Katibu mkuu UVCCM: Yanayofanyika nchini ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM

MASIGA

Senior Member
Aug 29, 2015
130
281
Kutoka Mbeya 14/09/2018

Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha mapinduzi Mwl Raymond Mwangwala amezungumza na Makundi mbali mbali ya Vijana Wa Boda boda,Machinga,Mamalishe,pamoja na Wachimbaji wadogo wa Mawe kata ya Nsalaga katika mkutano uliofanyika tawi la Kibonde Nyasi.

Akizungumza na Makundi mbali mbali ya Vijana hao Katibu mkuu amemuombea kura mgombea udiwani kupitia CCM Ndg Daudi Ngogo kumchagua ili kumuunga mkono Rais John Magufuli
kufanikisha maendeleo nchini.

“Maendeleo yote yanayofanyika nchini ni utekelezaji wa ilani ya CCM hivyo msipotoshwe na wapinzani hapa
Nsalaga wanaojinadi kuwa watatekeleza maendeleo hizi
barabara za lami na miradi ya maji ni kazi ya Rais
Magufuli,” amesema.

Katibu Mkuu uvccm atazungumza na Wanachama wa ccm pamoja na Wananchi wa kata ya Maanga kumnadi mgombea Udiwani Ndg Newtown Mwatujobe katika mkutano wa hadhara utakao fanyika Mtaa wa Maanga "A"

#TukutaneKazini
IMG-20180914-WA0145.jpg
IMG-20180914-WA0141.jpg
 

Attachments

  • IMG-20180914-WA0143.jpg
    IMG-20180914-WA0143.jpg
    55.1 KB · Views: 14
Back
Top Bottom