli iingie madarakani taifa linazidi kuthibitisha tatizo kubwa la kutozingatia utawala wa sheria, huku viongozi wakuu wakionekana kuwa vinara wa kuzivunja, hali ambayo ikiachwa iendelee kuna hatari kubwa ya maendeleo ya wananchi kurudi nyuma badala ya kusonga mbele.
Akisisitiza umuhimu wa dhana ya utumishi wa umma ‘kutofanyiwa siasa’ kama inavyoanza kujitokeza, Dkt. Mashinji amesema kuwa hakuna maelezo yanaweza kuridhisha kwanini Rais Magufuli amevunja sheria na kuteua wanachama wa CCM, kuwa watumishi wa umma, wakati sheria na misingi ya utumishi wa umma inakataza.
Akirejea hotuba hiyo, Katibu Mkuu Dkt. Mashinji ametoa mfano mwingine akisema kuwa haikuwa sahihi kwa Rais Magufuli kuwaagiza wakurugenzi hao wapya kuwaadhibu walimu kwa kuwakata mishahara iwapo madawati ya wanafunzi waliyokabidhiwa hivi karibuni yatakutwa yamevunjika.
“Kwani walimu hao wanajua ubora wa madawati hayo? Wanajua yametengenezwa wapi? Walihusishwa katika mchakato wa manunuzi? Adhabu ya kumkata mtu mshahara katika utumishi wa umma ni kubwa sana, ni karibu na kumfukuza mtu kazi. Kwanini adhabu zingine kama kupewa onyo au onyo kali zinarukwa? Ni kama rais hatambui kuwepo kwa sheria au la awe anaandikiwa hotuba,” amesema Dkt. Mashinji.
Akizungumzia dhana mbalimbali kutokana na kauli za Rais Magufuli katika hotuba hiyo, Dkt. Mashinji ameongeza kusema kuwa ni jambo la hatari kwa mkuu wa nchi kubeza suala la uzoefu katika utendaji na ufanisi wa kazi yoyote hasa inayokusudiwa kuleta tija na ustawi kwa wananchi.
“Rais asichanganye mambo. Kuna tofauti kubwa kati ya uzoefu, weledi na ujuzi katika kazi na kufanya kazi kwa mazoea. Ukimsikiliza kwa makini anachanganya kati ya business as usual na experience. Hatuwezi kamwe kubeza uzoefu katika kazi halafu tukategemea maendeleo kutoka kwa watumishi wetu.
“Suala la uzoefu ni sifa inayokubalika na kuzingatiwa kimataifa. Kuna watu sasa wanakubalika kwa sifa inaitwa QBE yaani Qualifying By Experience. Kwa dhana hii ya kubeza uzoefu maana yake kuna siku tutapewa hata majenerali kwa sababu tu wana shahada bila kuzingatia uzoefu wake katika combat na kupiganisha. Kubeza uzoefu ni kukubali ubabaishaji kama kigezo cha kuteua makada wa CCM kwenye utumishi wa umma kinyume cha sheria,” amehoji Dkt. Mashinji na kuongeza;
“Lakini pia dhana ya uzoefu katika kazi isichanganywe na umri wa mtu. Si lazima uwe na umri mkubwa. Uzoefu kuwa sifa ya kazi ni suala la mtu kukijua na kukielewa kwa kiwango cha kutosha hicho kitu anachotakiwa kukifanya. Sasa ukiona mkuu wa nchi anabeza uzoefu, tena mbele ya watu wanaokabidhiwa majukumu ya utumishi wa umma, unapata shaka nchi inavyoendeshwa na inakopelekwa hata dhana nzima ya maendeleo inakuwa shakani.
“Jambo jingine ambalo ni vyema wananchi wakawa nalo makini kuhusu utawala huu wa CCM na kuendelea kulipinga, ni tabia ya Rais kutosikiliza maoni tofauti…inaonekana Rais Magufuli hapendi kukosolewa na zaidi ya hapo anapenda kufanya mambo kwa kukomoa watu. Kathibitisha hilo leo, tena mbele ya watu ambao wanatakiwa kwenda kufanya kazi na wananchi vijijini kuhusu maendeleo ambako lazima wawasikilize wananchi pia.
“Inasikitisha kumsikia Rais anawaambia wakurugenzi kuwa anatumia neno vilaza kwa sababu anajua watu hawapendi kulisikia…huku akijua kabisa kuwa neno hilo alilitumia isivyokuwa sahihi kuwaita wale wanafunzi wa Diploma ya Ualimu kule Chuo Kikuu Dodoma ambao walidahiliwa kwa mujibu wa sheria. Huu utaratibu wa rais kufanya mambo kwa kukomoa ndiyo alioutumia kufanya uteuzi wa baadhi ya watu alionao. Ni jambo la hatari sana,” amesema Katibu Mkuu.
Aidha amemtaka Rais Magufuli kuwachukulia hatua za kisheria Wakurugenzi wote ambao wameachwa katika uteuzi huu kwani ameutangazia umma kuwa amewaacha kwa sababu ni wezi sasa kama ameshathibitisha kuwa ni wezi ni vyema sasa sheria ichukue mkondo wake na kinyume na hivyo ni kuwadhalilisha watumishi hao na anatakiwa kuwaomba radhi mara moja tena hadharani au athibitishe wizi wao kwa kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria ili watanzania waweze kumwelewa.
“Watumishi hawa waliohukumiwa na Rais leo kuwa ni wezi waliteuliwa na serikali hii hii ya CCM na ambayo Magufuli mwenyewe anatokana nayo, sasa kama watu wote hao 120 walikuwa wezi ni nani yuko salama huko kwenye serikali ya CCM, maana hata aliowateua sasa ni makada wa chama hicho hicho” amehoji Dkt. Mashinji
Imetolewa leo Jumanne, 12 Julai, 2016 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA