Katibu Mkuu wa CCM aonekana kwenye Kampuni yenye kashfa nzito Tanzania ya OBC (funika kombe Mwanaharamu apite)

Watanzania hatujazaliwa kuwa wajinga muda wote kuna siku watu kama hawa watakuwa wanaongelea gerezani.
 
Mwezi November 2017 Waziri wa maliasili na utalii Dr.Hamis Kigwangala alisema ikifika mwezi Januari mwaka huu (2018), kampuni hiyo itaondoshwa nchini kutokana na kuwa na migogoro isiyoisha na wananchi. Kigwangala alisema OBC haitakuwa sehemu ya kampuni za uwindaji zitakazopewa upya leseni ya uwindaji, kutokana na madai ya uvunjifu wa haki za binadamu, ikiwamo kujihusisha na migogoro wa Loliondo kwa zaidi ya miaka 25.
Hivi yuko wapi huyu vuvuzela!
 
Katibu Mkuu wa CCM akiwa na viongozi wa kampuni ya uwindaji ya OBC. Kampuni hiyo ina tuhuma lukuki ikiwemo kuchoma nyumba za wafugaji wa jamii ya kimasai Loliondo na kuua mifugo yao. OBC wametajwa pia ktk kashfa ya ujangili kwa mwavuli wa uwindaji.
Mmebakia na kuchafua watu tu.
Hivi una habari kwamba Lowassa ana hisa nyingi sana kwenye hiyo kampuni zinazosimamiwa na Mollel?Uliwasiliana nae kabla ya kuja kuharisha hapa.,usije ukakosa posho kwa kuanika kampuni ya bosi wako ukidhani unamchafua kinana
Au umetumwa ujaribu kumtisha Kigwangallah asiishughulie hiyo kampuni kwa mgongo wa kinana?
 
Taratiiiibuuu bosi..
Mbona hasira sana??
 
INAONEKANA KUNA MAMBO HUWA YANAKUWA MAGUMU HATA UWE KAMA JIWE NANMA GANI. MHE. MAGUFULI PAMOJA NA JUHUDI ZOTE NAONA HUKO KWENYE MALIASILI AMEGOMA KABISA KWENDA. HII KAMPUNI KILA MWAKA INA MOGOGORO NA WANANCHI NA RIPOTI NYNGI SANA IMESHATOLEWA KUHUSIANA NA KAMPUNI HII JINSI INAVYOKIUKA HAKI ZA BINADAMU. MIAKA KADHAA ILIYOPITA KAMA SIJASAHAU HADI KAMATI YA BUNGE ILISHAWAHI KUFIKA HUKO. YAELEKEA HAWA WAARABU WANATISHA SANA. NADHANI NI MUDA MUAFAKA KWA MHE. RAIS KUTIA TIMU HUKO MAANA HAWA AKINA KIGWANGWALA KWA JINSI HAWA JAMAA WANAVYOTISHA ANAWEZA KUVUNJIKA MSAMBA BURE.
 
Taratiiiibuuu bosi..
Mbona hasira sana??
Jielekeze kwenye hoja,hakuna hasira namjulisha tu kanjanja wako aache kukurupuka anamchanganya bosi wake.
Alikurupuka kutaja shule ghali,akasahau kuwa bosi wake anamiliki shule ghali alipostuliwa akatelekeza threa
 
Kuna watu wenye kashfa nzito zaidi ya lowassa na sumaye nchi hii na bado mmewakumbatia chadema!
 
Aisee kumbe mzee kinana anamiliki meli?
Nilikua nauliza tu. hakuna na hakutakuja kua na Mzalendo wa kweli nchi hii zaidi ya Mwl Julius Kambarage Nyerere.
Hao wazalendo wa Sasa ni wazalendo wa mdomoni tu.!
Wezi wakubwa.
 
Katibu Mkuu wa CCM akiwa na viongozi wa kampuni ya uwindaji ya OBC. Kampuni hiyo ina tuhuma lukuki ikiwemo kuchoma nyumba za wafugaji wa jamii ya kimasai Loliondo na kuua mifugo yao. OBC wametajwa pia ktk kashfa ya ujangili kwa mwavuli wa uwindaji.

Ripoti ya AlJaazera iliyoonesha namna serikali inavyofadhili shughuli za ujangili nchini ilimtaja Kinana kama mmoja wa wanasiasa wanaofadhili ujangili, kutokana na meli yake kukamatwa na meno ya tembo huko China. Lakini alikanusha tuhuma hizo na kusema japo meli ni yake, meno hayo hayakuwa yake.

OBC ilianza uwindaji mwaka 1992 baada ya kupewa leseni na Waziri wa Maliasili na Utalii wa wakati huo, Abubakar Mgumia, imekuwa ikiendesha shughuli zake kwny pori tengefu la Loliondo, wilayani Ngorongoro. OBC imejenga uwanja mkubwa wa ndege ambapo wanyama huchukuliwa Ngorongoro hadi Uarabuni moja kwa moja. Pia eneo hilo mitandao ya simu inasoma Uarabuni.

Mwezi November 2017 Waziri wa maliasili na utalii Dr.Hamis Kigwangala alisema ikifika mwezi Januari mwaka huu (2018), kampuni hiyo itaondoshwa nchini kutokana na kuwa na migogoro isiyoisha na wananchi. Kigwangala alisema OBC haitakuwa sehemu ya kampuni za uwindaji zitakazopewa upya leseni ya uwindaji, kutokana na madai ya uvunjifu wa haki za binadamu, ikiwamo kujihusisha na migogoro wa Loliondo kwa zaidi ya miaka 25.
_
“Wananchi wa jamii ya kimasai wamekuwa wakichomewa nyumba zao, mifugo yao ikiuawa. Tumegundua OBC ipo nyuma ya vurugu hizi, siku zao zinahesabika, hawatapewa leseni mpya ya uwindaji Januari mwakani. Nasikia wanajitapa watanihonga dola laki 1 ili wapate kibali. Wanasema aliyepita walimhonga dola laki 2 (Kama Mil.420) kwahiyo mimi laki 1 zinanitosha. Waambieni mimi ni maskini mzalendo. Sihongeki. Wajiandae kuondoka" alisema Kigwangala.

Hata hivyo muda alioutoa umepita na kampuni hiyo haijaondoka. Kigwangala hajaweza kueleza kwanini kampuni hiyo bado ipo wakati alisema mwisho wake ni January. Je amepokea dola laki 1 alizosema wanataka kumhonga? Kitendo cha Kigwangala kukaa kimya na Kinana kuonekana na viongozi wa kampuni hiyo kinaibua maswali mengi, juu ya dhamira ya viongozi wetu kupigania rasilimali zetu na vita dhidi ya ujangili.

Zoezi la kutoa vibali vipya liliahirishwa. Naamini hili unalijua vyema. Ebu tusubiri pale vibali vipya vitakapotolewa ndio tuhoji.
 
Kenya wako vizuri sana kwenye investigative journalist ila hapa TZ hatuna kabisa, japokuwa naona Mwanahabari huru mara nyingi anajitahidi.
Je Azonda amepatikana?
"Rasilimali zetu zipo salama chini ya Raisi Magufuli". Discuss
 
Kuna Mambo Yanatia Kinyaa Ila Acha Yafanyike Maana Wanaofanya Wana Kinga
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom