Katibu mkuu uvccm taifa azindua dar es salaam jogging club kwa kishindo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,862
930


KATIBU MKUU UVCCM TAIFA AZINDUA DAR ES SALAAM JOGGING CLUB KWA KISHINDO

Katibu Mkuu wa Uvccm Taifa Ndugu Kenani Kihongosi (MNEC) leo amezindua Vijana Jogging Club Jijini Dar Es Salaam Iliyoandaliwa na UVCCM Mkoa Wa Dar Es Salaam ikiwa ni utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa wakati akizindua Vijana Jogging Club Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu amezungumza na vijana na kuwasisitiza umuhimu wa Mazoezi pia kudumisha umoja Amani na Mshikamano katika Taifa pia amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita Inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan itaendelea kuwashirikisha vijana fursa mbalimbali za Michezo kwani Michezo ni Ajira.

Pia amewaeleza vijana kuwa Mheshimiwa Rais anafanya kazi kubwa ya kuimarisha uchumi ambao wanufaika wakubwa ni vijana hivyo vijana wana wajibu wa kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwakufanya kazi pia kuhakikisha maendeleo yanakuja kwa wakati

Katika uzinduzi huo katibu Mkuu aliambatana na Mkuu wa wilaya ya Temeke ambaye tukio hilo lilifanyikia Mheshimiwa Jokate Mwegelo, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es salaam Ndugu Mussa Kilakala pamoja na viongozi wengine wa Jumuiya ya vijana.

Mwisho: Amewaomba vijana kuhakikisha wanalinda Amani na utulivu pia kudumisha umoja na mshikamano.

#Kazi iendelee
#Mtumishi wa Wote


IMG-20210829-WA0212.jpg


IMG-20210829-WA0211.jpg


IMG-20210829-WA0210.jpg


IMG-20210829-WA0221.jpg


IMG-20210829-WA0216.jpg


IMG-20210829-WA0228.jpg


IMG-20210829-WA0227.jpg


IMG-20210829-WA0208.jpg
 
Back
Top Bottom