Katibu Mkuu wa CCM (Dr. Bashiru Ally) nakuhakikishia hakuna atakayejitokeza kuonesha kukerwa na kauli yako; sote tunajua kuwa huo ndiyo ukweli

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Dr. Bashiru, nakusalimu kwa mara nyingine-mara hii kupitia hapa Jamii Forums baada ya ile salamu ya kiofisi asubuhi. Najua wajua kuwa Katibu Mkuu wa chama ni mtu na kiongozi mkubwa. Kwa mfumo wa kisiasa (kwa uelewa wa wengi), Katibu Mkuu wa CCM ni Zaidi ya Waziri Mkuu. Katibu Mkuu wa CCM, kama ulivyo wewe, ana nguvu na ushawishi mkubwa chamani.

Kauli ya Katibu Mkuu si ya kuibeza. Kauli ya Katibu Mkuu ni kauli ya chama. Ni kauli inayoanika ukweli, uchambuzi na mtazamo wa kichama juu ya jambo. Ni kauli inayopaswa kuchukuliwa na kufanyiwa kazi na watendaji wote wa Serikali inayoundwa na chama husika. Si kauli ya mchezomchezo. Nilipokuwa nikisomea siasa, nilifundishwa kuwa unapokuwa kiongozi mkubwa unapaswa kuwa makini na kauli zako. Ni rahisi mno kwa wasikilizaji kuchukua kauli zako.

Kauli yako Dr. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wetu wa CCM Taifa, kuhusu wananchi kupoteza Imani na mfumo mzima wa kiuchaguzi ni kauli thabiti na ni ukweli wenyewe. Kuanzia chamani hadi Serikalini, sote tunajua. Tunajua kuwa mfumo wa kiuchaguzi uliopo sasa umepoteza ladha na kupoteza kuaminika. Wananchi wanaona matendo na kusikia maneno ya watendaji wa mfumo wa kiuchaguzi. Wanaona jinsi wanaopaswa kushinda wanavyoshindwa; wanaopaswa kushindwa wanavyoshinda.

Wapigakura wanajionea kwa macho yao jinsi CCM yetu inavyobebwa na kutangazwa kushinda hata tunaposhindwa. Wanajionea jinsi 'mfumo' unavyowabeba CCM na kuwafanya wawe na uhakika wa kushinda kwa vyovyote vile. Uhakika hutufanya CCM kujiamini na kuwadharau wapinzani wetu hata bila maandalizi ya kutosha ya kiuchaguzi. Uhakika hutufanya tuwe na nyodo na kutojali uwepo wa demokrasia thabiti hapa nchini. Uhakika hutupa jeuri na kiburi ambacho si kizuri.

Kwa kauli yako, nakuhakikishia kuwa hatajitokeza kada hata mmoja wa CCM hadharani (kama ulivyosihi iwe) kukupinga au kutaka ufafanuzi. Huo ndiyo ukweli ambao kwa bahati mbaya au nzuri chama kimeusema hadharani kupitia wewe Katibu Mkuu wetu. Wananchi wanakuwaje na Imani na mfumo wa kiuchaguzi ikiwa Tume ya Uchaguzi ni ya kichama na huundwa na Mwenyekiti wetu? Wananchi hufurahia tu posho, takrima, muziki na burudani/fursa nyinginezo wakati wa uchaguzi. Siku ya kupiga kura, kwakuwa washindi huwa wameshajulikana, hawaendi kupiga. LAKINI, KURA ZAO HUPIGWA!

Dr. Bashiru Ally, uwe na Amani. Msimamo wako ni msimamo wa chama!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Dr Bashiru kama katibu wa chama ni mtu makini sana, lakini bahati mbaya anafanya kitu ambacho kwa wakati na sehemu au aina ya uongozi wa ccm usio sahihi kwa sasa.

Ccm hawatakubali, kwa maana wapo tayari kwa namna yeyote washinde uchaguzi na kuufifisha upinzani,
Wao wanaamini upinzani utakufa but sio kweli, upinzani wa kwl unaendelea kubaki kwenye mioyo ya watu hata bila mbunge mmojo kurudi bungeni 2020! njia alizotumia Kinana zilikuwa sahihi kuijenga Ccm pole kwao kwa kumpoteza.
 
Dr. Bashiru, nakusalimu kwa mara nyingine-mara hii kupitia hapa Jamii Forums baada ya ile salamu ya kiofisi asubuhi. Najua wajua kuwa Katibu Mkuu wa chama ni mtu na kiongozi mkubwa. Kwa mfumo wa kisiasa (kwa uelewa wa wengi), Katibu Mkuu wa CCM ni Zaidi ya Waziri Mkuu. Katibu Mkuu wa CCM, kama ulivyo wewe, ana nguvu na ushawishi mkubwa chamani.

Kauli ya Katibu Mkuu si ya kuibeza. Kauli ya Katibu Mkuu ni kauli ya chama. Ni kauli inayoanika ukweli, uchambuzi na mtazamo wa kichama juu ya jambo. Ni kauli inayopaswa kuchukuliwa na kufanyiwa kazi na watendaji wote wa Serikali inayoundwa na chama husika. Si kauli ya mchezomchezo. Nilipokuwa nikisomea siasa, nilifundishwa kuwa unapokuwa kiongozi mkubwa unapaswa kuwa makini na kauli zako. Ni rahisi mno kwa wasikilizaji kuchukua kauli zako.

Kauli yako Dr. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wetu wa CCM Taifa, kuhusu wananchi kupoteza Imani na mfumo mzima wa kiuchaguzi ni kauli thabiti na ni ukweli wenyewe. Kuanzia chamani hadi Serikalini, sote tunajua. Tunajua kuwa mfumo wa kiuchaguzi uliopo sasa umepoteza ladha na kupoteza kuaminika. Wananchi wanaona matendo na kusikia maneno ya watendaji wa mfumo wa kiuchaguzi. Wanaona jinsi wanaopaswa kushinda wanavyoshindwa; wanaopaswa kushindwa wanavyoshinda.

Wapigakura wanajionea kwa macho yao jinsi CCM yetu inavyobebwa na kutangazwa kushinda hata tunaposhindwa. Wanajionea jinsi 'mfumo' unavyowabeba CCM na kuwafanya wawe na uhakika wa kushinda kwa vyovyote vile. Uhakika hutufanya CCM kujiamini na kuwadharau wapinzani wetu hata bila maandalizi ya kutosha ya kiuchaguzi. Uhakika hutufanya tuwe na nyodo na kutojali uwepo wa demokrasia thabiti hapa nchini. Uhakika hutupa jeuri na kiburi ambacho si kizuri.

Kwa kauli yako, nakuhakikishia kuwa hatajitokeza kada hata mmoja wa CCM hadharani (kama ulivyosihi iwe) kukupinga au kutaka ufafanuzi. Huo ndiyo ukweli ambao kwa bahati mbaya au nzuri chama kimeusema hadharani kupitia wewe Katibu Mkuu wetu. Wananchi wanakuwaje na Imani na mfumo wa kiuchaguzi ikiwa Tume ya Uchaguzi ni ya kichama na huundwa na Mwenyekiti wetu? Wananchi hufurahia tu posho, takrima, muziki na burudani/fursa nyinginezo wakati wa uchaguzi. Siku ya kupiga kura, kwakuwa washindi huwa wameshajulikana, hawaendi kupiga. LAKINI, KURA ZAO HUPIGWA!

Dr. Bashiru Ally, uwe na Amani. Msimamo wako ni msimamo wa chama!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Hizi porojo peleka tu huko huko nyumbani ufipani kujifanya mwanalumumba
 
Uliwahi kuwashauri ndugu zako na wanaccm wenzako kuwa wajifunze kula na kipofu,nadhani baada ya kauli ya dr Bashiru watakuwa wamekuelewa!
 
Hahahaaa chichiem bwana ni watu wa ajabu, hivi unafurahiaje ushindi wa kutemgeneza
 
Ukweli daima hujitenga na udhalimu.Shetani huwapa wafuasi wake mafanikio ya bandia kwa Muda mfupi kisha anawafanya mbaya.
 
Lakini huyu Dr Bashiri si huwa anashiriki kwenye vikao vya kuwapitisha waliounga mkono juhudi za Rais bila kura za maoni?

Na yeye ni sehemu ya wanafki tu.
 
Anajaribu kuwafanya watz wajinga, ila shoka liko shinani, kama hutalipa hapa duniani,, shoka la mwammu wa ukweli linawasubiri.

Back
Top Bottom