Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ali aanza na mguu wa kushoto

Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,523
4,991
Namfahamu Bashiru Ali kama mjenga hoja mashuhuri, anayeelewa vema eneo lake la Sayansi ya Siasa. Ni mchambuzi mzuri sana. Lakini kuna tofauti kubwa sana kati ya Mwanasiasa na Mchambuzi wa siasa. wakati Mwanasiasa anajishughulisha na mambo ya papo kwa papo, "real time", anahitajika kufanya maamuzi ya papo kwa papo, kwa kufikiri haraka. Mchambuzi anao muda wa kuchambua na kufanya rejea. Pia mchambuzi anayo ile starehe ya kusema "tumpe muda kwanza". Mwanasiasa hana starehe hiyo. Pia "Uanasiasa" ni kipaji ambacho mtu anazaliwa nacho, ingawa kusoma kunasaidia.

Kwa hiyo, kufaulu au kutofaulu kwa Bashiru kutategemea zaidi karama zake, kabla ya kujumuisha taaluma yake. lakini pia itategemea umakini wake, na utayari wake kuzingatia "best practices" za mwanasiasa. na katika hili, tayari naona Bashiru ameshaanza kuingia mkenge. inabidi achukue tahadhari.

Mkenge alioingia ni kuendeshwa na matukio, wakati yeye ndiyo anahitaji kuendesha matukio. Kwa sasa hahitajiki kutoa kauli zozote zinazomfunga katika mwelekeo fulani, bali kauli jumla jumla ambazo zinampa nafasi ya kujipanga na kusoma mazingira. Bashiru alitakiwa kueleza kama atakuwa tayari, au kama anao uwezo, wa kukabiliana na siasa za majukwaa. Kabla ya hapo, alisema vizuri kabisa kwamba yeye atakuwa mtu wa kutumia VIKAO. Atatoa taarifa za vikao, siyo maoni au matamko ya kukurupuka. Lakini kwa hili la siasa za majukwaa, tayari amejifunga kwa kauli yake kwamba watu wa kuteuliwa kama yeye hawatakiwi kusimama majukwaani. hapo tayari kajifunga. Lakini mbaya zaidi akatoa agizo, kwamba makatibu wote hawatakiwi kusimama majukwaani kufanya siasa. Sasa hilo agizo limetolewa na KIKAO gani? maana yeye amesema kwamba atakuwa anaongelea maamuzi ya vikao!

Isitoshe, Bashiru ni Katibu Mkuu wa Chama cha Siasa. sioni kwa vipi akwepe kufanya siasa. nitaelewa kama MHASIBU MKUU wa CCM, hatapanda jukwaani. hilo linaeleweka. Lakini Katibu Mkuu, au makatibu wengine, hata kama hawatalazimika kupanda majukwaani au kufanya siasa, lakini hakuna haja ya kuwazuia kwa amri. wawe huru kufanya kutokana na mahitaji ya wakati na hali halisi, na karama zao. Tulimwona Kinana akipanda majukwaani mara kadhaa, na alifanya hivyo kwa mafanikio makubwa sana.

Wengine wanaweza kutafsiri kauli ya Bashiru kuwa inatokana na woga wa jukwaa. maana mhadhiri amezoea jukwaa la darasani, ambapo yeye ndiye anayemiliki kila kitu, na wasikilizaji wake ni watu wenye ujuzi fulani. wala hakuna atakayeripoti kwenye vyombo vya habari yale anayozungumza. lakini katika jukwaa, wasikilizaji ni watu wa aina tofauti. unasikilizwa na vyombo vya habari. unachosema kinaweza kutumika popote na wakati wowote dhidi yako. inahitaji uzoefu fulani na karama fulani.

Mkapa mwanzoni aliandikiwa machache ya kuongea jukwaani. alikuwa anasoma tu kwenye karatasi. baada ya mwaka na ushee, akazoea. japo ni kwa kufoka foka, lakini anaeleweka. Bashiru atumie uzoefu wa wengine. awe tayari kujifunza. ajipe muda wa kujifunza. asitoe kauli za kujifunga na pia kuonekana kuendeshwa na matukio.

Bahati nyingine mbaya ni kwamba Mwenyekiti wake siyo mwanasiasa. wote wawili sio "wananzengo" wa CCM. hawana mizizi, kama akina Nape na Kikwete. mbaya zaidi ni kwamba Mwenyekiti ana ka tabia ka kutoa maamrisho na matamko akitokea Ikulu, tena kwa kumtumia msemaji wake wa ikulu. anaweza kufanya maamuzi kutokea huko na kumwacha katibu wake mkuu akiwayawaya. ajiandae namna nzuri ya kufanya kazi na mtu wa aina hii. aufiche kabisa udaktari wake wa siasa, awe kama polepole, "ndiyo mzee", tena kwa kusujudu. hapo angalau ataanza vema.
 
Siku tukijua kwanini Makao Makuu ya Nchi yalipelekwa palipo na Hospitali kuu ya Wagonjwa wa vichwa, tutagundua maneno ya Mh. Mkosamali yalimaanisha nini!
Ukimchukua mtu mwenye akili zake ukampeleka FISIEMU kwishnehi! hakuna kitu tena GIGO
 
Kuna wasomi na watu makini wengi sana wameenda na maji katika awamu hii mfano

Dr ayoub rioba

Dr kitila mkumbo

Dr bashiru Ali

Hata haka chakubanga kalikuwa mtu makini sana



Magu kawaweza sana aisee kawapa vyeo wako tulii kama maji mtungini.

Ukiwa unakula usiongee

Mchawi mpe mwanao.

Daaah
 
Umesahau Alikuwa mbunge kwa zaidi ya miaka 20. Sio mwanasiasa kwa maana gani? Kwani wanasiasa wanapatikana wapi?
anaonekana tu siyo mwanasiasa:
1) mwenyewe kasema mara nyingi kwamba siyo mwana siasa
2) Ni mtu wa mwisho kwa wenyeviti wote wa CCM taifa kwa sifa ya uanasiasa. anazidiwa hata na Mkapa ambaye alionekana wazi kwamba siyo mwanasiasa. hatumii siasa. anatumia decree na vitisho. anatumia dola.
3) mwanasiasa haogopi wanasiasa. huyu anaogopa wanasiasa kiwango cha kufa mtu. kafunga bunge live, hataki wapinzani wafanye hata vikao vya ndani tu!!!!
4) hiyo ya kuwa mbunge au waziri miaka 20 siyo tatizo. chura pia anaishi ndani ya maji lakini huwezi kusema kwamba ni msafi
5) hajui wala hajali taratibu za kisiasa. anachanganya ikulu, serikali, CCM, Lumumba, vyote katika mchanyato mmoja. matokeo yake hata sijui kinatokea nini. mwenyewe pia hajui na hajali.
 
Huwa nashangaa mtu akisema JPM sio mwanasiasa. Angefikaje huko alikofika kama sio mwana siasa. Afadhali mtu aelezee mapungufu yake kama mwana siasa tuyajue. Sasa kama si mwanasiasa ni nani?
 
Siku tukijua kwanini Makao Makuu ya Nchi yalipelekwa palipo na Hospitali kuu ya Wagonjwa wa vichwa, tutagundua maneno ya Mh. Mkosamali yalimaanisha nini!
Ukimchukua mtu mwenye akili zake ukampeleka FISIEMU kwishnehi! hakuna kitu tena GIGO[/QUOTE Dah let me laugh Bro, siyo kwa jiwe hilo ‍♂️‍♂️‍♂️
 
Back
Top Bottom