The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 603
- 1,760
Hivi juzi pale mkoani Morogoro, wakati Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally akiwa ziarani kwa siku tatu kwa ajili kukagua utekelezaji wa ilani ya chama chake, kwenye mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Mikese, ilibainika uwepo wa ujenzi wa jengo jingine la mapokezi linalojengwa kwa fedha za fidia ya SGR kufuatia kubomolewa kwa zahanati ya Mikese kupisha ujenzi wa reli ya mwendokasi, ujenzi ambao haujalingana na thamani ya fedha iliyotolewa.
Dk. Bashiru Ally alimuagiza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Ole Sanare kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini gharama halisi iliyotumiwa na Kampuni ya Reli ya Mwendokasi (SGR) kwenye ujenzi wa kituo cha afya Mikese kutokana na uwepo wa ubadhirifu wa milioni 300.
Je, Katibu Mkuu wa chama ana mamlaka ya kumtuma, kumwamuru, kumuamrisha RC suala hilo?