Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad akutana na madiwani wa CUF jiji la Dar es salaam September 01, 2018

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF–Chama Cha Wananchi)

TAARIFA KWA UMMA

1. KATIBU MKUU Maalim Seif Sharif Hamad Leo amekutana na kufanya mazungumzo na Madiwani wa CUF katika Jiji la Dar es Salaam kwa lengo la kupeana Taarifa mbalimbali za Chama na Mwelekeo wa siasa nchini. Katika kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi ya Wabunge wa CUF iliyopo Magomeni. Madiwani 13 kati ya 15 walihudhuria kikao hicho huku wawili wakitoa udhuru. CUF ilikuwa na madiwani 21, madiwani 3 wamehama Chama, na madiwani 3 ni wafuasi wa genge la Lipumba.

2. Katika kikao hicho Madiwani walizungumzia mkakati wa kukiimarisha Chama na walimuahakikishia Katibu Mkuu kuwa wataendelea kuwa Imara kukilinda Chama cha CUF na kusimamia madhumuni na malengo ya kuundwa kwake. Na kamwe hawataweza kuwasaliti wananchi waliowachagua na Chama chao kinachosimamia mabadiliko ya kweli nchini.

3. Madiwani hao walimueleza Katibu Mkuu kuwa ni kweli mnada wa ‘biashara haramu ya kununua binaadamu’ bado unaendelea na kwamba wamekuwa wakifuatwa mara kwa mara kwa ajili ya biashara hiyo na wakati mwingine kukumbana na vitisho, kubambikizwa kesi na kuzuliwa mambo wasiyokuwa nayo kutokana na msimamo wao. Hata hivyo pamoja na umasikini na shida walizokuwa nazo kama walivyo watanzania wengi hawatakubali kuuza heshima zao kwa vipande vya dhahabu na fedha.

4. Madiwani wamemthibitishia Katibu Mkuu kuwa wanaojiudhuru na kuhama Chama si kweli kuwa wanahama kwa kufuata wanachodai mazuri yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano bali inatokana na dhambi zao binafsi walizonazo na kudhani kuwa huko wanakwenda watapata kichaka cha kujifichia maovu yao. Tamaa na kutanguliza maslahi binafsi ndio msingi wa kuhama kwako.

5. Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad aliwapongeza madiwani hao kwa msimamo waliouonyesha mbali na vishawishi wanavyokumbana navyo. Aliwaeleza Madiwani hao hali halisi ya mwelekeo wa siasa za ndani ya CUF na nchi kwa ujumla na kwamba hakuna aliyefanikiwa kwa usaliti. CUF ni Taasisi Imara na itaendelea kuwa Imara. Na wale wanaodhani kuwa CUF itakufa wanajidanganya. CUF haiwezi kufa. Kuhimiri mitikisiko ni sifa ya kiongozi Imara. Hali ya uchumi wa nchi yetu ni mbaya sana na kila mmoja wetu ni shahidi wa hili. Tusikubali kuwaangusha Watanzania wanaotutegemea kusimamia na kuleta mabadiliko nchini kupitia CUF na Viongozi wake.

6. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara Mhe. Joran Bashange, Naibu Mkurugenzi wa Uchaguzi Mhe. Shaweji Mketo, K/Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Wanawake CUF Taifa –JUKECUF Mhe. Bi. Riziki Shahari Ngwali na maafisa wa Chama Tanzania Bara. Kesho Katibu Mkuu atakutana na Viongozi wa CUF na Wenyeviti wa Serikali za Mtaa wanaotokana na CUF Mkoa wa Dar es Salaam.


HAKI SAWA KWA WOTE

Imetolewa na kurugenzi ya Habari CUF-Taifa leo Tarehe 1/9/2018;

MBARALA MAHARAGANDE
NAIBU MKURUGENZI-NMHUMU

maharagande@gmail.com
Tigo-0715 062 577, Voda -0767 062 577
 
Back
Top Bottom