Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo apongeza Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
664
829
CHONGOLO AWAPONGEZA UMOJA WA WANAWAKE TANZANIA (UWT)

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo amewapogeza Jumuiya ya umoja wa wanawake Tanzania (UWT) kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na kuandikisha wanachama wapya, kuhimiza wanachama kulipa ada na kubuni miradi mbalimbali ya kiuchumi.

Katibu Mkuu ametoa pongezi hizo akiwa mgeni rasmi katika kikao cha kawaida cha Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) lililofanyika leo tarehe 20 Disemba, 2021 Makao Makuu ya Chama jijini Dodoma.

Katibu Mkuu ameeleza kuwa, Maeneo hayo matatu kwa CCM ni muhimu sana, bila hayo hakuna Chama wala Jumuiya, kwani bila kuingiza wanachama wapya maana yake waliopo wataendelea kupungua, bila kuwa na msingi imara wa uchumi jumuiya itakuwa ombaomba na bila kujenga uhai wa jumuiya hatutakuwa na jumuiya imara na yenye nguvu ya kusimamia maslahi ya wanawake nchini.

Aidha, UWT kupitia kwa Mwenyekiti wake Taifa Ndg. Gaudensia Kabaka, imetoa tamko la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuunda kamati maalum ya kumshauri kuhusu masuala ya usawa wa kijinsia, ambapo itasaidia katika kufikia malengo ya hamsini kwa hamsini katika fursa mbalimbali.

Katika hatua nyingine, Makamu Mwenyekiti wa Uwt Zanzibar Ndg. Thuwaiba Kisasi amesisitiza kuwa, wanawake wataendelea kusimama kidete katika kusimamia maslahi ya wanawake wote nchini na ya Chama Cha Mapinduzi.

Kikao hicho za kawaida, kimehudhuriwa pia na baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa akiwemo Katibu wa NEC, Oganaizesheni Ndg. Maudline Castico na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Dkt. Edmund Mndolwa.

Imetolewa na;

Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
 

Attachments

  • VID-20211220-WA0094.mp4
    4.7 MB
  • Thanks
Reactions: Lee

Similar Discussions

Back
Top Bottom