Kada wa CHADEMA
JF-Expert Member
- Feb 27, 2016
- 289
- 615
Hili kimedhihiri jijini Arusha wakati Lowassa akiongea na Mameya wa Majiji, Miji na Halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA. Yaani hakika nilistaajabu sana. Eti Edward Mbona polisi hawakumzuia? CHADEMA na BAVICHA yake nafikiri sasa mard Lowasa, Mjumbe wa Kamati Kuu ndiye anakuwa mgeni Rasmi ilhali Mwenyekiti wetu Mbowe yupo. Ijapokuwa Mbowe hakuwepo kwenye kikao hicho, nilimuona Katibu Mkuu wetu Dr Vicent Mashinji akiongea kwa lugha ya upole kabisa kama anafanya doagnosis kwa mgonjwa.
Yaani Katibu kapwaya sana na sijajua mpaka sasa sifa zilizomshawishi Mwenyekiti wangu Mbowe mpaka akapendekeza jina la Katibu Mkuu dhaifu kama huyu. Anaongea taratiiiibu na hata kama mtu anaharibu mbele yake, anamuacha tu anaharibu na hamkemei. Mathalani, wakati Lowassa anatoa tamko kuwa CHADEMA sasa kimegraduate kutoka kikundi cha harakati na kuwa chama cha siasa, Dr Mashinji alikuwa anamuangalia tu na hakuchukua hatua yoyote. Nilimuona alipoa kabisa tena nimemuona akipiga makofi kuonesha kuwa anachosema Lowassa ni sahihi.
Hakika nawaambia. Tukiendelea na huyu jamaa chama chetu kitapotea sana. Nasikia CCM wana mpango wa kumpa Mangula kuwa Katibu Mkuu. Sasa linganisha Mangula na huyu muigizaji wetu wapi na wapi. Lazima tuisome namba. Ni wakati sasa wa kubadilika na kumshinikiza Mbowe abadili gia angani kwa kutengua uteuzi wa Dk Mashinji.