Katibu Mkuu UN azungumzia mpaka wa Ziwa Nyasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katibu Mkuu UN azungumzia mpaka wa Ziwa Nyasa

Discussion in 'International Forum' started by MziziMkavu, Oct 5, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Rais Jakaya Kikwewe akiwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon (wa pili kushoto) na Meya wa Jiji la New York, Michael Bloomberg (kushoto), wakimsikiliza, Hellen Agerup kutoka taasisi ya H&B Agerup Foundation akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Anayefuatilia kwa makini kulia ni Msemaji wa Katibu Mkuu wa UN, Martin Nesirky.


  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki- Moon, amepongeza msimamo wa Tanzania kutafuta majawabu ya amani katika kujadiliana kuhusu mzozo wa mpaka kati yake na Malawi kwenye Ziwa Nyasa.

  Amesema uamuzi wa Tanzania ndiyo njia sahihi na inayokubaliwa kimataifa kutafuta na kupata suluhisho la migogoro ya namna hiyo.

  Ban Ki Moon ametoa pongezi hizo kwa Tanzania mjini hapa juzi wakati alipomkaribisha na kukutana kwa mazungumzo na Rais Jakaya Kikwete ambaye yuko New York, kwa ziara ya siku mbili.

  “Majuzi nilikutana na Rais Joyce Banda wa Malawi na akanielezea mzozo wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa na mazungumzo ambayo nchi zetu mbili zinafanya ili kupata ufumbuzi wa amani. Hii ndiyo njia sahihi na Umoja wa Mataifa unaunga mkono njia hiyo,” Ban Ki Moon alimemweleza Rais Kikwete.

  Rais Kikwete alimweleza Katibu Mkuu huyo wa UN kuwa Tanzania bado inaamini kuwa njia sahihi na maelewano zaidi ni kutafuta ufumbuzi wa mvutano huo wa mpaka kwa njia ya mazungumzo.

  Rais Kikwete alisema: “Wazo la awali la kutafuta ufumbuzi wa tatizo hili la miaka mingi sana lilitokana na Rais wa Malawi, marehemu Bingu wa Mutharika ambaye aliniandikia barua ya kutaka nchi zetu zianze mazungumzo kuhusu mzozo huo. Nasi tulikubali. Hivyo, ndivyo tulivyoanza kuzungumza.”

  Rais Kikwete alisema kuwa Tanzania inaongozwa na msingi mkuu wa mipaka inayopita kwenye maeneo ya maji ambako mipaka hiyo inakuwa katikati.

  “Mpaka kati ya Malawi na Msumbiji kwenye ziwa hilo hilo, Nyasa, umekuwa katikati ya Ziwa tokea mwaka 1954 wakati nchi hizo zilipokubaliana kusahihisha makosa ya kuuweka mpaka huo nje ya Ziwa. Mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye mto mkubwa zaidi unaoingiza maji katika Ziwa Nyasa uko katikati ya mto wenyewe,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:

  “Kila mahali ambako nchi zinatengenishwa na maji, mpaka unakuwa katikati ya nchi. Sisi tunadhani hata kwenye mpaka wetu wa Malawi kwenye Ziwa Nyasa ni lazima uwe katikati ya Ziwa.”
  CHANZO: NIPASHE

   
 2. Mkali Tozz

  Mkali Tozz JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 9, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa Dhaifu , pigania hilo la mpaka kwa nguvu zako zote, umalize madaraka yako kwa kumbukumbu iliyotukuka.
  Tumia exposure yako ya kimataifa na nguvu ya safari zako za nje kuwasomesha.
  Ingawa nasikia majadiliano yako na Aunt JOY walishayachomolea.
   
 3. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Ok mm napita maana hii Mada ina ushabiki wa ajabu watakapoingia WaMalawi na asilani Malawi hawataiuweza TZ hata Kijeshi
   
 4. Anthony Lawrence

  Anthony Lawrence JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1,544
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 180
  Thank you Mr President
   
 5. TZ biashara

  TZ biashara JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 523
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tatizo hapa watanzania wengine bado wanaingiza ktk usiasa wetu wa kinyumbani na wanasahau kwamba hili ni suala letu pamoja na tunahitaji kumsapoti kiongozi wetu na tuweke kando tofauti zetu.Kwavyovyote Kikwete bado ni raisi na sidhani kama anachukulia suala hili ni upumbavu nadhani anajua jukumu lake na anatumia fursa nzuri ya kiubinaadamu kwanza.Kwakuwa alipitia jeshi basi namuamini atakuwa anazijua sheria vizuri za kuhusu vita.Na vilevile tukumbuke kwamba mipaka hii iligawanywa na haohao wazungu na sitoshangaa kama wao ndio wanaochonganisha na kuchochea huu mgogoro.Kwani wazungu siku zote wanaangalia maslahi yao kwanza.Na UN vilevile wakati mwingine huwa sioni kama wanasaidia isipokuwa ni kupigwa tarehe na mwishowe wasubiri wakubwa wa dunia wanataka nini na sio ukweli upo wapi.Watanzania tuungane ktk hili suala na tuwe na kauli moja na tuache kumnyanyasa raisi wetu hata katika masuala ya nje na tuwaunge mkono wanajeshi wetu na tuwaombee mungu ili wamalize kwa amani kuliko vita.Uchumi wetu hauna nguvu za kuingia ktk vita kwahiyo sio suala la udhaifu wa mtu ila ni changamoto kubwa anakabiliana nayo huyu kiongozi wetu.Ni mtazamo wangu tu
   
Loading...