Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally kuongea na Mabalozi tarehe 15 Oktoba 2020

Amani Msumari

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
1,830
976
Tarehe 15 Oktoba, 2020, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, atakutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Mazungumzo hayo yatafanyika Ofisi Ndogo za Makao Makuu Lumumba jijini Dar es salaam kuanzia mida ya saa nne asubuhi.

Vyombo mbalimbali vya habari vinaalikwa kufuatilia na kuhabarisha Umma katika mazungumzo hayo.

Imetolewa na;
Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
14 Oktoba, 2020

==========
UPDATE:

Mabalozi wameanza kufika ofisi ndogo za CCM, Lumumba

38E3C75F-C140-41C9-A401-B10F15FAB141.jpeg

B4EC605C-4D77-4D1A-AAF4-786523F111F1.jpeg

7F1CDC49-7E1E-49BD-AD70-93DCF5E20BF7.jpeg

F8BF09B8-2A29-4078-8D51-C260C46645C0.jpeg

EA749374-C4FC-4EFE-BFDD-57F30F8CAF21.jpeg


👆🏽Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amempokea Balozi wa Marekani Tanzania Dkt. Donald J. Wright ambaye amefika katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM), Lumumba jijini Dar es Salaam.
 
Hawa CCM wana Akili Sana Moves zao zina impact kubwa kwenye kuwaletea Ushindi

Lakini Hata hivyo CCM watashinda No way Hata tufanyaje yani

Najua Mtanitukana hapa
Lahaula
Tunaenda kuliziba tundu kwa kujaza ukweli na kuliwekea mfuniko mzito na hatimaye kulifunga kwa makufuli
Haha
Daah we jamaa huogopi kupigwa humu

Sasa hivi utaambiwa Huna akili, Wasted Sperm, Buku 7, Mbumbumbu nk Subiri uone
My blazaz mmenishinda🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Ukikaa bandari usiogope honi za meli ila kiukweli kesho hawa jamaa zetu wanaenda kupata kipigo cha mbwa Koko. Tutawajuza waheshimiwa mabalozi Kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi kwa facts & figures
Halafu tutawaambia ambia na ndugu zenu huko nyumbani kuwa hapa kila kitu kipo mahali pake. CCM ina magwiji wa siasa. Tulikuwa tunamuangalia tuu Mr. Much Know akijiona kamaliza kumbe tunamuandalia roba ya mbao vile comrade Bashiru anaongea polepole kila neno litapenya kwenye ngome za masikio ya mabalozi
 
Kuna watu sijui ilikuwaje wakazaliwa.
Imagine CCM ilivyowafukarisha Watanzania kwa miaka 60 sasa lakini hawalali usiku kucha kuhakikisha CCM haiondoki madarakani
Fanya kazi Acha kukaa maskani kucheza pool table, hakuna chama kinachompa mtu utajiri, wakaa maskani wengi wanadhani upinzani ukishika dola ndio watapewa mabegi ya hela, mmoja wapo ni wewe pole sana
 
Kuna watu sijui ilikuwaje wakazaliwa.
Imagine CCM ilivyowafukarisha Watanzania kwa miaka 60 sasa lakini hawalali usiku kucha kuhakikisha CCM haiondoki madarakani
Diamond, Kiba, Lady Jay Dee, Samatta ni wanaijeria?

Mzee Bakhressa, Mo, Manji, etc n wachina?

Sikiliza, njoo tuongee Kuhusu fursa za Kilimo na ufugaji ili uache kulalamika umtukuze Mungu.

NB: masikini hata Marekani wapo, muhimu ni kazi nzuri inayofanywa ya kutengeneza mazingira ya kuwawezesha watanzania kujikwamua. Tufanye kazi kwa bidii.
 
Ngoja tusikie 'vingereza' vya PhD za sisiem! Mgombea wetu kawakwepa?
 
Back
Top Bottom