Katibu Mkuu wa CCM, Kinana na Nape watua Butiama,Wazuru kaburi la Baba wa Taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katibu Mkuu wa CCM, Kinana na Nape watua Butiama,Wazuru kaburi la Baba wa Taifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaDiwani, Sep 22, 2013.

 1. MwanaDiwani

  MwanaDiwani JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2013
  Joined: Mar 22, 2013
  Messages: 5,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katikati akiwa katika picha ya pamoja na Andrew Nyerere Mtoto wa Kwanza wa Baba wa taifa Mwalimu Julius K. Nyerere wakati alipozuru kaburi la Mwaasisi huyo wa taifa la Tanzania Mwitongo, Butiama Nyumbani kwa mwalimu Mkoani Mara jana, Kinana alifanyakazi na Andrew
  Nyerere wakati wakilitumikia Jeshi la Ulinzi la wananchi la Tanzania (JWTZ), Katibu Mkuu huyo jana aliendelea na ziara yake katika wilaya ya Butiama katika kuimarisha chama na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi, Kinana ataendelea na ziara yake katika Wilaya ya Serengeti leo. Kushoto ni Nape Nnayue Katibu wa (NEC) Itikadi Siasa na Uenezi.
  [​IMG]
  Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na Andrew Nyerere mara baada ya kuzuru Kaburi la Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere Mwitongo Butiama jana[​IMG]
  Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa tatu kutoka kulia akiongozwa na ndgu wa Mwalimu Mzee Jack Nyamwaga wakati akielekea kuweka shada la maua katika kaburi la Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere jana mjini Butiama, Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Butiama Mama Mabula[​IMG]
  Katibu Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katikati akiweka shada la maua kwenye kaburi la Hayati. Mwalimu Julius K. Nyerere huku Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi akishuhudia tukio hilo.[​IMG]
  Wana habari nao wakishiriki kuweka mashada ya maua katika Kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere jana kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Mtandao wa Fullshangwe Bw. John Bukuku, Said Mwishehe kutoka Jambo Leo Oktavian kutoka CCM Gerson Msigwa wa TBC, Ufo Saro wa ITV na Prosper Dereva wa CCM.
  [​IMG]
  Katibu Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa pili kutoka kulia akimsikiliza Balozi Safari wakati alipotembelea Shina namba 14 Mwitongo Butiama na kuzungumza na wanachama wa shina hilo ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero zao.[​IMG]
  Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi akisalimiana na Mzee Jack Nyamwaga huku katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa pili kulia akizungumza na mzee Mdogo wa Mwalimu Julius K. Nyerere Daniel Nyerere mara baada ya kumaliza kikao chake na wanachama katika shina namba 14 Mwitongo.[​IMG]
  Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi CCM kulia akizungumza na Mh. Nimrod Mkono aka "Mkono kwa Mkono"Mbunge wa Jmbo la Musoma Vijijini. [​IMG]
  Hili ni Jengo la zahanati ya kata ya Busegwe ambalo ujenzi wake unaendelea kwa kushirikisha Halmashauri ya wilaya ya Butiama vijijini Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Mh. Nimrod Mkono na nguvu za wananchi.
  [​IMG]
  Katibu Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupia lipu wakati alipokagua ujenzi wa zahanati ya Busegwe jana kulia ni Mgendi Sikila mmoja wa mafundi wanaojenga zahanati hiyo.[​IMG]
  Katibu Mkuu wa UWT Taifa na Mbunge w
  a viti maalum kutoka mkoa wa Mara Amina Makilagi akishiriki kubeba udongo, wakati Katibu Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokagua ujenzi wa zahanati hiyo kata ya Busegwe
  [​IMG]
  Katibu Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mganga mkuu wa Wilaya ya Butiama Dk Wilbert Manase wakati alipotembele ujenzi wa zahanati hiyo. [​IMG]
  Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini Mh. Nimrod Mkono akitoa maelezo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akikagua ujenzi wa zahanati Busegwe
  [​IMG]
  Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini Mh. Nimrod Mkono akishiriki kucheza ngoma na moja ya vikundi vilivyokuwa vikitumbuiza katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.[​IMG]
  Katibu Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimuangalia Katibu Mkuu wa UWT Taifa Bi. Amina Makilagi wakati akishiriki kucheza ngoma.

  [​IMG]
  Mkuu wa Wilaya ya Butiama Mama Mabula akizungumza na wananchi katika kijiji cha Bwai.


  [​IMG]
  Katibu Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimshukuru Diwani wa kijiji cha Bwai Jamila Nyamanda kupitia TPP Maendelea kwa ushirikiano wake katika kutekeleza ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM[​IMG]
  Katibu Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia jambo wakati alipokuwa akimsikiliza mzee Nyanda Totela wakati alipokagua Shule ya Msingi ya Bwai Musoma vijijini jana[​IMG]
  Shule ya Msingi Bwai inavyoonekana
  [​IMG]
  Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi CCM kulia akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana Kyabakari Butiama jana

  [​IMG]
  Katibu Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa mgolole na Katibu wa kabila la Zanaki Mzee Peter Nyamrubwe Nyamrubwe kama ishara ya kuwa mmoja wa viongozi wa kimila wa kabila la wazanaki, kulia ni Mh Nimrod Mkono Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini.
  [​IMG]
  Katibu Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi baiskeli kwa Gwesani M. Gwesani moja wa makatibu kata waliokabidhiwa baiskeli hizo kwa ajili ya kuimarisha Chama Wilayani Butiama
  [​IMG]
  Baadhi ya ananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara[​IMG]
  Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi akiwahutubia wakazi wa mji wa Kyabakari Wilayani Butiama jana

   
 2. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2013
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,397
  Likes Received: 231
  Trophy Points: 160
  wakuu ninahitaji kipande cha pembe ya NDOVU ninaweza kupata vipi? muhimu sana!
   
 3. b

  bakwesi Member

  #3
  Sep 22, 2013
  Joined: Jun 15, 2013
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi Kinana ni mwenyeji wa mkoa gani? Ni kabila gani maana hilo jina halimo katika kabila lolote Tanzania. Operesheni "kimbunga"!!
   
 4. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #4
  Sep 22, 2013
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 15,990
  Likes Received: 3,175
  Trophy Points: 280
  Wamekwenda kunajisi kaburi la Mwasisi wa CCM!
   
 5. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2013
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,701
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Samahani naomba kuuliza Labda mimi sielewi..! Hivi kuna diwani wa kijiji?
   
 6. MwanaDiwani

  MwanaDiwani JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2013
  Joined: Mar 22, 2013
  Messages: 5,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Umesahau kusema 'Kaburi la baba yako wa kufikirika'.

  Ulidanganya sana wanaJf kuwa wewe ni mtoto wa Mwl. Nyerere na kila jambo lilikuwa linahusu familia ya Mwl. Nyerere ulikuwa uko upfront kutoa comment ili uzidi kuwaaminisha wanaJf kama wewe ni mmoja wa watoto wa Mwl. Nyerere.

  Hata hii comment umeleta cynically kutaka watu wasiofahamu uwongo wako wadhani 'Mtoto halisia wa Mwl. Nyerere anatoa comment' kumbe ni tapeli anayetumia jina la Mwl. Nyerere ili innocent people wafikirie kama ni mtoto wa Baba wa Taifa.

  Umemuona mtoto halisia wa Mwl. Nyerere kwenye picha ya juu ambaye alitaka kukupeleka mahakamani kwa utaperi wa kutumia jina la Baba yake.

  Huyo ndiyo kiboko yako, hakutaka uendelee KULINAJISI jina la baba yake mzazi.
   
 7. o

  obeid666 JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2013
  Joined: Nov 19, 2012
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi ingetokea kwamba wamefika hapo kaburini halafu Nyerere akafufuka wangemwambia wameenda kufanya nini hapo kwake? Make Tanzania aliyowaachia sio ilivyo sasa hivi,Katibu mkuu wa ccm anamaliza Tembo woote Tanzania,Nape mropokaji asiye na mfano,hajui anachokiongea ili kudanganya Watanzania wameamua kufanya maigizo ili ionekane walikwenda kuzuru kaburi la Nyerere,angefufuka akawakuta hao watu wako hapo asingeamka ANGEKUFA TENA kulikoni kuonana na watu wachafu hao
   
 8. Supervisor

  Supervisor JF-Expert Member

  #8
  Sep 22, 2013
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 553
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Zome zomea ndo dawa yao hao. Najua hata Familia ya Mwalimu inawaonea haya tu lakni wangemzomea Kinana kwa kumaliza Tembo wetu. Shame on you Gambaz..
   
 9. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #9
  Sep 22, 2013
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 15,990
  Likes Received: 3,175
  Trophy Points: 280
  Ningeshangaa sana usingechangia kauli ya aina hii,

  Ni vigumu kuugeuza mcha kuwa usiku na usiku kuwa mchana,

  Yericko "NYERERE" ni yule yule wa juzi, jana, leo na mpaka kifo chake chini ya Jah!

  Lakini MwanaDiwani/Nape wa sasa si huyu wa kesho bali tumbo lake tu ndio linaamua aweje siku hiyo!
   
 10. MwanaDiwani

  MwanaDiwani JF-Expert Member

  #10
  Sep 22, 2013
  Joined: Mar 22, 2013
  Messages: 5,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Ningeshangaa sana kama Yericko Yohanes Msambila 'Nyerere' angebadilika kwa sababu tafiti zinabainisha kuwa TAPELI au MWIZI huwa habadiliki bali HUJIGEUZA sura ya mwonekano ili aendelee kufanikisha utapeli na wizi wake.

  Tapeli Yericko " NYERERE" ataendelea kutapeli kama alivyofanya juzi, jana, leo na mpaka kifo chake chini ya shetani.
   
 11. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #11
  Sep 22, 2013
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 15,990
  Likes Received: 3,175
  Trophy Points: 280
  CCM wanajivunia sana uwepo wa Mwenge, Faida yake kuu ni kuzaliwa PAKA SHUME mmoja ambae ni kilaza maarufu wao na mpiga domo wa Lumumba, kwa hili hakika ccm lazima waulinde mwenge na kuuenzi kwa nguvu zote na kutembea vifua mbele mataako nyuma!

  Heko MwanaDiwani katibu msema HOVYO wa viunga vya Lumumba!
   
 12. MwanaDiwani

  MwanaDiwani JF-Expert Member

  #12
  Sep 22, 2013
  Joined: Mar 22, 2013
  Messages: 5,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Yericko Yohanes Msambila,

  Umesahau kusema mwasisi wa mwenge wa uhuru 1966 ni baba wa Taifa ambaye kwa fikra zako za KISHETANI ulipenda awe baba yako mzazi kwa sababu katika fikra zako, Marehemu Mzee Yohanes Msambila hakufaa kuwa baba yako na pia mama yako alifanya makosa kuolewa na Marehemu Mzee Yohanes Msambila na wakapata mtoto waliyemuita Yericko Yohanes lakini yeye kwa sasa anajiita Yericko Nyerere.
   
 13. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #13
  Sep 22, 2013
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,717
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  1098448_158784690991774_1397186238_n.jpg
   
 14. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #14
  Sep 22, 2013
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 15,990
  Likes Received: 3,175
  Trophy Points: 280
  Bregedia amekwenda kaburini na kihoro kwakulea PAKASHUME asiewake kisa mwenge,

  Na amekufa akiulaani mwenge kwakuwa ndio uliomletea huo msukule unaotumiwa na ccm,

  Familia ya marehemu afande hawakutaki, Familia ya Mack hawakutambui, umekuwa kama dodoki la bafuni tu tena bafu la kizaramo!
   
 15. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #15
  Sep 22, 2013
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 16,864
  Likes Received: 9,699
  Trophy Points: 280
  Asante Yericko Nyerere, umenifumbua macho.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #16
  Sep 22, 2013
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 16,864
  Likes Received: 9,699
  Trophy Points: 280
  Huyu mwanadiwani anatujazia seva na mapicha yake yasiyo na tija. MOD angalieni jinsi ya kutupatia utulivu jukwaani dhidi ya huyu mgagagigikoko.
   
 17. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #17
  Sep 22, 2013
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,109
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hii ipo chini ya kiwango cha Great Thinker! vipi ziara ya Dr. Slaa Marekani, bado inakusababishia vichomi?
   
 18. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #18
  Sep 22, 2013
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 15,990
  Likes Received: 3,175
  Trophy Points: 280
  Nape anaweweseka, anataka kuleta mambo ya kichokoraa, anarusha mawe huku kasahau yupo kwenye nyumba ya vioo,
   
 19. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #19
  Sep 22, 2013
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 15,990
  Likes Received: 3,175
  Trophy Points: 280
  Namsubiri aendelee kuropoka tu nimpe vitasa vya uhakika mpaka aione jf chungu,
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #20
  Sep 22, 2013
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,069
  Likes Received: 3,438
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na ww Yericko!Mikono ya Kinana haitakiwi kuligusa kabuli la Baba wa Taifa!Kinana ni najisi.
   
Loading...