Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu, Dkt. Bashiru Ally unasumbuka sana. Rais Samia tarehe 30, Aprili atashinda kwa asilimia 100%

Pagan Amum

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
1,932
4,395
Dr. Bashiru juhudi zako unazofanya za chuki na hasira dhidi ya Rais wetu mpemdwa tukwambie tu unasumbuka sana.

CCM ni chama chetu, Tumekulia ndani ya CCM, tunazijua tamaduni zetu, tunazijua saisa za rough na nzuri za CCM. Tunakuhakikishia tu kuwa Rais Mama Samia Suluhu tunaenda kumpa Uenyekiti wa CCM kwa asilimia 100. Hakuna hata Mjumbe moja wa Mkutano Mkuu atamnyima Mama kura. Mama ni zao letu CCM na tunamjua.

Umekuwa ukifatiliwa sana mara kwa mara na tumegundua unafanya juhudi kubwa sana ili Mama asipata asilimia 100. Unasumbuka na unahangaika. Tarehe 30, April unaenda kupata pigo takatifu la Mwaka.

Ulibebwa na mfumo wa awamu ya tano, pamoja na kuwa You were outsider. Hukuijua CCM bali kwa muda uliokaa umekiua Chama kabisa. Sasa hili unalofanya huwezi kufanikiwa.

Tarehe 30, April 2021. Rasmi Mama tunaenda kumpa Chama ili naye akisuke mpya.
 
Andika ujinga wako lakini mali za CCM bado mtazitapika tu.

Bashiru hana muda wa kupoteza kwa huo ujinga wako.

Sina uhakika kama wewe ni mwana CCM bali una chuki zako tu.

Wana CCM hawapo wajingawajinga kama wewe kwenye mambo ya msingi.
 
Hii ya wezekana ni project na mtu kapewa na budget yake. Anazuia asipate 100% Au akipata 100% itasaidia nini?

Viwango alishaweka mwendazake JPM vya kumpima kiongozi. Avifikie atafanikiwa akishindwa imekula kwake bigtime. Si ajabu akajikuta analazimika kumuhitaji Doktori Bashiru atake asitake, unaelewa uhanga wa kimazingira wewe?
 
Kwa upande wangu CCM haina faida ulilingabisha na hasara ambazo tumepata kama taifa kwa kuwepo nadarakani. Wizi,uporaji wa ardhi, ufisadi ubadhirifu wa mali ya uma, ubabe, siasa chafu za kuuua na kubambikizia kesi, kufinya uhuru wa habari na mambo yote machafu yamekuwa ni sehemu ya utamaduni wa maisha chini ya uongozi wenu. You can go to hell, mmeleta hasara zaidi kwa taifa kuliko faida.
 
Andika ujinga wako lakini mali za CCM bado mtazitapika tu.
Bashiru hana muda wa kupoteza kwa huo ujinga wako.
Sina uhakika kama wewe ni mwana CCM bali una chuki zako tu.

Wana CCM hawapo wajingawajinga kama wewe kwenye mambo ya msingi.
Hizo mali ndiyo zimeshakwenda hizo! Hakuna wa kuzitapika tena! Muanzilishi wa huo mkakati ameshakwenda zake. Ccm imesharudi kwa wenyewe!

Bashiru na ccm wenzake makinikia, wataishi kama Mamluki tu ndani ya chama! Yuko wapi Polepole? Yuko wapi Ole Sabaya? Yuko wapi Albert Chalamika? Yuko wapi Kheri James?

Kwisha habari yao!!!
 
Unamuitaje "mstaafu" labda mimi sijui kiswahili vizuri (maana ya kustaafu). Anafanya rough gani tena huko? Kwa sababu nafasi zote mbili (Katibu mkuu wa chama na Katibu mkuu Kiongozi) zote hakustahili. Ameleta mikakati michafu sana ndani ya CCM, mikakati ya manunuzi ya "wanachama" na amechangia uchafuzi mkuu wa October 2020. Angetulia tu na hiyo heshima aliyoheshimishwa ya ubunge wa kuteuliwa wakati akijipanga kwa siasa za majukwaani kama ana uwezo nazo, maana huyu amekuwa ni wa kuteuliwa mwanzo mwisho.
 
Kwenye siasa kufuata makundi na falsafa fulani inaruhusiwa. Lakini hili jambo la kumchukia Bashiru kwa kua alitimiza majukumu yake vizuri na wewe ukaathirika si vema.

Kumgombanisha na Rais si sawa na ninaamini Rais ana vyombo ambavyo vinamsaidia na vitasema km Bashiru ni threat au la.

Ifike mahala tuwe tunareason kidogo tuache majungu na fitina ambazo hazitasaidia kujenga nchi hii.

Mimi na wewe tunaowajibu wa kujenga nchi hii kwa kutoa mawazo ya kujenga sio kufitinisha.

Rais pia anapaswa kutulia naona kuna miruzi mingi mno kipindi hichi.
 
Back
Top Bottom