Freetown
JF-Expert Member
- Apr 6, 2008
- 882
- 78
Katibu Mkuu Miundombinu ni Mkurugenzi mgodi...
2008-04-14 09:24:39
Na Mwandishi Wetu
Wakati Rais mstaafu Benjamin Mkapa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini wa awamu yake, Bw. Daniel Yona, wanashutumiwa kwa kujimilikisha mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Bw. Omar Chambo, anadaiwa kuwa Mkurugenzi wa kampuni yao ya Tanpower Resources iliyonunua mgodi huo. Hata hivyo, Bw. Chambo amejitetea kwamba ukurugenzi wake katika Tanpower Resources ni kwa ajili ya kulinda maslahi ya taifa.
``Nimo kwa ajili ya serikali. Ni mkurugenzi wa hisa za serikali. Tanpower Resources ina asilimia 70 za hisa na serikali inamiliki zilizobakia 30. Tuko mimi na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,`` alisema bila kutaja jina la mkuu huyo wa mkoa. Mkuu wa sasa wa mkoa huo ni Bw. John Mwakipesile.
Katibu Mkuu wa Miunbombinu anadaiwa kupewa wadhifa huo wakati huo akiwa Kaimu Kamishna wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini kipindi hicho Bw. Yona akiwa Waziri.
Bw. Chambo alisisitiza kuwa yuko pale kwa niaba ya serikali na si kwamba alichaguliwa na akaongeza kuwa aliingia pale kwa cheo chake kama Kamishna wa Madini ili kulinda maslahi ya taifa na si kosa lake.
Alipoulizwa iwapo cheo hicho alikipata kwa staili ya wadhifa wake, Kamishna wa Madini wa sasa anaweza kuchukua jukumu la kuwa Mkurugenzi wa Tanpower Resources? Alijibu , `siyo lazima bila kufafanua zaidi``.
Alipoulizwa juu ya madai kuwa umiliki huo unalalamikiwa na ulifanywa bila stahili kwa vile Rais na Waziri wake walijinyakulia mali nje ya utaratibu aliwatetea wahusika.
Alimtetea Rais Mkapa kuwa hayumo kwenye mradi wa Kiwira na kwa upande wa Bw. Yona alisema naye pia hayupo bali ni mtoto wake.
Alishauri watu kusoma mkataba wa makubaliano ya mradi wa Kiwira ndipo watajua na ni nani katika mradi huo.
Pamoja na malalamiko ya miradi ya Richmond uliyowahusisha viongozi kadhaa, Rais Mkapa amekuwa akilalamikiwa kwa kujinyakulia mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira ambao ni mali ya umma.
Imekuwa ikidaiwa kuwa alichukua machimbo hayo chini ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC).
Madai dhidi ya Rais mstaafu yanasema kuwa yeye na Bw. Yona walijimilikisha mradi huo akiwa Ikulu baada ya kuunda kampuni yao binafsi Tanpower Resources iliyosajiliwa Desemba 2004 na kisha `kujitwalia` mgodi huo rasmi Machi 2005.
Makaa ya Kiwira, mkoani Mbeya baada ya kuchimbwa na kuchakatwa, huzalisha umeme katika mradi mkubwa wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 271.8 karibu sawa na Sh. bilioni 340.
Umeme huo unatarajiwa kuuzwa kwa Shirika la Umeme TANESCO.
Licha ya Rais mstaafu Mkapa kuhusishwa na tuhuma mbalimbali za kufanya biashara akiwa Ikulu, hajawahi kujibu kama `anapakaziwa` wala kuomba radhi taifa kama madai hayo ni ya kweli.
SOURCE: Nipashe
Swali langu kwanini asiachie huo ukurugenzi kama aliupata akiwa kama Kaimu Kamishna wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini ili anayeshikilia wafidha huo aweze kuchukua hiyo nafasi?????????.