Katibu Mkuu CCM, tusaidie haya wilayani Kakonko

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Oct 7, 2020
1,382
1,246
Kwanza nichukuwe fursa hii kukukaribisha - KARIBU SANA

Pili, nikuombe utusaidie haya yafuatayo:-

(a) Jumuiya za chama
Hizi zianzishe miradi ya kiuchumi ili ziweze kuwa na nguvu za kiuchumi kwa ajili ya kupanua wigo wa utendaji kazi na kupunguza utegemezi kwenye chama - miradi ipo mingi sana iwezayo kuingiza mapato makubwa i.e kilimo cha kibiashara cha zao la parachichi aina ya Hass;

(b) Huduma za kijamii na kiuchumi

Tatizo la upatikanaji wa maji vijijini, umeme, na mtandao wa barabara za mashambani bado ni changamoto kubwa - kwa kuwa yapo mahusiano ya karibu kati ya siasa na huduma za kiuchumi basi tunaomba kasi ya upatikanaji wa huduma hizo uendane na mahitaji ya jamii;

(c) Malipo kwa makatibu, wenyeviti na wenezi wa ngazi ya tawi na Kata
Watendaji hawa ni muhimili mkuu wa ufanisi ktk kufikiwa malengo ya chama. Mara nyingi hata posho zinazotolewa na chama haziwafikii kwa wakati. Hawana uhakika wa kushiriki vikao kutokana na ukosefu wa nauli toka, taarifa za chama kuchelewshwa, nk
Posho kwa viongozi hao zitawasaidia kutekeleza majukumu yao na kujijenga kiuchumi;

(d) Mahusiano ya taasisi za umma vs jamii
Pamoja na mahusiano mazuri yaliyopo baina ya taasisi za umma kwa jamii lkn baadhi ya maeneo bado kuna changamoto i.e madereva wa vyombo vya moto hususan gari za kutoka Kakonko - Nyakanazi wana changamoto nyingi njiani (watakuambia); bodaboda za abiria na binafsi nao watakuambia.

(e) Makundi ndani ya CCM
Hapo wilayani upo mpasuko mkubwa ktk chama unaotokana na kura za maoni za mwaka 2020. Makundi hayo yakiendelea mwisho wake unaweza kuathiri CCM hapo baadae kwenye chaguzi (Diwani aliyeshindwa na aliyeshinda hawakai pamoja, hawashiriani vizuri, na hawashauriani ipasavyo).

Vinginevyo nichukuwe fursa hii kukutakia kazi njema

Msakila M Kabende
Economist / Political Analyst
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom