Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Vincent Mashinji hana commanding power ndani ya chama

Mkuu huku shida sana. Kilio kabisa.

Maana wakati Edo anakataza watu kulipa kodi hana la zaida zaidi ya kupiga makofi.

Sauti tu nayo shida. Unapoongea ni kama kikao cha harusi na si mkubwa.

Ingawa si shida kwake maana alikuwa anaongea na mtu asiyempenda.
Dah! Aiseeee! Kumbe hata nyie wana CHADEMA mmeliona hili!
 
Umesahau pia kuwa Lowasa kanunua chama

Katika bei aliyouziwa hicho chama wewe au chama chako kilimwongezea kisi gani kukinunua?Kwanza Lowassa hashindi Lumumba mnakolipiwa hizo buku saba na huna uwezo wala sifa ya kuingia ofisini kwake sasa suala la yeye kununua chama hadi kuijua na bei taarifa hizo umezipata huko huko Lumumba?Nawe hangaika ya miaka yote isiyopungua 15 hukuambulia hata ukuu wa wilaya?Kina Shonza na Mwampamba wa juzi huoni wanakuacha ukizeekea buku saba Lumumba? Au tatizo ni elimu au umri umeenda mno?Dodoma yapo madili kwa sasa utabeba hata briefcase za wanaokulipa huko Lumumba maana kazi nyingine huwezi.
 
Hili kimedhihiri jijini Arusha wakati Lowassa akiongea na Mameya wa Majiji, Miji na Halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA. Yaani hakika nilistaajabu sana. Eti Edward Mbona polisi hawakumzuia? CHADEMA na BAVICHA yake nafikiri sasa mard Lowasa, Mjumbe wa Kamati Kuu ndiye anakuwa mgeni Rasmi ilhali Mwenyekiti wetu Mbowe yupo. Ijapokuwa Mbowe hakuwepo kwenye kikao hicho, nilimuona Katibu Mkuu wetu Dr Vicent Mashinji akiongea kwa lugha ya upole kabisa kama anafanya doagnosis kwa mgonjwa.

Yaani Katibu kapwaya sana na sijajua mpaka sasa sifa zilizomshawishi Mwenyekiti wangu Mbowe mpaka akapendekeza jina la Katibu Mkuu dhaifu kama huyu. Anaongea taratiiiibu na hata kama mtu anaharibu mbele yake, anamuacha tu anaharibu na hamkemei. Mathalani, wakati Lowassa anatoa tamko kuwa CHADEMA sasa kimegraduate kutoka kikundi cha harakati na kuwa chama cha siasa, Dr Mashinji alikuwa anamuangalia tu na hakuchukua hatua yoyote. Nilimuona alipoa kabisa tena nimemuona akipiga makofi kuonesha kuwa anachosema Lowassa ni sahihi.

Hakika nawaambia. Tukiendelea na huyu jamaa chama chetu kitapotea sana. Nasikia CCM wana mpango wa kumpa Mangula kuwa Katibu Mkuu. Sasa linganisha Mangula na huyu muigizaji wetu wapi na wapi. Lazima tuisome namba. Ni wakati sasa wa kubadilika na kumshinikiza Mbowe abadili gia angani kwa kutengua uteuzi wa Dk Mashinji.
Nonsense
 
Mimi sio mwanachadema na sijawaji kuwa mwanachadema ila mimi najua umuhimu wa kuwa na vyama vingi vyenye nguvu.

Wewe ni kati ya wapinzani wasiojua kuwa vyama vyao sio vikundi au NGOs za kiharakati bali ni vyama vya siasa.

Lowasa ndilo gwiji la siasa Tanzania nzima tangu enzi za ujana wake. Kwa mtu yeyote anayejua siasa atakubaliana na Lowasa kuwa kwa sasa CHADEMA kinapaswa kuwa chama cha siasa na sio chama au NGOs ya harakati .
Kauli hii ya Lowasa iliwaumiza sana kichwa CCM . Baadha ya wanasiasa uchwara ndani ya Chadema ndio walishtuka mana wao bado Chadema ni NGOs ya kutafutia mikopo na pesa za ufadhili.

Chadema kwa sasa keshajijenga kwa kiwango kikubwa na ni wakati sasa wa kuhakikisha kinauza sera na mikakati ya ushindi kwa wananchi kwa njia ya amani.
Chama chenye Mawaziri wakuu wastaafu wawili hakiwezi kuendelea kufanya siasa za matukio. Hakiwezi kuwa chama cha kulalamika na migomo na maandamano.
Kwa mfano suala la Kuzuia uhuru wa kujieleza na kupata habari ulioko kikatiba sio suala la vyama vya upinzani vilivyokomaa kuandamana kabla ya kujua nini msimamo wa jamii iliyopo.Je,inauelewa wa kutosha juu ya hilo?
Je ndani ya chama kuna uelewa wa pamoja juu ya hilo?
Chama kikubwa kama chadema kinapaswa kufanya siasa kwa vikao na nyaraka zenye matamko ambayo yatasomwa kama msimamo wa chama kuanzia juu mpaka chini.
Na haya yatawezekana watakapoanza kufanya kazi kisera na kuwa na ofisi mpaka kwenye matawi.

Kuna watu wanafikiri kuwa kutumbua majipu ni sera ya chama pekee. Hilo ni suala la kila mtanzania na linapaswa kusimamiwa kuanzi ngazi ya tawi mpaka juu. Hilo ni suala la kisheria. Ndio maana inakua vigumu kujua nani fisadi na mwizi. Mfano leo tukiulizana tuhuma zote zilizowahi kulalamikiwa bungeni ziliishia wapi?
Mfano tuhuma za Kashfa ya Chavda, Richmond,EPA, Meremeta, Kiwira, Uuzwaji holela wa nyumba za umma, Kivuko kibovu, mabehewa feki, ESCROW, IPTL , Radar,ndege ya rais ,Lugumi n.k.
Ukiangalia utagundua kuwa ziliishia hewani kwa sababu zililenga kummaliza mtu kisiasa wakati zilifanya na watu kisheria kutokana na mamlaka waliyokuwa wamepewa kisheria.Pia zilishirikisha wataalam kwenye wizara ambao wengi ni makada wa chama tawala.

Sasa bila kuwa na chama cha upinzani chenye kuhubiri sera na namna ya kuondoa huo mfumo ulioshikamana na kila baya na jema kwenye nchi hii itakua ni vigumu kuiondoa CCM madarakani. Na kama chama cha upinzani kitaendelea na kufanya kazi kiharakati itakua ni vigumu kukabidhiwa nchi na waliopo mana kitakua hakijajiandaa kufanya mambo yake ki mikakati. Lazima CDM sasa waandae sera na mikakati imara ya namna ya kukuza uchumi na sio kila siku kuzungumzia matukio tu au kukosoa tu.
Lazima wajiulize je,walioko nadarakani kama hawata kosea ina maana watakosa sera.?
Mbona nchi zenye maendeleo kama Marekani na Ujerumani na Uingereza wana upinzani imara na wanabadilishana mara kwa mara? Jibu ni kwamba wana shindana kwa sera nzuri na namna ya kuwapa wana nchi unafuu wa maisha, kulinda uhuru wao wa kuheshimika na kuishi kama binadam na ulinzi wa maisha na mali zao .
Kwetu wapinzani wanazunguka na kufanya harakati za kuwaambia wananchi wapambane na vyombo vya dola. Je, wao wakiingia madarakani hao wananchi watakua wameacha kupambana na dola?

Na pia uelewe kuwa Kwenye hali ya kawaida Lowassa anaweza kuwa mgeni Rasmi au mtoa mada kutokana ukweli kuwa ni waziri mkuu mstaafu( ndio ni mstaafu kwa kuwa hiyo ni nafasi ya uongozi ya kisiasa na haina kikomo maalum, unaweza ukabadilishwa au kujiuzulu au kuondolewa kwenye nafasi hiyo) . Na pia alikua ni mgombea urais wa UKAWA.

Suala la katibu mkuu kupwaya hilo liko wazi.
Chadema hawana Katibu mkuu. Kwani muda alioingia madarakani hajaonyesha jambo lolote hata kutoa tamko tu la masuala muhimu ya nchi kama anashindwa kukosoa basi azunguke nchi nzima kumuunga mkono Magufuli na serikali yake. Pia itamsidia baadae kukosoa.
Vinginevyo chama kimepwaya kwenye nafasi hiyo ya ukati mkuu.

Pia inaonekana kuwa chadema hawakujiandaa kushindwa kwenye uchaguzi hivyo hawakujiandaa kurudi mtaani na kuendelea na siasa.
 
Dr Mashinji anapambana na wapayukaji ndani ya chama.

Ndani ya chadema kuna visebengo wa kuropoka kila kitu bila kujua kuwa chadema haina ofisi yake kwa miaka 20!!!
 
Naona wazee wa buku saba mnatafuta kuibadil mada kutusahaulisha tarehe 23 Julai....Loading
 
Huyu ndo kavaa viatu vya dr silaa au kavaa tuu soks viatu kaacha...sdm mpo kwenye wakati mgumu sana
 
Hili kimedhihiri jijini Arusha wakati Lowassa akiongea na Mameya wa Majiji, Miji na Halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA. Yaani hakika nilistaajabu sana. Eti Edward Mbona polisi hawakumzuia? CHADEMA na BAVICHA yake nafikiri sasa mard Lowasa, Mjumbe wa Kamati Kuu ndiye anakuwa mgeni Rasmi ilhali Mwenyekiti wetu Mbowe yupo. Ijapokuwa Mbowe hakuwepo kwenye kikao hicho, nilimuona Katibu Mkuu wetu Dr Vicent Mashinji akiongea kwa lugha ya upole kabisa kama anafanya doagnosis kwa mgonjwa.

Yaani Katibu kapwaya sana na sijajua mpaka sasa sifa zilizomshawishi Mwenyekiti wangu Mbowe mpaka akapendekeza jina la Katibu Mkuu dhaifu kama huyu. Anaongea taratiiiibu na hata kama mtu anaharibu mbele yake, anamuacha tu anaharibu na hamkemei. Mathalani, wakati Lowassa anatoa tamko kuwa CHADEMA sasa kimegraduate kutoka kikundi cha harakati na kuwa chama cha siasa, Dr Mashinji alikuwa anamuangalia tu na hakuchukua hatua yoyote. Nilimuona alipoa kabisa tena nimemuona akipiga makofi kuonesha kuwa anachosema Lowassa ni sahihi.

Hakika nawaambia. Tukiendelea na huyu jamaa chama chetu kitapotea sana. Nasikia CCM wana mpango wa kumpa Mangula kuwa Katibu Mkuu. Sasa linganisha Mangula na huyu muigizaji wetu wapi na wapi. Lazima tuisome namba. Ni wakati sasa wa kubadilika na kumshinikiza Mbowe abadili gia angani kwa kutengua uteuzi wa Dk Mashinji.

ni dhahiri wewe si kada wa CDM, ni fixi zako tu, maamuzi ya chama kuwa cha kisiasa zaidi yalishafanywa na vikao kitambo, wataalam mbalimbali walikilaumu Chadema kiko kiharakati zaidi, hivyo hata kikishinda uchaguzi hakitaweza kuongoza nchi, hivyo jitihada kubwa zilifanyika ili kiwe kisiasa zaidi, Dr Slaa alikuwa kiharakati zaidi, Dr Mashinji tangu ashike wadhifa wake anafanya kazi usiku na mchana
, ndani na nje ya nchi kukijenga chama kifikie hadhi ya Government in waiting, na so far anafanya vizuri sana. Kama mlitarajia Ktb Mkuu wa kupiga kelele majukwaani na kuandikwa/kuoneshwa kwenye vyombo vya habari huku chama kikiwa shaghalabaghala, basi mmenoa!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom