KATIBU Mkuu Dkt. Slaa kuunguruma leo Tabora, Uwanja wa Shule ya Sekondari Uyuwi

CHADEMA

Verified Member
Apr 13, 2013
469
1,000

Akiwa ameingia mkoani Tabora kupitia Kaliua, Urambo na jana akafanya mikutano maeneo ya Mhulidede, Shitage na Bukumbi, wilayani Uyuwi, leo atakuwa na mikutano miwili eneo la Kakola asubuhi kisha jioni atafanya mkutano Uwanja wa Shule ya Sekondari Uyuwi, mjini Tabora, kuanzia saa 9 jioni.

Mikutano ya jana Shitange na Bukumbi na mapokezi ya Tabora mjini, wakati msafara wa Dkt. Slaa ukipita hapo kuelekea Uyuwi, Jimbo la Tabora Kaskazini.

Slaa kuhutubia Bukumbi 1..jpg
 

CHADEMA

Verified Member
Apr 13, 2013
469
1,000

Katibu Mkuu akihutubia Shitange


 

Attachments

 • Slaa kuhutubia Shitange 1..jpg
  File size
  1.2 MB
  Views
  1,700

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,903
2,000
Duh! Kweli Rais wetu kachuja. Yaani pamoja na hadhi hali ndo kama tunavyoiona?
 

Mr Suggestion

JF-Expert Member
May 2, 2011
605
250
Uyui au Uyuwi? kama ni Uyui basi karibu na shule ya mazoezi mwenge na pia karibu na uwanja wa Vita@ Kurugenzi ya Habari
 

mwahaja

JF-Expert Member
Aug 25, 2013
387
225
Ni kweli kabisa tupo hapa na maandalizi yameanza,vijana watafanya maandamano mafupi ya amani kutoka Student center jirani na Saut-Tabora kuelekea viwanja vya Uyui.Mungu tusaidie.
 

CHADEMA

Verified Member
Apr 13, 2013
469
1,000

Hapa ndipo zilipigwa nondo za ufisadi zilizoko kwenye Ripoti ya siri ya CHC kuhusu mashirika ya umma yaliyouzwa kiholela na serikali ya CCM. Hapa Dkt. Slaa alifichua siri kubwa kwamba serikali inamiliki (kwa siri?) asilimia 30 ya hisa za NBC kwa niaba ya Watanzania, lakini jambo hilo limefichwa.

Akabainisha nama ambavyo ripoti ya CHC imeandika kwamba NBC imepata hasara ya bil. 50 ambazo zinatakiwa kulipwa na serikali kwa ABSA na sasa serikali imelazimika kukopa tena kwa ABSA bil 250 ili kulipa mkopo huo hadi 2015.


 

Attachments

 • Slaa kuhutubia Urambo 2..jpg
  File size
  1.1 MB
  Views
  931

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
21,252
2,000
Taifa linahitaji ukombozi, Taifa hili linatakiwa kuzaliwa upya, Go on DR.Slaa -- Go on CHADEMA; tumaini pekee la watanzania.
 

CHADEMA

Verified Member
Apr 13, 2013
469
1,000
Shabaan Mambo.jpg

Mwenyekiti wa Kanda ya Magharibi, Shaaban Mambo, akiwajibika jukwaani
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom