Katibu mkuu kiongozi wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar azindua mtandao wa Tshrmnet

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
832
533
KATIBU MKUU KIONGOZI WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR AZINDUA MTANDAO WA TPSHRMNET.

Na Prisca Libaga, Arusha.

Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Zena Said amezindua rasmi mtandao wa mameneja rasilimali watu katika utumishi wa umma barani Afrika ,Tawi la Tanzania (TPSHRMNET) Mkoani Arusha .

Akizungumza kwenye uzinduzi huo ,Bi Zena amesema kuwa uwepo wa mtandao huo barani Afrika utasaidia sana kukutana na kuangalia changamoto ya rasilimali watu katika sekta ya umma barani Afrika.

Amesema kuwa, kukutana kwao mkoani Arusha katika mkutano wao sambamba na kuzindua mtandao huo utasaidia sana kuboresha utendaji kazi wao mahala pa kazi sambamba na kuimarisha juhudi za utoaji haki kwa nchi za Afrika .

“Ili kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa katika kazi zetu ni lazima swala la rasilimali watu lipewe kipaumbele na kuendelea kusimamiwa vizuri sambamba na kutoa elimu kwa wananchi ili kuepuka migongano isiyo ya lazima .”amesema Zena.

Aidha amewataka mameneja rasilimaliwatu kuhakikisha wanasimamia dhana ya serikali mtandao na kutatua changamoto huku wakihakikisha wanarahisisha utoaji wa huduma kwa watanzania ili wafanye vizuri zaidi kwenye maswala ya Tehama.

Hata hivyo amewataka mameneja hao kuhakikisha wanafanya kazi kwa uadilifu mkubwa sambamba na kuwa wazalendo katika utendaji kazi wao wa kila siku huku akiwataka kuacha majungu na uzushi katika maeneo yao ya kazi.

“Nawaombeni sana msiwadharau wale mnaowaongoza kutokana na vyeo vyenu tendeni haki na msikilize changamoto zao na kuzifanyia kazi kwa wakati tuache kuchafuana kila mmoja atimize wajibu wake kwa wakati “amesema .

Hata hivyo amewataka mameneja hao kuondokana na wizi wa fedha kwenye taasisi zao kwani kuna baadhi ya watu wamekuwa wakifanya wizi kwa kuwaibia watumishi wanaowaongoza haki za watu.
 

Attachments

 • 20240506_211155_InSave_0.jpg
  20240506_211155_InSave_0.jpg
  123.2 KB · Views: 1
 • 20240506_211155_InSave_1.jpg
  20240506_211155_InSave_1.jpg
  139.6 KB · Views: 2
 • 20240506_211155_InSave_8.jpg
  20240506_211155_InSave_8.jpg
  135.2 KB · Views: 2
 • 20240506_211155_InSave_7.jpg
  20240506_211155_InSave_7.jpg
  142.7 KB · Views: 2
 • 20240506_211155_InSave_6.jpg
  20240506_211155_InSave_6.jpg
  120.7 KB · Views: 2
 • 20240506_211155_InSave_5.jpg
  20240506_211155_InSave_5.jpg
  114.5 KB · Views: 2
 • 20240506_211155_InSave_4.jpg
  20240506_211155_InSave_4.jpg
  186.7 KB · Views: 2
 • 20240506_211155_InSave_3.jpg
  20240506_211155_InSave_3.jpg
  200 KB · Views: 2
Back
Top Bottom