Katibu Mkuu (Sophia Kaduma) Arubuniwa Na Mh. George Mkuchika Dhidi ya TANECU Ltd

SINA JINA1

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
391
151

Nchiyetu imekubwa na janga kubwa sana ambalo kimsingi limesababishwa namatumizi mabaya ya KATIBA ya nchi. Huwezi kushangazwa na maamuzi yawatendaji wakuu wa serikali tena wa kada ya juu kabisa (KATIBU MKUU)akifanya maamuzi ama anato maagizo kutokana na shinikizo la kisiasabila kujali utaalamu wake na uwezo aliyojengewa kwa kupewawasaidizii wa kutosha na wenye elimu katika fani mbalimbali.
Tarehe06/09/2013 Katibu Mkuu wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika aliandikabarua kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara kwa kushinikizwa na waziriwa nchi Ofisi ya raisi Utawala Bora Mh. George Mkuchika bilakuzingatia anayoandika ni kinyume na taratibu /sheria za mamboanayotaka yafanyike.

KatibuMkuu mama Sophia E. Kaduma ameteuliwa kwenye nafasi hiyo mweziuliopita, hivyo hakupaswa kukurupuka kusaini barua yenye mapungufukiasi kile kwani ana wataalamu lukuki wa kumshauri. Moja ya mamboyaliyonishtua ni yeye kusaini barua na kumpa nakala Mrajisi wa vyamavya Ushirika na kuwapa nakala makatibu wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara naKatibu wa Waziri ofisi ya nchi( sio katibu mkuu bali PersonalSecretary) tafsiri yake nimeshindwa kuielewa . Sheria ya Ushirikaimeimtaja Mrajisi kama mshauri wa waziri kwenye maswala ya Ushirikana ni mteuliwi wa Raisi. Japo kiutendaji pia ni Mkurugezi Mkuu Idaraya Maendeleo ya Ushirika chini ya Katibu Mkuu wizara ya Kilimo,Chakula na Ushirika ,sheria haijampa mamlaka yoyote Katibu Mkuukufanya maamuzi ya juu kuhusu ushirika na kumtaarifu Mrajisi. Hapamama alilewa madaraka.

Mrajisindiye mwenye mamlaka ya juu katika kutatua migogoro ya ushirika nashughuli nyingine za ushirika -kiushauri na kimaamuzi kwea upande waserikali ukiacha waziri ambaye ni wa final. Katibu Mkuu hukupaswakuweka sahihi yake kumwelekeza Katibu Tawala wa Mkoa kwani hata yeye (Katibu Tawala wa Mkoa) atalipeleka kwa Mraji msaidizi wa Mkoaambaye sina shaka
LAZIMAataomba ushauri kwa Mrajisi wa vyama vya Ushirika Tanzania. Hivyo nidhahiri kuwa katibu Mkuu umetumika bila kujijua ,tabia hii ya kusiinivitu bila kuwaita washauri wa chini wenye taaluma ya jambo lililopomezani ni hatari sana, naamini kabisa kama huu ndio utendaji wakatibu mkuu huyu mwakani kwenye bunge la Budget tutasikia mengikuhusu mikataba mibovu iliyosainiwa na wizara hii nyeti kwa taifaletu.

Ngojanielezee kiufupi nini hasa kimenishangaza mpaka nikaona niyalete humujavini. Vyama vya Ushirika vinaongozwa na Sheria ya Ushirika Na. 20ya 2003 ambapo mswada wa marekebisho ya sheria hio umepitishwa kwakufanyiwa marekebisho makubwa na kuundwa Kamisheni ya Vyama vyaUshirika nchini. Sheria inayotumika mpaka sasa mpaka hapo raisiatakaposaini mswada ule ndani ya siku 21 kuanzia bungelilipowasilisha kwake wiki iliyoishia ijumaa ya tarehe 06/09/2013.Sheria inawataja wanachama kupitia mkutano mkuu kuwa ndio wenyemamlaka ya juu katika maamuzi ya chama chao. Kifungu 61
.-(1)’’The control of the affairs of a registered society shall be vested inthe general meeting summoned in accordance with the by-laws of thesociety and the rules.’’


Hapaimenishtua kuona Mh. George Mkuchika akitaka kuwaaminisha Katibu Mkuuna Waziri wa kilimo chakula na Ushirika kuwa Wabunge wanauwezo wakushinikiza jambo linalohusu Chama cha Ushirika kwa matakwa yaobinafsi ya kutaka kugawa chama cha Ushirika bila idhini ya wanachamawenyewe kwenye mkutano mkuu. Mh. George Mkuchika amekuwa na mvutanowa muda mrefu na Mwenyekiti ( Mzee Yusuph Nanila), Makamu Mwenyekitiwa Bodi ya Uongozi na Meneja Mkuu wa Chama Kikuu TANECU( TandahimbaNewala Cooperative Union) . Mh. George Mkuchika kwa mvutano huoameshindwa kufuata taratibu sahihi na kuweka wazi ubadhilifuunaofanywa na viongozi hao na kuona suluhu ni kuigawa Tanecu kuwe nachama kikuu Tandahimba na Chama Kikuu Newala.


Ushirikakwa Mikoa ya kusini unakuwa kwa kasi sana na hata Uwekezajiunaofanywa na vyama hivi vikuu wa Mkoa wa Mtwara ni mkubwa na sio wakubezwa .mfano TANECU ambayo Mh. Mkuchika anataka kuivunja wamejengaghala Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba gahala lenye thamani yatakribani Tsh1bilioni linaloweza kuweka korosho tani 5,000 achiliambali hilo tayari Tanzania Investment Bank (TIB) wameshawakopeshakiasi cta Tsh 1.5 bilion kwa ajili ya ujenzi wa ghala jinginelitakalogharimu Tsh 2.1bilioni (uwewezo tani 10,000) ambapo ujeziwake ushaanza kwa kasi. Ghala hilo jipya linatazamiwa kukamilikandani ya miezi sita ijayo . Kama hiyo haitoshi tayari TANECUwameshaanza kusafisha uwanja kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda chakubangulia Korosho ambapo watapewa mkopo na Tanzania Investment Bank(TIB) usiopungua 12bilioni. Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wakubangua korosho tani 30,000 kwa mwaka.


Hiyoni kwa uchache tu , hivyo ni jambo la kushangaza kuona kuwa KatibuMkuu wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika anashindwa kujua ninimipango ya serikali yake juu ya uongezaji wa thamani katika mazao.Chama hichi kupitia Mradi wa Ujenzi wa kiwanda cha kubangua Koroshokitawakomboa wakulima wa Tandahimba na Newala kwa kuongeza thamani yakorosho ambazo zimekuwa zikimpa mkulima hasara kwa kuuzwa ghafi hukoIndia.


Niukweli usiofichika kwamba makampuni ya wahindi yanayonunua Koroshoghafi hayapendi kuona mradi huu ukifanikiwa kwani ni kikwazo kwaunyonyaji wao wa bei kwa wakulima wa Korosho. Hili naliweka wazikwamba katika mkataba kati ya Tanzania Investment Bank (TIB) ambaponilifanikiwa kuupitia ni kwamba TIB haitaweza tena kukopesha TANECUikigawanywa kwani nguvu za kiuchumi zitakuwa zimepungua na marejeshoyatashindikana kurudishwa kama mkataba ulivyo sasa ,hivyo mradi waghala unaoendelea na mradi wa kiwanda unaotarajia kuanza mwakaniitakuwa imekufa. Wahindi wanaoshirikiana na baadhi ya viongoziwanaonunua korosho ghafi watakuwa wameshinda kwa kuendelea kununuakorosho ghafi kwa bei waitakayo wao huku wakulima wakiendeleakuteseka na kufa umasikini . Hili linafanywa na Mh. George Mkuchikaambaye ameshindwa kuona mateso wanaopata ndugu zake wa Mtwara .


Angalizo;
TanzaniaInvestment Bank (TIB) ni benki ya serikali ,fedha ambazo imeshazitoakwa miradi hiyo niliyoitaja ni za walipakodi wa Tanzania. Itakuwa niswala la kustajabisha kuingiza Banki ya serikali hasara kubwa yamamia milioni kwa sababu za waziri mmoja anayetunishiana misuli nabaadhi ya viongozi wa Ushirika.


Kamaviongozi ni tatizo zipo njia sahihi za kuwatoa na si kugawa chama nakukidhoofisha kiuchumi bila kufuata taratibu. Katibu mkuu kwaumbumbu wake ameshindwa kujua kuwa kwa sheria hii ya Ushirikaniliyoitaja hapo juu angeweza kumshauri waziri wa Kilimo Chakula naUshirika kumwagiza Mrajisi wa vyama vya ushirika kuiondoa Bodi yaTANECU ( Kama sababu za kuitoa zipo) kuliko kugawa chama kamaanavyotaka.
67.-(1)‘’Subject to the provisions of sections 66, where the Registrarafter consultation with the Minister is satisfied that it is in theinterest of the members and the public, he shall remove the Board andappoint a care taker Board which shall have the duty to manage theaffairs of a registered society and to comply with the directionswhich the special general meeting may give and the appointedcaretaker Board shall, serve for the period of not exceeding threeyears.
(2)Where the Registrar removes the Board under subsection (1), themember of the Board so removed may appeal to the Minister and thedecision of the Minister shall be final.’’


Mojaya mambo anayotaka Mh. George Mkuchika ni kuwepo na Ushirika wilayaya Newala ambao utawajibika kwa Baraza la Madiwani –wakisemawakulima wakatwe Tsh 20 kwa kilo basi ifanyike mara moja bila ridhaaya wakulima /wanaushirika. Hili haliwezi kukubalika kwani hata huomswada mpya ndio umezingatia hayo kama kikwazo na kuwasukuma mbalikabisa wanasiasa kuingilia Ushirika . Haiwezekani fedha za wakulimazikatwe ili mfanyie vikao vya madiwani wa Halmashauri na posho zawatendaji wa serikali bila kuangalia mkulima anaemia kwa kiwango ganikuhudumia mazao yake.


Katibumkuu katika barua yake amemwandikia Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwaraakitaka Mkutano Mkuu wa mwaka wa TANECU unaotarajiwa kufanyika tarehe16-17/09/2013 uhamishiwe Mtwara mjini ili hali TANECU ipo Tandahimbana Newala. Mkutano Mkuu wa chama cha ushirika utahamishwa endapo kunamalalamiko ya wanachama kuhusu eneo mkutano unapofanyika .

Kilichotokeakwenye barua ya Katibu Mkuu ni kutojua nguvu ya bodi ya chama chaUshirikaa, Kama Mh. Mkuchika anataka mkutano wake amwambie wazirimwenzake Mh. Christopher Chiza (Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika)amwagize mrajisi atumie sheria kifungu 64 (1) kinachomruhusu mrajisiwa vyama vya Ushirika kuitisha mkutano mkuu maalumu na ataelekezanini kijadiliwe 61(4)’’TheRegistrar or any other person authorized by him may summon a specialgeneral meeting of the society in such a manner and at such a timeand place as he may direct. The Registrar may also direct whatmatters shall be discussed at the meeting. Such meeting shall haveall the powers and subject to the same rules as meeting called inaccordance with the by-laws of the society’’.


Mkutanomkuu wa TANECU wa mwaka wa tarehe 16-17/09/2013 ni wa kisheria naanayeitisha ni Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi kama kuna malalamiko yawanachama kuhusu mahala pa Mkutano watampelekea Mwenyekitiwaliomchagua wao kidemokrasia na si waziri Mh. George Mkuchika amaMbunge wa Tandahimba.


Naombakuwasilisha na nakala ya barua kwenda kwa Katibu Tawala Mkoa waMtwara.
[/FONT]

View attachment Barua TANECU0002 (1).pdf
 
mimi binafsi haya mambo ambayo yanaongzwa na serikal ya CCM sipendi kuyachangia kwa sababu CCM na watendaji wake walishanuka na harufu ya rushwa na uzalendo ulisha watoka
 
mimi binafsi haya mambo ambayo yanaongzwa na serikal ya ccm sipendi kuyachangia kwa sababu ccm na watendaji wake walishanuka na harufu ya rushwa na uzalendo ulisha watoka

Inaumiza sana pale viongozi wanapotumia madaraka yao kujinufaisha na kuwaumiza wananchi wa chini. Tabia ya kulindana ndio inatufikisha hapa tulipo ,nchi imekuwa ni tegemezi mpaka inatia kero. Watu wamejukusanya kwa ridhaa yao wenyewe kujijengea nguvu za kiuchumi ghafla anatokea mtu mmoja anawavurugia kwa maslahi binafsi.
 
Bwana huyu ana lengo la kukiweka hicho kipande kitachokwenda Newala mikononi mwake.Ameshajaribu sana kulazimisha wakulima kukatwa 20/ kwa kika kilo bila ya kuwashirikisha wakulima.Taarifa ambazo zimeenea ni kwamba anahaha kupata pesa zilizokopwa 2010
 
na NDF kwa ajili ya maendeleo ya Wilaya,yeye akazitumia kwenye kampeni kuhonga kuhonga shs 2000/-10000/.Dhamana ya mkopo huo ni jengo la Sekondari Tandahimba na gari 2 za NDF.Deni limeshazaa riba na majaribio yake kuwakata wakulima limeshindwa.
 
shirika unatakiwa uwe wana ushirika. Waziri au mbunge kama naye analima au anashghuli zinazochangia ushirika ana haki ya kujiunga. Lakini inatia kichefuchefu pale wanasiasa wanaoishi Dar au nje ya sehemu husika kujidai wanawahurumia wanaushirika. Ushirika utaendelea kuwa na matatizo kama yalivyo mashirika ya umma kwa kuwa na wajumbe ya bodi na uongozi ambao hauna hisa na ushirika zaidi ya ajira na kula.
 
Bwana huyu ana lengo la kukiweka hicho kipande kitachokwenda Newala mikononi mwake.Ameshajaribu sana kulazimisha wakulima kukatwa 20/ kwa kika kilo bila ya kuwashirikisha wakulima.Taarifa ambazo zimeenea ni kwamba anahaha kupata pesa zilizokopwa 2010
Huyu Kiongozi ni mbinafsi sana ,halafu hana hoja ya msingi . Ni kiongozi anaye amini kuwa yeye yupo sahihi siku zote ,anaona kuvuruga maisha ya wengine kwa manufaa yake binafsi ni sawa kabisa .
 
shirika unatakiwa uwe wana ushirika. Waziri au mbunge kama naye analima au anashghuli zinazochangia ushirika ana haki ya kujiunga. Lakini inatia kichefuchefu pale wanasiasa wanaoishi Dar au nje ya sehemu husika kujidai wanawahurumia wanaushirika. Ushirika utaendelea kuwa na matatizo kama yalivyo mashirika ya umma kwa kuwa na wajumbe ya bodi na uongozi ambao hauna hisa na ushirika zaidi ya ajira na kula.
Halafu cha kushangaza anawasemea wanaushirika ili hali yeye si mshirika . Taarifa zilizopo wilayani kwake newala Hawataki kumsikia hata kidogo .Anatapatapa kwenye korido za wizara ya kilimo bila mafanikio
 
Halafu cha kushangaza anawasemea wanaushirika ili hali yeye si mshirika . Taarifa zilizopo wilayani kwake newala Hawataki kumsikia hata kidogo .Anatapatapa kwenye korido za wizara ya kilimo bila mafanikio
Essence ya ushirika ilikufa kutokana na nguvu waliyokuwa nao viongozi wa ushirika. Mtu hajawahi kulima korosho eti ndio meneja mkuu. Tokea hapo ufanisi wa ushirika ulipngua na wakajaa walaji wasio na uchungu. Sasa ushirika mpya usirubuniwe na viongozi tena. Hata nchi za kibepari kuna ushirika wa wakulima ili waweze kutetea bei kwa mazao yao kwa kulobby wanasiasa si kinyume!! NYANZA BUCOP viliweza kusomesha watoto wa wanachama wake popote. Leo hii kila kiongozi anafikiria kumsomesha mtoto wake tu.
 
Mama Kaduma ni mtendaji mwadilifu amini hivyo, na kwamba yuko katika kiti kwa mrefu, kabla ya kywa Katibu mkuu (KM) alikuwa naibu lakini kwa miaka miwili ilopita yy ndo alikuwa kama KM kwakuw aliyekuwa bosi wake alikuwa na matatizo kidogoya kiafya so anajua majukumu yake vyema
pia mrajisi yuko chini yake na kwamba katika hili ameshirikishwa na ndo aloshauri,kilichomfanya KM aandike yy barua ni utaratibu wa kiutawala na kwamba kiutendaji mrajis asingeweza mpa maagizo katibu tawala wa mkoa.
 
Mama Kaduma ni mtendaji mwadilifu amini hivyo, na kwamba yuko katika kiti kwa mrefu, kabla ya kywa Katibu mkuu (KM) alikuwa naibu lakini kwa miaka miwili ilopita yy ndo alikuwa kama KM kwakuw aliyekuwa bosi wake alikuwa na matatizo kidogoya kiafya so anajua majukumu yake vyema
pia mrajisi yuko chini yake na kwamba katika hili ameshirikishwa na ndo aloshauri,kilichomfanya KM aandike yy barua ni utaratibu wa kiutawala na kwamba kiutendaji mrajis asingeweza mpa maagizo katibu tawala wa mkoa.
Hujasoma vyema kilichoandikwa hapo juu ,huyo mama ni Boss wa mrajis ila hapo tunazungumzia sheria . Sheria hamtaji Katibu Mkuu inamtaja Registrar ambaye anateuliwa na Raisi tofauti na wakurugenzi wengine wa Idara ,hapa ni kwamba unachotaka kutuaminisha kuwa Katibu mkuu wizara ya fedha anaweza kufanya kazi za kamishna wa kodi .
 
Mama Kaduma ni mtendaji mwadilifu amini hivyo, na kwamba yuko katika kiti kwa mrefu, kabla ya kywa Katibu mkuu (KM) alikuwa naibu lakini kwa miaka miwili ilopita yy ndo alikuwa kama KM kwakuw aliyekuwa bosi wake alikuwa na matatizo kidogoya kiafya so anajua majukumu yake vyema
pia mrajisi yuko chini yake na kwamba katika hili ameshirikishwa na ndo aloshauri,kilichomfanya KM aandike yy barua ni utaratibu wa kiutawala na kwamba kiutendaji mrajis asingeweza mpa maagizo katibu tawala wa mkoa.

unajua au unasikia...?
 
viongozi wa ccm ni majanga sn ktk jamii, baadala ya kuw problem solvers wamekuwa problem makers...Mkuchika kwa kweli ni kikwazo cha maendeleo Newala na kusini kiujumla.
 
Tumesikia upande mmoja ebu tsikie na upande wa pili,kama mpo kitokezeni mjiu hoja
 
Wanajamvi Mimi naomba munisaidie maswali yafuatayo.
Mosi, hivi TANECU tangia kugawanywa toka MAMCU ambayo sasa ni Masasi na Mtwara wameweza kufanya nini cha kujivunia katika kumwendeleza mkulima wa korosho?

Pili, TANECU zaidi ya kusimamia ununuzi wa korosho ni jambo lipi lingine ambalo ni la kujivunia katika miaka 20 iliyopita kabla ya kuanza kujengwa kwa Ghala la Tandahimba?

Tatu, TANECU imekuwa ikilalamikiwa na wananchi kwa kutowasaidia na kujitajirisha wenyewe hususan viongozi wa TANECU wakiwaacha wakulima hoi bin taabani. Je nini kifanyike kuwasaidia wakulima wenu?

Mi siungi mkono hoja ya kuovunja TANECU lakini naipenda kuiona inafanya kazi kwa weledi na kubuni njia mbadala za kuwasaidia wakulima na kuondokana na kusimamia ununuzi pekee miaka nenda rudi. TANECU lazima mfikirie mbali zaidi la sivyo Mkuchika atapata nguvu ya kuwagawa.
 
Back
Top Bottom