Katibu Mkuu Miundombinu

Freetown

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
883
73
Katibu Mkuu Miundombinu ni Mkurugenzi mgodi...

2008-04-14 09:24:39
Na Mwandishi Wetu

Wakati Rais mstaafu Benjamin Mkapa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini wa awamu yake, Bw. Daniel Yona, wanashutumiwa kwa kujimilikisha mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Bw. Omar Chambo, anadaiwa kuwa Mkurugenzi wa kampuni yao ya Tanpower Resources iliyonunua mgodi huo. Hata hivyo, Bw. Chambo amejitetea kwamba ukurugenzi wake katika Tanpower Resources ni kwa ajili ya kulinda maslahi ya taifa.

``Nimo kwa ajili ya serikali. Ni mkurugenzi wa hisa za serikali. Tanpower Resources ina asilimia 70 za hisa na serikali inamiliki zilizobakia 30. Tuko mimi na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,`` alisema bila kutaja jina la mkuu huyo wa mkoa. Mkuu wa sasa wa mkoa huo ni Bw. John Mwakipesile.

Katibu Mkuu wa Miunbombinu anadaiwa kupewa wadhifa huo wakati huo akiwa Kaimu Kamishna wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini kipindi hicho Bw. Yona akiwa Waziri.

Bw. Chambo alisisitiza kuwa yuko pale kwa niaba ya serikali na si kwamba alichaguliwa na akaongeza kuwa aliingia pale kwa cheo chake kama Kamishna wa Madini ili kulinda maslahi ya taifa na si kosa lake.

Alipoulizwa iwapo cheo hicho alikipata kwa staili ya wadhifa wake, Kamishna wa Madini wa sasa anaweza kuchukua jukumu la kuwa Mkurugenzi wa Tanpower Resources? Alijibu , `siyo lazima bila kufafanua zaidi``.

Alipoulizwa juu ya madai kuwa umiliki huo unalalamikiwa na ulifanywa bila stahili kwa vile Rais na Waziri wake walijinyakulia mali nje ya utaratibu aliwatetea wahusika.

Alimtetea Rais Mkapa kuwa hayumo kwenye mradi wa Kiwira na kwa upande wa Bw. Yona alisema naye pia hayupo bali ni mtoto wake.

Alishauri watu kusoma mkataba wa makubaliano ya mradi wa Kiwira ndipo watajua na ni nani katika mradi huo.

Pamoja na malalamiko ya miradi ya Richmond uliyowahusisha viongozi kadhaa, Rais Mkapa amekuwa akilalamikiwa kwa kujinyakulia mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira ambao ni mali ya umma.

Imekuwa ikidaiwa kuwa alichukua machimbo hayo chini ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC).

Madai dhidi ya Rais mstaafu yanasema kuwa yeye na Bw. Yona walijimilikisha mradi huo akiwa Ikulu baada ya kuunda kampuni yao binafsi Tanpower Resources iliyosajiliwa Desemba 2004 na kisha `kujitwalia` mgodi huo rasmi Machi 2005.

Makaa ya Kiwira, mkoani Mbeya baada ya kuchimbwa na kuchakatwa, huzalisha umeme katika mradi mkubwa wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 271.8 karibu sawa na Sh. bilioni 340.

Umeme huo unatarajiwa kuuzwa kwa Shirika la Umeme TANESCO.

Licha ya Rais mstaafu Mkapa kuhusishwa na tuhuma mbalimbali za kufanya biashara akiwa Ikulu, hajawahi kujibu kama `anapakaziwa` wala kuomba radhi taifa kama madai hayo ni ya kweli.

SOURCE: Nipashe

Swali langu kwanini asiachie huo ukurugenzi kama aliupata akiwa kama Kaimu Kamishna wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini ili anayeshikilia wafidha huo aweze kuchukua hiyo nafasi?????????.
 
Freetown, ndio nimeisoma hiyo nikawa nataka kuiweka hewani sababu kuna mapungufu mengi sana....

Tatizo ni kwamba kwenye hivi vyeo watu wanachanganya sana. Kuna wakati niliangalia kwenye ule mfumo wa Civil Service nikakuta kuna vitu hivi kwa harakaharaka:
1. Cheo cha kimuundo - Kuna respect na mafao extra
2. Cheo cha kimfumo - Kuna respect but not necessarily mafao extra, also kuna seniority hapa
3. Cheo cha kimajukumu - hiki ni kama hicho cha Katibu Mkuu Fedha ni board member BOT etc

Naona hapo ndugu yetu Chambo mambo yamepiga amejikanyaga manake hajaelezea kwa nini alikaa kwenye board ya TanPower na kwa nini hajang'atuka alipoenda Miundombinu amuachie Kamishna mpya wajibu wake kule mahali.... Kwa mimi moja kwa moja inannionyesha kuwa hakukaa pale mahali kama Kamishna bali kama Chambo!!!

These are my 2 cents and I stand to be corrected as this is my deirect translation using my small Maasai head baada ya mori kupanda!!!
 
Swali langu kwanini asiachie huo ukurugenzi kama aliupata akiwa kama Kaimu Kamishna wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini ili anayeshikilia wafidha huo aweze kuchukua hiyo nafasi?????????.

Freetown;

Yale yaleee!!! Kama mwandishi angekuwa makini angekuwa amekuulizia swali lako, lakini kwa bahati mbaya haikuwa hivyo!!!!

Swali tu:-
Hivi ni lazima wakurugenzi wanaowakisha serikali kwenye board wawe watumishi wa umma, mimi nadhani hapa ndio source kubwa ya ufisadi.
 
Chambo! Mmh naona mambo haya, yanaleta rongo rongo. lakini haonekani kama fisadi
 
Kasheshe;

Huyu aliwekwa hapo ili kulinda maslahi ya wakubwa, na siyo kwa maslahi ya taifa kama anavyosema. kama unavyosema hii ni kuendeleza ufisadi tu
 
Katibu Mkuu Miundombinu ni Mkurugenzi mgodi...

2008-04-14 09:24:39
Na Mwandishi Wetu

Wakati Rais mstaafu Benjamin Mkapa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini wa awamu yake, Bw. Daniel Yona, wanashutumiwa kwa kujimilikisha mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Bw. Omar Chambo, anadaiwa kuwa Mkurugenzi wa kampuni yao ya Tanpower Resources iliyonunua mgodi huo. Hata hivyo, Bw. Chambo amejitetea kwamba ukurugenzi wake katika Tanpower Resources ni kwa ajili ya kulinda maslahi ya taifa.

``Nimo kwa ajili ya serikali. Ni mkurugenzi wa hisa za serikali. Tanpower Resources ina asilimia 70 za hisa na serikali inamiliki zilizobakia 30. Tuko mimi na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,`` alisema bila kutaja jina la mkuu huyo wa mkoa. Mkuu wa sasa wa mkoa huo ni Bw. John Mwakipesile.

Katibu Mkuu wa Miunbombinu anadaiwa kupewa wadhifa huo wakati huo akiwa Kaimu Kamishna wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini kipindi hicho Bw. Yona akiwa Waziri.

Bw. Chambo alisisitiza kuwa yuko pale kwa niaba ya serikali na si kwamba alichaguliwa na akaongeza kuwa aliingia pale kwa cheo chake kama Kamishna wa Madini ili kulinda maslahi ya taifa na si kosa lake.

Alipoulizwa iwapo cheo hicho alikipata kwa staili ya wadhifa wake, Kamishna wa Madini wa sasa anaweza kuchukua jukumu la kuwa Mkurugenzi wa Tanpower Resources? Alijibu , `siyo lazima bila kufafanua zaidi``.

Alipoulizwa juu ya madai kuwa umiliki huo unalalamikiwa na ulifanywa bila stahili kwa vile Rais na Waziri wake walijinyakulia mali nje ya utaratibu aliwatetea wahusika.

Alimtetea Rais Mkapa kuwa hayumo kwenye mradi wa Kiwira na kwa upande wa Bw. Yona alisema naye pia hayupo bali ni mtoto wake.

Alishauri watu kusoma mkataba wa makubaliano ya mradi wa Kiwira ndipo watajua na ni nani katika mradi huo.

Pamoja na malalamiko ya miradi ya Richmond uliyowahusisha viongozi kadhaa, Rais Mkapa amekuwa akilalamikiwa kwa kujinyakulia mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira ambao ni mali ya umma.

Imekuwa ikidaiwa kuwa alichukua machimbo hayo chini ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC).

Madai dhidi ya Rais mstaafu yanasema kuwa yeye na Bw. Yona walijimilikisha mradi huo akiwa Ikulu baada ya kuunda kampuni yao binafsi Tanpower Resources iliyosajiliwa Desemba 2004 na kisha `kujitwalia` mgodi huo rasmi Machi 2005.

Makaa ya Kiwira, mkoani Mbeya baada ya kuchimbwa na kuchakatwa, huzalisha umeme katika mradi mkubwa wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 271.8 karibu sawa na Sh. bilioni 340.

Umeme huo unatarajiwa kuuzwa kwa Shirika la Umeme TANESCO.

Licha ya Rais mstaafu Mkapa kuhusishwa na tuhuma mbalimbali za kufanya biashara akiwa Ikulu, hajawahi kujibu kama `anapakaziwa` wala kuomba radhi taifa kama madai hayo ni ya kweli.

SOURCE: Nipashe

Swali langu kwanini asiachie huo ukurugenzi kama aliupata akiwa kama Kaimu Kamishna wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini ili anayeshikilia wafidha huo aweze kuchukua hiyo nafasi?????????.

Maslahi gani ya Taifa anayolinda wakati Tangold ni moja ya makampuni ambayo yalichota mabilioni ya pesa toka BoT kinyemela.? Kama likuwa analinda maslahi ya Taifa mbona hakuhoji wizi wa mabilioni uliofanywa na kampuni hiyo ya Tangold? :confused:
 
Chambo! Mmh naona mambo haya, yanaleta rongo rongo. lakini haonekani kama fisadi

Mgoyangi/

Hapa hakuna longolongo ni kwa matamshi yake mwenyewe kama alivyohijiwa na mwandishi wa habari anaonyesha kujikanyaga namnukuu alivyosema
"Alipoulizwa iwapo cheo hicho alikipata kwa staili ya wadhifa wake, Kamishna wa Madini wa sasa anaweza kuchukua jukumu la kuwa Mkurugenzi wa Tanpower Resources? Alijibu , `siyo lazima bila kufafanua zaidi"
 
Back
Top Bottom