Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu akamatwa na Polisi usiku wa manane

SGR, Stielgers gorge, Ndege, Fulahi ova, mabarabara vyote hivyo hamuwezi kuvinadi kwa watanzania hadi mtumie polisi kupata ushindi? CCM nani kawaloga
SGR ni Mradi wa East African Community wenye nia ya kuwa na Gauge moja katika nchi zote 6 wanachama pamoja na ile iliyoanzia Mombasa ambayo sasa imefika mbali kwetu iko Kibaha. Ikikamilika treni itatoka Dar mpaka Mombasa kupitia Bujumbura au Kigali au Juba, Kampala, Nairobi na Voi.

Mradi mzuri sana lakini bahati mbaya sana unatekelezwa wakati wa Awamu ya Tano ya maneno mengi vitendo hafifu. Tanzania inatakiwa kujenga toka Dar hadi Uvinza inapokea Burundi, hadi Isaka inapokea Rwanda, hadi Mwanza mwisho wa ujenzi kwa Tanzania. Kipande cha Uvinza/Bujumbura na Isaka/Kigali hata mawe ya msingi yamesha wekwa wanangoja reli toka Dar ifike waanze kujenga.

Flyover zote na Salender Bridge ni Miradi ya Kikwete ujenzi wake ukaangukia Awamu ya Tano ya maneno kama miradi mikubwa ya Awamu hii itakavyokamiliswa Awamu ijayo. Stiegler's Gorge ni Mradi wa toka Nyerere lakini iliachwa kwa kuheshimu mikataba ya kimataifa, madege na kiwanja cha ndege cha Chato ndo miradi mkubwa ya Awamu hii.
 
Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ndugu Ado Shaibu Ado amekamatwa na Jeshi la Polisi wilayani Tunduru jana Agosti 27 2020 saa sita usiku.

Askari Polisi Wilayani Tunduru wakiongozwa na Mkuu wa Kituo (OCD) wakiwa na silaha za moto walimfuata Katibu Mkuu Ndugu Ado Shaibu nyumbani kwake Mtaa wa Kalanje, Tunduru na kumuamuru wafuatane naye hadi kituo Cha Polisi Tunduru kwa kile walichodai kuwa ni suala la kulitolea ufafanuzi

Baada ya kufika kituoni OCD alimweleza Katibu Mkuu ambaye pia ni Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini kuwa gari lake linasemekana limeteka watu kijijini Malombe.

Hata hivyo, baada ya OCD kuelezwa kuwa gari hilo lilibeba viongozi na wanachama wetu alilazimika kumuachia Ndugu Ado na kumtaka kurejea leo asubuhi, Agosti 28, 2020 kwa mahojiano zaidi.
Gari la Ndugu Ado ambalo lilikaguliwa na kukutwa na bendera za chama pekee, linaendelea kushikiliwa Polisi.

ACT-Wazalendo tunapenda kuutaarifu umma wa Watanzania kuwa huu ni mwendelezo wa matukio ya kumuandama Ndugu Ado katika Jimbo la Tunduru Kaskazini kwa kuratibiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinachoogopa ushindani wa wazi nawa kidemokrasia.

Wakati hayo yakiendelea, mapema jana tarehe 27 Agosti (saa 4 asubuhi) Ndugu Ado aliitwa na Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Tunduru kuwa kuna pingamizi dhidi yake.

Ndugu Ado alipohoji kuwa mbona hadi saa 10.00 muda wa mapingamizi ulipofika mwisho CCM walikuwa hawajaweka pingamizi lolote na kwa nini apokee pingamizi nje ya muda, Msimamizi wa Uchaguzi aling'ang'ania kuwa pingamizi hilo lilikatwa kwa wakati.

Chama cha ACT- Wazalendo tumebaini pasipo shaka kwamba, mpango uliopo chini ya uratibu wa CCM wilayani Tunduru ni kuwaengua wagombea wetu wawili, Ndugu Ado Shaibu Ado (Tunduru Kaskazini) na Mtutura Abdallah Mtutura (Tunduru Kusini) pamoja na wapinzani wengine ili CCM ipite bila kupingwa.

Kwa msingi huo tunalitaka Jeshi la Polisi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inayoongozwa na Jaji Semistocles Kaijage watoe maelekezo na kumuonya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Tunduru na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutenda haki na kuwaacha Wanatunduru Kaskazini na Kusini na kwingineko wachague wawakilishi wanaowapenda.

Janeth Rithe
N/Katibu wa Uenezi, Habari na Mahusiano kwa Umma

ACT Wazalendo Taifa

28 Agosti 2020

Tunaelezwa kwamba ccm ni chama makini duniani kama si afrika, + magufuli amefanya mengi makubwa ambayo hayaja wahi kufanywa na viongozi walio mtangulia tokea uhuru. Ameimarisha miundo mbinu ya barabara, madaraja na reli. Huduma za afya, maji, umeme vijijini, ndege na mengineyo mengi yaliyoipeleka TZ uchumi wa kati.
Kwa mtaji huu kikawaida ccm haikuwa na haja hata yakufanya kampeni. Lakini tunaona nguvu kubwa inayo tumika na ccm kutafuta kura, je ccm haina uhakika na yale wanayojivunia? Ama tatizo hasa ni nini?
 
SGR ni Mradi wa East African Community wenye nia ya kuwa na Gauge moja katika nchi zote 6 wanachama pamoja na ile iliyoanzia Mombasa ambayo sasa imefika mbali kwetu iko Kibaha. Ikikamilika treni itatoka Dar mpaka Mombasa kupitia Bujumbura au Kigali au Juba, Kampala, Nairobi na Voi.

Mradi mzuri sana lakini bahati mbaya sana unatekelezwa wakati wa Awamu ya Tano ya maneno mengi vitendo hafifu. Tanzania inatakiwa kujenga toka Dar hadi Uvinza inapokea Burundi, hadi Isaka inapokea Rwanda, hadi Mwanza mwisho wa ujenzi kwa Tanzania. Kipande cha Uvinza/Bujumbura na Isaka/Kigali hata mawe ya msingi yamesha wekwa wanangoja reli toka Dar ifike waanze kujenga.

Flyover zote na Salender Bridge ni Miradi ya Kikwete ujenzi wake ukaangukia Awamu ya Tano ya maneno kama miradi mikubwa ya Awamu hii itakavyokamiliswa Awamu ijayo. Stiegler's Gorge ni Mradi wa toka Nyerere lakini iliachwa kwa kuheshimu mikataba ya kimataifa, madege na kiwanja cha ndege cha Chato ndo miradi mkubwa ya Awamu hii.

Umepuyanga ndg,

Panapohitajika kusifia sifia tu usione aibu!!
 
Back
Top Bottom