Katibu Mkuu UVCCM Ndg. Kenani Kihongosi afanya ziara wilaya ya Kyerwa. Wananchi waishukuru Serikali kuwapelekea fedha nyingi za miradi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,863
930
KATIBU MKUU UVCCM Ndg. KENANI LABAN KIHONGOSI AFANYA ZIARA WILAYA YA KYERWA,WANANCHI WAISHUKURU SERIKALI KUWAPELEKEA FEDHA NYINGI ZA MIRADI.

14.12.2021

Katibu mkuu wa Uvccm Ndugu Kenani Kihongosi amefanya ziara wilaya ya Kyerwa kukagua utekelezaji wa Ilani Ya Uchaguzi ya Chama cha mapinduzi na Kuzungumza na Wanachama katika Mashina Matatu.

Katibu mkuu ametembela miradi mbalimbali ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM TAIFA Mheshimiwa SAMIA SULUHU HASSAN Ametoa fedha ili kupeleka maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi wa Wilaya ya Kyerwa.

Miradi ambayo ameitembelea ni Pamoja na:-

1. Ujenzi wa Maabara na Madarasa 2 katika Shule ya Sekondari Murongo unaogharimu Tsh. Milioni 70

2. Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Rutunguru ambao unagharimu Tsh Milioni 250.

3. Ujenzi wa Shule Mpya ya Bweni ya Sekondari Inayogharimu Tsh. Bilioni Moja.

4. Uboreshaji wa Miundombinu ya maji ambayo wamepokea Tsh. Milioni 500.

5. Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan mepeleka pesa Tsh Bilioni 1 na Milioni 700 ili kujenga Madarasa 85 katika wilaya ya Kyerwa.

Pia katibu Mkuu alitembelea na kukagua ujenzi wa Ofisi ya chama cha mapinduzi wilaya ya Kyerwa pamoja na kuzungumza na Wajumbe wa Shina namba 4 Kishanda, Shina namba 3 Rutunguru na Shina namba 4 Rwenkorongo.

Pia Katibu Mkuu wa Uvccm alitembelea wafanyabiashara wa Soko la ndizi lililopo mpakani kati ya Tanzania na Uganda,amewasisitiza wananchi kuzidi kumuunga mkono Serikali pia kulipa kodi kwa maendeleo ya Taifa.

Wafanyabiashara na wananchi wakawaida wamempongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuwapelekea fedha nyingi za maendeleo wameahidi kulinda miundombinu na kuendelea kumuunga mkono kwa kufanya kazi kwa bidii kubwa.

Katibu Mkuu wa Uvccm amewasisitiza kuchukua tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Uviko 19, Kushiriki zoezi la Sensa Pamoja na Kulinda amani na Utulivu wa Taifa letu na Kuepuka vitendo vya Rushwa kwani Rushwa ni Adui wa haki.



Mwisho katibu Mkuu wa Uvccm Alizungumza na wazee wa Wilaya ya Kyerwa,ambao wameishukuru serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzania kwa Ujumla.

Kazi Iendelee
Mtumishi wa Wote


IMG-20211114-WA0013.jpg


IMG-20211114-WA0012.jpg


IMG-20211114-WA0011.jpg


IMG-20211114-WA0014.jpg


IMG-20211114-WA0015.jpg
 
Kwanini katibu mkuu ccm na katibu uvccm wa chama hiki chakavu wote wanafanya ziara mkoa wa Kagera?

Wanasafisha harufu ya nyodo za jini jiwe nini?
 
Back
Top Bottom