Katibu Mkuu wa CCM taifa, Daniel Chongolo afanya mazungumzo maalumu na Joel Nanauka

KATIBU MKUU WA CCM TAIFA CDE DANIEL CHONGOLO AFANYA MAZUNGUMZO MAALUMU NA JOEL NANAUKA, DODOMA.

28.03.2022

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Cde Daniel Chongolo, Leo amekutana na Ndg Joel Nanauka na kufanya naye mazungumzo katika ofisi Kuu za CCM jijini Dodoma.

Katika mazungumzo hayo wamejadiliana mambo mbalimbali ikiwemo mchango wa Ndg Nanauka katika program mbalimbali za uimarishaji wa chama kwa ujumla na program maalumu zinazohusu vijana.

Ndg Joel Nanauka , alimpongeza Katibu Mkuu kwa kazi kubwa anayofanya na alimhakikishia kuwa yuko tayari kuendelea kutoa mchango wake kwa chama kuanzia ngazi ya Taifa hadi chini kabisa Kama ambavyo amekuwa akifanya siku zote.

Ndg Nanauka ambaye ni balozi wa Mtwara, alitumia nafasi hiyo pia kuwasilisha mambo mbalimbali ya kisekta yenye manufaa kwa mkoa wa Mtwara.

Baada ya Mazungumzo, Ndg Nanauka alimkabidhi Katibu Mkuu Zawadi ya baadhi ya Vitabu alivyoandika na kumtakia kila la Kheri katika mkutano Mkuu maalumu wa CCM Taifa unaofanyika tarehe 01.04.2022.
@joelnanauka_

Mtwara Online Tv
Habari Kiganjani Kwako

Joel NANAUKA ndiyo nani? Hii siyo mada ya kuwa Jukwaa La Siasa. Lapda iende Jamii pictures
 
Du balozi wa mtwara ! usijekuta huyu ndiye alietengeneza kale kabomu ka moshi ka kwenye ile V8 ya Jiwe siku zile,CCM ujanja janja za chini ya kapeti wanasema hata KATELEFONI siku Ile anatupiga FIX Pale msikitini njombe kuwa jiwe yupo kazini,kumbe alikuwa kwenye mazungumzo na mganga aliyemfufua Mangula yule mganga alimtolea nje
 
Hii nchi jamani, balozi wa Tanzania huko Mtwara? Au ni Balozi wa CCM huko Mtwara?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom