Chademakwanza
JF-Expert Member
- Jun 11, 2014
- 6,346
- 1,871
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Taarifa inatolewa kwa vyombo vya habari na umma kuwa chama kupitia Ofisi ya Katibu Mkuu kimeanza kutekeleza mpango wa mafunzo kwa viongozi wa chama, wabunge pamoja na madiwani nchi nzima ili kutimiza kiu ya MABADILIKO kwa Watanzania, ikiwa ni moja ya maazimio ya kikao cha Baraza Kuu kilichomalizika jijini Mwanza hivi karibuni.
Pamoja na masuala mengine, Baraza Kuu lililojadili na kupitisha Mpango Mkakati wa Chama kwa miaka 5, liliazimia kwa kauli moja kuanza kwa mafunzo ya viongozi wa chama katika ngazi mbalimbali kuanzia chini hadi taifa na wawakilishi wa chama katika vyombo vya serikali, wakiwemo wabunge, madiwani na wenyeviti wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji.
Mafunzo hayo yameganywa katika awamu mbili, ambapo tayari timu 8 zenye wakufunzi 4 kila moja zimeanza kazi hiyo katika maeneo mbalimbali nchi nzima tangu Machi 16, 2016, zikiwa ni siku chache baada ya kumalizika kwa kikao cha Baraza Kuu.
Awamu ya kwanza ya mafunzo hayo itahusisha halmashauri zote 25 zinazoongozwa na CHADEMA ambapo chama kimelenga kuwajengea uwezo wa kuongoza na kusimamia halmashauri kwa ufanisi, kufikia MABADILIKO yanayotarajiwa na wananchi, ikizingatiwa umuhimu na nafasi ya Serikali za Mitaa katika mikakati ya maendeleo.
Katika awamu ya pili ya mafunzo hayo, Chama kimekusudia kuwajengea uwezo viongozi wa chama na madiwani kwenye halmashauri ambazo haziko chini ya CHADEMA, lakini kina wajibu wa kuimarisha kambi ya upinzani iliyo imara kutetea maslahi na matakwa ya wananchi katika mabaraza ya halmashauri husika.
Baada ya hapo yatafuatia mafunzo kwa ajili ya Kamati Kuu ya Chama, Kamati za Utendaji za Mabaraza ya Chama na Wabunge ambao wanao wajibu wa kuunda Kambi ya Upinzani iliyo imara inayowajibika kuisimamia serikali kwa niaba ya wananchi ndani na nje ya bunge.
Imetolewa leo Alhamis, Machi 17, 2016 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano