Katibu Mkuu wa CCM, Aondoke?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,460
39,928
Unapokuja mkutano Mkuu wa CCM siku chache zijazo bila ya shaka kati ya mambo ambayo CCM inaweza kufanya ni kuangalia kama Katibu Mkuu wao Lt Mstf Yusuph Makamba amewafaa sana au la. Je utendaji wake ukilinganisha ule wa waliomtangulia kina Kawawa, Kolimba, Mangula n.k umeifaa CCM hasa katika mazingira ya kisiasa ya wakati huu? Je, ataendelea kuwafaa kuelekea katika uchaguzi mkuu wa 2010? Je unaridhishwa na jinsi ambavyo ameiongoza CCM katika kujibu hoja na tuhuma mbalimbali ndani ya CCM na ndani ya serikali ya chama chake?

Inawezekana kuwa mzee Makamba kazi hii ya Ukatibu Mkuu imeanza kuwa ngumu na anashindwa kutafutia majibu ya kuelewa hasa kutokana na kauli zake ambazo huko nyuma zimewahi kutishia mufaka wao na CUF na hasa kauli za kutoyapa uzito unaostahili maswala ya kitaifa na hoja zinazohusu Taifa?

Je, wakati umefika CCM ijitafutie KM mpya ili iandane na wakati na kujiandaa kujibu mapigo. Je, Mangula arudishwe? Itakuwaje kama Mwanri atapandishwa cheo na kuwa Katibu Mkuu? Mnaonaje kama Kinana akarudishwa na kupewa Ukatibu Mkuu?

aende asiende, na kwanini?
 
karibu kikwete kutoka china,Je umeshajua kwanini sie ni masikini?
naamini umepata japo kukumbushwa mambo aliyoyafanya Mungu wa wachina Mao,
karibu vasco da gama,mpenda safari na pamba,mpenda kuwalinda mafisadi,
Baada ya kusema hayo,naomba nitoe yaliyopo moyoni mwa mzee mie wa kitanzania,
naomba uniwie radhi manaake sitapenda kukuelekezae mambo ya uchumi sababu haujui,
Mh. Amri jeshi mkuu,Makamba yupo hapa kutuharibia chama tulichoachiwa na Mwalimu..iko wapi sisiemu Mathubuti?
Kwanini ulimpa Ubunge?kwanini unaendelea kumlea wakati amesababisha mazungumzo ya Muungano yapungue kasi,huku akijenga makundi ndani ya Chama?
Mhe. Jk tafadhali mtoe huyu mfitina ambaye anatamani kuwa fisadi.
 
Mwanakijiji anaongelea mawazo yake. Mimi kama Mwana CCM, nasema tumpe muda. Ila kwa kweli tunatakiwa kuwa na katibu mwenye vision. Makamba angefaa sana awe Katibu mwenezi!
 
yeah.. sasa unafikiri vipi kuhusu Yusuph Makamba. Ni kiongozi ambaye CCM bado inamhitaji katika nafasi zake za juu? au wakati umefika wa kumtema.
 
hata siyame ni mtu wa kuondolewa,suala la wahdazabe ni nuksi katika nchi yetu na naamini haya mambo ya kuwapuuzia watu masikini Mungu ndio anawalipa hivyo,ajali hizi za kushtukiza na mambo kuwaendea kombo..
Mie kwa Makamba,Yusuph sina kipingamizi ang'oke,wewe mtu ambaye hakubaliki kijijini kwao Bumbuli huko Lushoto atawezaje kuongoza Chama kikubwa chenye wafuasi kama FD na kada Mpinzani?
ana sifa,ana sifa za kuongoza madereva wa Daladala na Mabasi,arudishe huko tu..
 
Lt Makamba bado anafaa sana kuendelea kushika nafasi ya Ukatibu Mkuu. Utendaji wake upo katika kiwango cha juu kupita wakati wote wa uongozi wake kwa sasa. Tatizo ni mitazamo hasi ya wengi, ambao hupenda kusikia yale yaliyo kwenye nafsi zao tu. Mpaka sasa ameweza kuwazindua watendaji wengi goi goi ndani ya CCM kuanzia ngazi za matawi, ambao walikuwa wameanza kujisahau katika utendaji wao wa kila siku. Kitaifa ameendelea vema kusimamia matakwa ya CCM katika awamu ya kuziba mpasuko huko Visiwani.

Hapana shaka ataendeleza vema mazungumzo ya kufikia muafaka ambao utakuwa na manufaa kwa pande zote mbili.

Hoja za Upinzani kuhusu Ufisadi na mafisadi ameweza kuzijibu kwa ufasaha kabisa na kisiasa zaidi, na hakuna mjadala kwa hilo.
 
FD, as a matter of fact sikufikiria hilo ila it makes more sense than kumuacha tu. Mzee Makamba ana kipaji cha kuzungumza na ushawishi na hasa kuweza kujibu hoja kwa kutozijibu hoja. Niliangalia Mwanri anavyozungumza kuhusu masuala mbalimbali, kwa kweli si mshawishi bali ni mtu ambaye anafaa kutoa maagizo na kufuatilia utendaji. Mzee Makamba kwa upande mwingine ni mtu ambaye anaweza kukiuza CCM kwa ucheshi wake, na kwa kutumia 'wit' na kwa vile anaijua vizuri CCM nadhani si mtu wa kumpoteza kabisa.. Hivyo ila hilo la Katibu Muenezi nadhani itakuwa demotion kwake. Ila kwa kada kama yeye nadhani atapiga saluti na kuwa tayari kukitumikia chama.

Je Mzee Malecela asipoutaka/pewa Umakamu tena, anaweza kuwa Katibu Mkuu?
 
Mwanakijiji anaongelea mawazo yake. Mimi kama Mwana CCM, nasema tumpe muda. Ila kwa kweli tunatakiwa kuwa na katibu mwenye vision. Makamba angefaa sana awe Katibu mwenezi!

Naunga mkono hili wazo. Nafasi ya sasa ya Makamba unahitaji mtu mtendaji, sio mwingi wa maneno.
 
Tatizo kubwa nililoliona ni suala la muafaka wa Zanzibar kuna wakati alivurunda na kama siyo usharp wa Kikwete maji yalikuwa yamemwagika. Nafikiri lile lilikuwa ni miongoni mwa makosa ya kuangaliwa sana.
 
Hivi akiendelea kuwa Katibu nyinyi kinawauma nini? Na kama chama chetu kinaona kina imani naye, nyinyi kinawakera nini? Go Makamba go.. endelea kuitumia nchi na chama chako.

asante.
 
Wakuu labda kuna something sijaelewa hapa, uwezo wa kiongozi wa chama cha siasa si unapimwa unapokuja uchaguzi wa siasa, au?

Uchaguzi wa Madiwani si umefanyika majuzi na CCM under yeye Makamba imeshinda viti vingi, tena sana, sasa huyu anakuwa hafai kwa vigezo vipi wakati tayari ameshinda uchaguzi huu madiwani, tena he was so sffective mpaka kuna kata kama tano, ambazo ameweza kuwapitisha wagombea wa CCM, bure kwa kukosa wapinzani, ambao ninaamini walijua kuwa kugombea hapo ni kupoteza muda tu!

Sasa eti hafai? Waliowahi kufaa ni kina nani?
 
Uzuri wa kitu huonekana kikishatoweka.

Mkuu Worm,

Heshima mbele, ninakubaliana sana na wewe, lakini pia kuwe na sababu ya msingi ya Makamba kutoka, so far sijaiona?

A winner kama Makamba, anatakiwa kuongezwa cheo, sio kutolewa!
 
A winner kama Makamba, anatakiwa kuongezwa cheo, sio kutolewa!

ES bwana, hapa umeniua mbav kabisa. Mkuu hapa nakupinga kiduuuchu; Makamba is not a winner yet!

I have reasons, ila wewe subiri by 2009 utagundua he's a good looser. Angalia response yake kwenye tuhuma za BoT, kachechetuka kumbe wenzio huko huko BoT wanasema tuhuma hizo zina uzito (wahusika haswaa) yeye anasema 'Ni uzushi m2pu'. Ikigundulika tuhuma zina ukweli kiwango flani (hata kidogo) Makamba nitamfuata popote kuckia anasemaje
 
ES bwana, hapa umeniua mbav kabisa. Mkuu hapa nakupinga kiduuuchu; Makamba is not a winner yet!

I have reasons, ila wewe subiri by 2009 utagundua he's a good looser.

nani aliyekwambia mbali kote huko atafika ??
 
Mzee ES, yaani jinsi alivyoehandle suala la Muafaka nusura kuufanya ucollapse hadi Rais akaingilia kati unaita kule ni kushinda? Jinsi alivyoshindwa kuiongoza CCM kwenye suala la Zitto hadi juzi wanatupiwa michanga na watoto unaita huko ni kushinda, Jinsi ambavyo ameiongoza CCM katika sakata la rushwa ndani ya chama hicho hadi Rais aingilie kati unaita huko ni kushinda. Kaka unataka kusema jinsi serikali ya CCM ilivyoshindwa kutetea maslahi ya nchi kwenye mikataba kiasi cha kukubali kufanya siri mambo muhimu hadi yanaibuliwa na wapinzani, ndiyo kushinda huku? Unataka kusema kuwa jinsi ambayo wameshindwa kupelekana wenyewe mahakamani kwa tuhuma za ubadhirifu na na wanaamua kuminyiana kishikaji ndugu yangu unakuita kushinda? Yaani unataka kusema serikali ya CCM iliyoshindwa kusimamia Benki Kuu hadi watu wanachota mabilioni ya fedha mchana kweupe na leo hii wanazawadiwa vyeo na kupepewa na bendera kweli ndiyo kushinda huko kaka? Yaani unataka kusema mfano ya kushinda viti vya udiwani ambapo leo madiwani wanalipwa chini ya House Girls na ma Bar Maids, kweli ndiyo ushindi wa kushangilia huo?

Sasa hivi CCM wamebanwa na suala la kadhi wanashinda pa kuhemea na jana wamepigwa mkwara kwenye channel 10 na shehe mmoja kuwa wawape kadhi ama sivyo 2010 kweli ndiyo ushindi huo? Suala la Zanzibar lina miaka nenda sasa wanashindwa kulimaliza mara moja wanabakia kupigana vijembe tu, kweli ndio uongozi huo?

kama huko ni kushinda basi kufeli kumepoteza maana.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom