afsa
JF-Expert Member
- Dec 6, 2012
- 1,986
- 1,585
Hii ni habari muhimu Sana kwa Wafanyakazi wanaoitwa wenye vyeti feki. Popote mlipo waathirika zingatieni hili.
"Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Dk Yahya Msigwa amesema wafanyakazi wa umma 9,932 waliobainika kuwa na vyeti bandia wakiacha kazi kwa hiari watakuwa wamekosa viinua mgongo vya miaka waliyoitumikia Serikali.
Dk. Msigwa amesema kama watumishi hao wataendelea kubaki kazini watashtakiwa kwa kughushi vyeti na kujipatia mshahara kinyume na sheria.Kwa mujibu wa Sheria ya Kazi na Uhusiano Kazini namba 6 ya mwaka 2004, mwajiri anawajibika kumlipa haki zake mfanyakazi pale anapomwachisha kazi.
Hata hivyo, Dk Msigwa amesema Serikali ikiamua kuwafukuza kazi kwa sheria hiyo ni lazima walipwe stahiki zao kwa sababu wameondolewa kwenye ajira kwa lazima.
Akinukuliwa na gazeti la Mwananchi amesema kuwa,“Kwa sheria ya kazi namba sita (ya mwaka 2004) hakuna neno kufukuzwa kazi, ukimwondoa kazini mtumishi ni lazima umlipe kiinua mgongo, ndiyo maana hapa ninaona agizo la Rais Magufuli ni mtego ili waache kazi wenyewe,” alisema."