Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo afanya mazungumzo na Zitto Kabwe

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
257
500
KATIBU MKUU WA CCM DANIEL CHONGOLO AFANYA MAZUNGUMZO NA ZITTO KABWE

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo amefanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Ndg. Zitto Kabwe.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 08 Septemba, 2021 Makao Makuu ya CCM Dodoma, ambapo Ndg. Zitto aliambatana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Ndg. Lawrence Malawa.

Pamoja na mambo mengine, Mazungumzo hayo yamelenga zaidi kujitambulisha kwa Mwenyekiti mpya wa TCD Ndg. Zitto Kabwe alieyechaguliwa mwezi Agosti mwaka huu.

Imetolewa na;

Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

IMG-20210908-WA0128.jpg

IMG-20210908-WA0124.jpg

IMG-20210908-WA0125.jpg
 
mmh

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
2,871
2,000
Amechoka kukaa behind scene sasa anataka awe public kabisa.
Huu upinzani wenu huu kwa waliopo mi kwa kweli hapana. Tuvute subiraaa.
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
123,024
2,000
Naam Mkuu huyo mchumia tumbo yuko katika nafasi aliyokuwa anaitafuta sana. Kwenye mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yanayotjwa tajwa inawezekana kabisa akawemo ili kuonyesha tuna “Serikali ya umoja” hivyo kupewa Ubunge kisha kuteuliwa kama naibu Waziri au Waziri kamili.
Ni wakati wake sasa
 
MSAGA SUMU

JF-Expert Member
May 25, 2015
5,461
2,000
Zitto siku ya leo tarehe 8.09.2021 amefanya mazungumzo na ndugu katibu mkuu wa CCM ndugu Daniel Chongolo kwa niaba ya CCM.

Mazungumzo hayo yaiyodumu kwa zaidi ya masaa 7 yalijadili vitu vingi ikiwemo ushirikiano baina ya vyama vyao. Zitto pia alipongeza ukuaji wa uchumi na demokrasia hapa nchini.

Taarifa zaidi inafuata

E-wz4c7XIAEvezM.jpg
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
7,590
2,000
"Zitto pia alipongeza ukuaji wa uchumi na demokrasia hapa nchini"

Huyu huyu alielia juzi kufanyiwa rafu Zanzibar mpaka jamaa wa CCM akajitoa au Zitto mwingine?!

Nina wasiwasi na hiyo nukuu hapo juu, inawezekana mleta mada umeikosea, tazama tena rekodi zako.
 
kipara20

JF-Expert Member
Jul 30, 2021
875
1,000
View attachment 1929653
Zitto siku ya leo tarehe 8.09.2021 amefanya mazungumzo na ndugu katibu mkuu wa CCM ndugu Daniel Chongolo kwa niaba ya CCM.
Mazungumzo hayo yaiyodumu kwa zaidi ya masaa 7 yalijadili vitu vingi ikiwemo ushirikiano baina ya vyama vyao. Zitto pia alipongeza ukuaji wa uchumi na demokrasia hapa nchini.
Taarifa zaidi inafuata

Zitto ni ccm
 
haka kajamaa ni kakinyonga ka kiwango cha lami
 
Relief Mirzska

JF-Expert Member
Jun 13, 2017
12,516
2,000
"Zitto pia alipongeza ukuaji wa uchumi na demokrasia hapa nchini"

Huyu huyu alielia juzi kufanyiwa rafu Zanzibar mpaka jamaa wa CCM akajitoa au Zitto mwingine?!

Nina wasiwasi na hiyo nukuu hapo juu, inawezekana mleta mada umeikosea, tazama tena rekodi zako.
Kwani na nyie juzi juzi si mlilia kwamba Magufuli hafai na Leo mnajidai eti mnamkumbuka na ni Bora kuliko Mama Samia.

Muacheni Zitto afanye siasa za kistaarabu
 
Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
6,903
2,000
Mnamuamini kweli aliyeleta hizi habari? Zitto alienda kujitambulisha kama Mwenyekiti mpya wa TCD na aliongozana na Mtendaji Mkuu wa TCD. Hakwenda kama kiongozi wa ACT. Na kwa yeyote mwenye uzoefu hamna kikao cha masaa saba nje ya vikao vya utendaji. Huu ni uongo mtupu wenye lengo la kumchafulia Zitto.

Amandla...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom