Katibu Mkuu wa CCM aonekana kwenye Kampuni yenye kashfa nzito Tanzania ya OBC (funika kombe Mwanaharamu apite)

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,260
2,000
Katibu Mkuu wa CCM akiwa na viongozi wa kampuni ya uwindaji ya OBC. Kampuni hiyo ina tuhuma lukuki ikiwemo kuchoma nyumba za wafugaji wa jamii ya kimasai Loliondo na kuua mifugo yao. OBC wametajwa pia ktk kashfa ya ujangili kwa mwavuli wa uwindaji.

Ripoti ya AlJaazera iliyoonesha namna serikali inavyofadhili shughuli za ujangili nchini ilimtaja Kinana kama mmoja wa wanasiasa wanaofadhili ujangili, kutokana na meli yake kukamatwa na meno ya tembo huko China. Lakini alikanusha tuhuma hizo na kusema japo meli ni yake, meno hayo hayakuwa yake.

OBC ilianza uwindaji mwaka 1992 baada ya kupewa leseni na Waziri wa Maliasili na Utalii wa wakati huo, Abubakar Mgumia, imekuwa ikiendesha shughuli zake kwny pori tengefu la Loliondo, wilayani Ngorongoro. OBC imejenga uwanja mkubwa wa ndege ambapo wanyama huchukuliwa Ngorongoro hadi Uarabuni moja kwa moja. Pia eneo hilo mitandao ya simu inasoma Uarabuni.

Mwezi November 2017 Waziri wa maliasili na utalii Dr.Hamis Kigwangala alisema ikifika mwezi Januari mwaka huu (2018), kampuni hiyo itaondoshwa nchini kutokana na kuwa na migogoro isiyoisha na wananchi. Kigwangala alisema OBC haitakuwa sehemu ya kampuni za uwindaji zitakazopewa upya leseni ya uwindaji, kutokana na madai ya uvunjifu wa haki za binadamu, ikiwamo kujihusisha na migogoro wa Loliondo kwa zaidi ya miaka 25.
_
“Wananchi wa jamii ya kimasai wamekuwa wakichomewa nyumba zao, mifugo yao ikiuawa. Tumegundua OBC ipo nyuma ya vurugu hizi, siku zao zinahesabika, hawatapewa leseni mpya ya uwindaji Januari mwakani. Nasikia wanajitapa watanihonga dola laki 1 ili wapate kibali. Wanasema aliyepita walimhonga dola laki 2 (Kama Mil.420) kwahiyo mimi laki 1 zinanitosha. Waambieni mimi ni maskini mzalendo. Sihongeki. Wajiandae kuondoka" alisema Kigwangala.

Hata hivyo muda alioutoa umepita na kampuni hiyo haijaondoka. Kigwangala hajaweza kueleza kwanini kampuni hiyo bado ipo wakati alisema mwisho wake ni January. Je amepokea dola laki 1 alizosema wanataka kumhonga? Kitendo cha Kigwangala kukaa kimya na Kinana kuonekana na viongozi wa kampuni hiyo kinaibua maswali mengi, juu ya dhamira ya viongozi wetu kupigania rasilimali zetu na vita dhidi ya ujangili.

 

Ss Jr

JF-Expert Member
Jan 15, 2018
464
500
Vimbwanga hivi lazima viendelee maana kiongozi wa malaika ameshindwa kutumbua majipu kwa hiyo majipu yanaendelea kuongezeka kama kawaida yao
 

Tindikali

JF-Expert Member
Mar 26, 2010
1,655
2,000
Ndio hizi airstrip za mikoani ambazo Magufuli alikuwa anazichimbia mikwara. Kumbe bado zipo business as usual?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom