Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo afanya mazungumzo na Zitto Kabwe

Kadhi Mkuu 1

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
11,162
2,000
"Zitto pia alipongeza ukuaji wa uchumi na demokrasia hapa nchini"

Huyu huyu alielia juzi kufanyiwa rafu Zanzibar mpaka jamaa wa CCM akajitoa au Zitto mwingine?!

Nina wasiwasi na hiyo nukuu hapo juu, inawezekana mleta mada umeikosea, tazama tena rekodi zako.
Huwezi kukubali wewe pingapinga fc.
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
49,614
2,000
"Zitto pia alipongeza ukuaji wa uchumi na demokrasia hapa nchini"

Huyu huyu alielia juzi kufanyiwa rafu Zanzibar mpaka jamaa wa CCM akajitoa au Zitto mwingine?!

Nina wasiwasi na hiyo nukuu hapo juu, inawezekana mleta mada umeikosea, tazama tena rekodi zako.
yule ni CCM full
 
Duplicate_90

JF-Expert Member
Mar 29, 2020
251
500
Ccm walitaka tu hyo picha na zitto na wameigharamia fedha nyingi ili mabeberu waone kuna demokrasia...
 
Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,363
2,000
Kama huwawezi jiunge nao au mnaupinga usemi wetu mkuu wa kiswahilia,sijaona tatizo ikiwa wengine waliomba kwenda Ikulu kfungua kibaraza cha kahawa na watawala hatimae mnajua kinachoendelea serikali kasweka jela mwenyekiti.
 
RAISI AJAE

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
2,247
2,000
zito anajiandaa kuwa kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni 2025-30!! Na anajua hatma ya Mbowe!!!kikwete alimuandaa zito kuiua Chadema kupitia ACT!!!MISSION ACOMPLISHED!!!
 
The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
13,376
2,000
"Zitto pia alipongeza ukuaji wa uchumi na demokrasia hapa nchini"

Huyu huyu alielia juzi kufanyiwa rafu Zanzibar mpaka jamaa wa CCM akajitoa au Zitto mwingine?!

Nina wasiwasi na hiyo nukuu hapo juu, inawezekana mleta mada umeikosea, tazama tena rekodi zako.
Nafikiri Maza atakuwa anataka kumshirikisha kwenye serikali yake.....!!
 
Jaminati

Senior Member
Feb 18, 2021
178
250
Zitto siku ya leo tarehe 8.09.2021 amefanya mazungumzo na ndugu katibu mkuu wa CCM ndugu Daniel Chongolo kwa niaba ya CCM.

Mazungumzo hayo yaiyodumu kwa zaidi ya masaa 7 yalijadili vitu vingi ikiwemo ushirikiano baina ya vyama vyao. Zitto pia alipongeza ukuaji wa uchumi na demokrasia hapa nchini.

Taarifa zaidi inafuata

View attachment 1929653
ZT ccm damu
 
Trillion

JF-Expert Member
Apr 24, 2018
2,348
2,000
"Zitto pia alipongeza ukuaji wa uchumi na demokrasia hapa nchini"

Huyu huyu alielia juzi kufanyiwa rafu Zanzibar mpaka jamaa wa CCM akajitoa au Zitto mwingine?!

Nina wasiwasi na hiyo nukuu hapo juu, inawezekana mleta mada umeikosea, tazama tena rekodi zako.
Haaa haa just haaa haa..! CCM ndivyo walivyomwandikia Zito cha kusema.😄
Rejea vikaratasi vya waunga juhudi kina Katambi zilivyokua zinatolewa na Polepole,

Zitto alitaka kutuuza CHADEMA, akashindwa.
Lipumba akafanikiwa kuiuza CUF.
 
  • Love
Reactions: BAK

kipara20

JF-Expert Member
Jul 30, 2021
875
1,000
Zitto kakutana na katibu mkuu wa ccm kwa cheo chake cha mwenyekiti mpya wa TCD (Tanzania centre for democracy) na ameshatembelea ofisi za chadema na nccr mageuzi

Zitto siku zote anatumika kwa masrahi ya watawala ni ngumu sana kumuamini zitto,
 
kipara20

JF-Expert Member
Jul 30, 2021
875
1,000
zito anajiandaa kuwa kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni 2025-30!! Na anajua hatma ya Mbowe!!!kikwete alimuandaa zito kuiua Chadema kupitia ACT!!!MISSION ACOMPLISHED!!!

Chadema haitokufa leo wala kesho kila aliyejaribu kuiuwa chadema alikufa yeye, ( MEKO)
 
Gift mzalendo

Senior Member
Dec 13, 2019
139
250
Ayatollah Zitto ni msaliti sasa maccm yameanza kumtumia wazi wazi. ACT Wazalendo
Aliopokutana na katibu wa CDM Mnyika hakuwa msaliti , Leo kukutana na katibu was ccm ndo usaliti?
Hizi fikra za usaliti kwa kila mtu ni za kijinga tuachane nazo zitadumaza akili za viongozi wa upinzani washindwe kutafuta mbinu mbadala za ushindani
Fikiri ndo mmepewa madaraka alafu kila anaetofoutiana na nyie ni msaliti , si mtawawaliza wapinxani wenu
Tubadili mbinu na mitazamo kama tunajiandaa kupokea serikali
 
majege

Senior Member
May 3, 2009
136
225
KATIBU MKUU WA CCM DANIEL CHONGOLO AFANYA MAZUNGUMZO NA ZITTO KABWE

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo amefanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Ndg. Zitto Kabwe.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 08 Septemba, 2021 Makao Makuu ya CCM Dodoma, ambapo Ndg. Zitto aliambatana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Ndg. Lawrence Malawa.

Pamoja na mambo mengine, Mazungumzo hayo yamelenga zaidi kujitambulisha kwa Mwenyekiti mpya wa TCD Ndg. Zitto Kabwe alieyechaguliwa mwezi Agosti mwaka huu.

Imetolewa na;

Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

Ananikumbusha ya Mongosutu Buthelezi wakati ANC na makundi mengine yakipigania uhuru yeye alikuwa aki-sneak behind na kushirikiana na Makaburu kuwajumu waafrika wenzake. Hizo ni roho za kibinafsi na kutaka kutumia advantage ya kupata madaraka kwa kutumia mgongo wa CHADEMA ndiyo maana kila siku unamuona ni kigeugeu. Kilichopo kichwani kwake yeye ni Cheo na hana falsafa anayoisimamia ambayo unaweza kusema ameiuza kwa wananchi na wameielewa. Mkakati wake muda wote ni kutafuta mahali penye ombwe la uongozi au ombwe la mfumo wa kufanya siasa basi yeye ndiyo anaingia hata kama kwa macho ya kawaida inaonekana ni kujidhalilisha yeye huwa hajali.
 
Lihove2

JF-Expert Member
Mar 23, 2018
2,365
2,000
KATIBU MKUU WA CCM DANIEL CHONGOLO AFANYA MAZUNGUMZO NA ZITTO KABWE

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo amefanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Ndg. Zitto Kabwe.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 08 Septemba, 2021 Makao Makuu ya CCM Dodoma, ambapo Ndg. Zitto aliambatana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Ndg. Lawrence Malawa.

Pamoja na mambo mengine, Mazungumzo hayo yamelenga zaidi kujitambulisha kwa Mwenyekiti mpya wa TCD Ndg. Zitto Kabwe alieyechaguliwa mwezi Agosti mwaka huu.

Imetolewa na;

Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

Zitto alialikwa na CCM kama kiongozi mwandamizi wa TCD au?
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
24,677
2,000
mambo si mambo zenji.... CCM wameona wakae mezani tena kutafuta muafaka ndani ya muafaka.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom