Katibu mkuu CHADEMA ngoma nzito; Mchakato kuchukua mwezi mzima

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,596
36,018
Mchakato wa kumpata katibu mkuu mpya wa Chadema unatarajiwa kufanyika kwa mwezi wote wa kwanza wa mwaka 2016, imethibitishwa.

Wakati mchakato huo ukikaribia kuanza, John Mnyika mbunge wa Kibamba ndiye anayependekezwa na wengi ndani ya chama hicho kutwaa nafasi hiyo.

Aidha, kupitishwa kwa John Mnyika kunaweza kuimarisha chama hicho kwa kiasi kikubwa hasa baada ya kuzingatiwa kwamba ndiye mwanasiasa ambaye ameonyesha uelekeo wa siasa za @Dr.W.Slaa aliyekuwa katibu mkuu kabla ya kung'atuka ambaye siasa zake ziliweza kuleta mvuto wa hali ya juu ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

Mbali na hayo, wanachama wengine chama hicho unapendekeza katibu mkuu mpya kupatikana kanda ya ziwa ili kutawanya madaraka ya chama sehemu mbalimbali za nchi.

Kumekuwa na habari kuwa mrithi wa @Dr.W.Slaa huenda angekuwa Fredrik Sumaye aliyejiunga na chama hicho hivi karibuni habari ambazo zimekanushwa vikali na viongozi wa chama hicho.

Watu wengine wanaopendekezwa kutwaa wadhifa huo ni Salum Mwalim naibu katibu mkuu na Benson Kigaila.
 
G Sam wewe ni Mhandisi mwenzangu lakini kuna wakat huwa una mihemko
 
Hicho kipengele cha kutumia "Ukanda au Kabila" kumpata katibu naomba kisiwepo. Mtu apewe nafasi kutokana na uwezo wake, otherwise italeta mpasuko mkubwa.
 
mambo ya muhimu hayaitaji uharaka bali ni umakini na busara ndio huitajika. tuwaoatie mda cdm ili watupatie katibu mkuu makini.
 
Back
Top Bottom