Katibu Mkuu Kiongozi wa Ikulu, rekebisha dosari hii

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,021
2,477
1075081
 
MIHIMILI YA DOLA AU NCHI
.
Naongelea Dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hii ni nchi moja yenye MAMLAKA MOJA.

Mamlaka hiyo imegawanyika katika mihimili mitatu muhimu.

Kuna Serikali, Mahakama na Bunge.

Rejea Katiba hapa chini, hasa kifungu cha 4(1) kinachoongelea "mamlaka ya utendaji," "mamlaka ya kutekeleza utoaji haki," na "mamlaka ya kutunga sheria."



1075091

1075092
 
Nakumbuka Civics ya Form 1

Government imegawanyika kwa:
1.Executive (Uongozi)
2. Judiciary (Mahakama)
3.Parliament (Bunge)

hivyo ndivyo haswaa! executive =uongozi . na kwa kuwa ameanza na serikali juu , wapo sawa tu,
 
.
Uongozi gani?

Wa Bunge?

Wa Kiserikali?

Wa Mahakama?

Kuna tatizo hapo.
hakuna tatizo mama

"The Executive Branch directs and oversees day-to-day operations of government"

Mbona iyo statement ipo wazi sana, tena Executive ndio inachukua % kubwa kwenye Serikali

mfano: Njoo Serikali za Mitaa, shuuli zote zile zinadondokea kwenye 'Executive'
 
Ingekua Chema kama ungetuma email moja kwa moja kwa katibu mkuu kiongozi au kwa ile idara ya serial inayoshughulika na TEHAMA.
.
Mimi nimechagua njia hii.

Sababu: Mie ni mwanahabari raia--citizen journalist.

Njia yangu ya kuwasiliana na watawala ni kutandaa namna hii.

Watawala wanapswa kuweka utaratibu mwafaka wa kunisikiliza kupitia mfumo huu pia.

Kwa hiyo, zile enzi za umevuka ngazi na kwenda juu bila kufuata mkondo wa kimamlaka zimepita.

Mambo ya ICT hayo!

Mabosi wakongwe bado yanawapa shida.

Lakini taratibu tutazoea.
 
Ingekua Chema kama ungetuma email moja kwa moja kwa katibu mkuu kiongozi au kwa ile idara ya serial inayoshughulika na TEHAMA.

Wote wamo humu humu, usishangae kwa email wasifanyie kazi. Sasa hivi hakuna kiongozi au mtumishi wa Muhimili wowote asiyeingia kwenye mitandao hasa jf. Ushauri mzuri lakini, ataandika na email isipokuwa humu jukwaani itabaki, sio kazi yao iwe kuwaza wizi wa kura tu.
 
@Watu wasiojulikana wanakuangalia tuuuu, huu utawala haukosolewagi hadharani
.
JF ni chanzo kimojawapo cha taarifa za kiintelijensia.
Unaowaita watu wasiojulikana wanaweza, na wanapaswa, kutumia uzi huu kuishauri serikali.
 
Back
Top Bottom