Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,188
Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally, akiongea jijini Dodoma jana wakati wa kufunga Kikao cha Baraza la Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), amewaonya Makada wa Chama hicho walioanza mbio za kusaka urais, akisema Chama hicho hakitamvumilia kiongozi yeyote kutumia muda, rasilimali za Serikali kwa lengo la kusaka na kuendesha makundi ndani ya Chama hicho.
Tuna Chama kimoja na Rais mmoja, kusaka urais kabla ya muda huko ni kujishushia sifa. Kila mmoja jina lake tunalo, kipindi kikifika tutasema wapi walipokutana na muda ukifika tuta-print na tutawaonyesha."
Dk. Bashiru alikumbushia maneno aliyoyasema pia akiwa huko Zanzibar hivi karibuni wakati alipokwenda kujitambulisha: "Cheo hiki (urais) ni cha watu wote, si mtu kujipitisha. Urais si wa mapambo ni sifa na ikumbukwe kuwa mtu anayefaa kuwa Rais anaombwa."
Vilevile, Bashiru aliongelea juu ya uwepo wa makundi ndani ya Chama na kukiri kuwa hali si shwari kwani kuna viashiria vya makundi. Alisema kuwa, Ndani ya CCM kuna maovu yanayoendelea na yaliyokuwa yakifanyika na kusababisha makundi. Maovu hayo ni:
- Makundi ya Uchaguzi.
- Kutosimsmia Muungano.
- Utovu wa nidhamu.
- Kukosekana kwa umoja ndani ya Chama na (kati ya) Viongozi wa Chama na Serikali.
Hali ya Watia nia wa kuwania urais mwaka 2015 ya ku-keep "low profile" inawezekana haijawasaidia the way walivyotaka kwani kila kukicha, equilibrium inazidi kuwatupa mkono na now they feel as if they keep being marginalized every how and then.
Cha ajabu Watia nia wengi wa mwaka 2015, wame-struggle kiutendaji katika Serikali ya Awamu ya Tano, licha ya baadhi yao kuwa katika nafasi za kuwafanya waonekane. Hali hiyo imetoa room ya kuibuka kwa Makada wengine wapya ambao waliojaza vacuum ya utii (kwa Rais) na ya kiutendaji iliyoonyeshwa na baadhi ya Watia nia wa 2015.
Hivyo, kwa hofu ya kupotezwa kisiasa na Siasa za Awamu ya Tano, Makada hao ndio maana wameanza mapema kuunda mitandao yao mapema.
Ni akina nani walengwa hapa wanaotumia rasilimali za Serikali kusaka urais?