Katibu mkuu na waziri wana tofauti gani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katibu mkuu na waziri wana tofauti gani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zing, Jul 2, 2009.

 1. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2009
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  sijui organisation structure ya serkali ilivyo lakininina changamoto na dukuduku juu ya hivi vyeo vikubw aviwili kwenye wizara

  Waziri yuko juu kuu ya katibu mkuu ki cheo lakini naamini mtendaji mkuu wa wizara ni katibu mkuu na si waziri.wote karibu mkuu na waziri wanateuliwa na rais.

  Sasa sijui shughuli za kila siku za waziri ni zipi na zina tofauti gani na zile shighuli za mtendaji mkuu wa wizra ambaye ni katibu mkuu? i nahisi inagwa mambo yankwenda lakini kunaweza kuwa na conclict of responsibility na hivyo kuchangia matatizo kwenye decisiaon makin juu ya utendaji wa wizara zetu.

  Kwa maana hiyo mi nilikuw anapendekeza ceo kimoja kufutwe kupunguza ukubwa wa serikali . kwenye wizara tubaki na makatibu wakuu au tuwe na mawaziri.

  Kama basi ni muhimu vyeo hivi vyeto ni lazima viwepo kwa nini makatibu wakuu wasiajiriwe kwa kufanya application na ikulu iwa fanyie usaili na kuwapa mkakati wa majukumu watayotakiwa kutekeleza .

  Uwajibikaji unakosekana sababu nafasi nyingi zinaoenekana ni za kisiasa. nasema ni za kisiasa sababu ni za kuteuliwa . Kwa sababu wizarani sio tu waziri na katibu wanateuliwa lakini hata wakurugenzi nao. Somewhere juu juu ya utawala anatakiw awepo mtu ambaye hata kama kateuliwa basi ujilikane alifanyiwa usaili na kukidhi mahitaji ya wizara au idara husika.

  Naamini kwa style hii JK anaweza kupunguza zigo la serikali kubwa na kuongeza uwajibikaji.
   
 2. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wewe ni nani mpaka utoe mapendekezo? unajua utaratibu wa kubadilisha katiba?
  Anza kuwa mbunge ndio uanze harakati hapa unapoteza muda!
   
 3. M

  Masatu JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Tofauti ni kuwa mmoja ni katibu mkuu mwingine ni waziri! mbali hapo? swali jingine pls......
   
 4. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,646
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  Mkuu hii inanikumbusha lile sakata la Masha na katibu mkuu wake kwenye mradi wa vitambulisho!
   
 5. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Aah, sijui kwanini wasiotaka kukujibu hawakai kimya na kuachia wenye nia ya kukujibu kufanya hivyo. Naamini sio lazima kuandika tu hata kama huna cha kuandika.

  Mkuu, mimi ngoja nijaribu kukujibu maswali yako kama ninavyohisi kuwa ninafahamu. Wenye nia wengine watasaidia zaidi.

  Katibu Mkuu wa Wizara ndie mtendaji mkuu wa Wizara. Yeye ndie mwenye mamlaka na rasilimali zote za Wizara. Pia ni Treasurer wa Wizara. ivyo ndie anaemiliki matumizi yote ya wizara na usimamizi wote wa Wizara. Pia ndie anaeajiri na kusimamia manunuzi yote ya Wizara. Barua na mawasiliano yote ya wizara hufanyika kupitia kwake.

  Katibu Mkuu ni mwajiriwa wa serikali (mtumishi wa serikali) hivyo ana muda wa kustaafu kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma, na anastahili mafao kama mfanyakazi mwingine yeyote. Pamoja na kuwa huteuliwa kushika wadhfa huo na Rais, lakini huteuliwa kutoka katika watumishi wa serikali (kama promotion).

  Waziri kwa upande mwingine ni mwanasiasa. Kama unavyojua, huteuliwa kuwa Waziri kwa mujibu wa Katiba (kutoka katika wabunge wa Bunge la JMT). Shughuli za Waziri pamoja na mambo mengine ni usimamizi wa utekelezaji wa sera za chama tawala. Waziri ni msemaji wa wizara na si mtendaji. Yeye hawajibiki kwa utendaji wa Wizara yake moja kwa moja.

  Waziri si lazima awe msomi. Just imagine, jinsi tunavyopata wabunge wetu (uchaguzi/uteuzi) inawezekana kabisa kuwa wabunge wanaoweza kufanyakazi na Rais wasiwe wasomi kabisa (labda std 7 leavers). Hii haina maana kuwa Baraza la mawaziri halitaundwa. Litaundwa kutokana na hao hao std 7 leavers.

  Utendaji wa viongozi hao wawili uko wazi. Ila kutokana na siasa kushika nguvu nchini, wanasiasa hupenda kujikweza na kufanya hata yale ambayo yako nje ya mipaka ya kazi zao. Mifano iko mingi (mmoja ni wa Vitambulisho).
   
Loading...