Katibu Mkuu CCM kufanya uzinduzi wa kukomaza demokrasia Mkoani Dodoma

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
368
1553207427010.png


Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Dk. Bashiru Ally anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kukomaza Demokrasia katika Mkoa wa Dodoma ambao utakwenda sambamba na ugawaji wa Ilani pamoja na vitendea kazi ambavyo ni nyezo.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma March 21 mwaka huu Katibu wa CCM mkao wa Dodoma Jamila Yusuph,amesma uzinduzi huo utafanyika Machi 23 mwaka huu jijini Dodoma.

Amesema,umuhimu wa mkakati huo wa kukomaza Demokrasia katika mkoa wa Dodoma, unalenga kufikia malengo na madhumuni ya CCM kwa mujibu wa katiba ya Chama hicho ya mwaka 1977 toleo la 2017, katika Ibara ya Tano ya katiba inachozungumzia malengo na madhumuni ya CCM.

“Kipengele kidogo cha kwanza kinazungumzia lengo na dhumuni kuu la CCM kushinda katika chaguzi za serikali za mitaa na chaguzi kuu kwa upande Tanzania bara na Zanzibar ili kuunda na kushika dola kwa maana ya kuunda na kushika serikali kuu na serikali za mitaa katika jamhuri ya muungano wa Tanzania na Zanzibar,”alisema.

Amesema, wanapozungumzia kukomaza demokrasia katika mkoa wa Dodoma maana yake ni kuzingatia vipengele vya inamanisha ni pamoja na kuimarisha misingi ya uongozi bora, uwajibikaji kwa viongozi na wanachama, kulinda na kudumisha nidhamu ya wanachama, kuongeza kiwango cha ushiriki kwa wanachama katika shughuli za maendeleo, ulinzi na usalama katika maeneo yao, kulinda na kudumisha nidhamu ya wanachama.

Jamila amefafanua kuwa, mashina ndicho chombo kinachodhihirisha uwepo wa uhai na nguvu ya chama, ndio daraja la mawasiliano baina ya chama na wananchi ambao ndio wanatoa lidhaa ya CCM kuendelea kushika dola,

Pia ameongeza kuwa, shina limeonekana kama ni chombo muhimu cha kisiasa cha kuunganisha wanachama pamoja na umma, ili kufanikisha dhumuni la kwanza la kukiwezesha chama kuchukua hatua za haraka katika kushughulikia kero za wananchi katika eneo husika, lina uwezo wa kukifanya chama kuendelea kukubalika na kuwa kimbilio la wananchi walio wengi.

“Sisi kama mkoa wa Dodoma mkakati huo wa kukomaza demokrasia mashinani kisiasa kimuundo na kiuchumi ni wajibu wetu, hivyo tunategemea kuutumia mkakati huo kufikia maelngo mbalimbali,”alisema.

Aidha ameyataja malengo hayo kuwa ni kupata ushindi wa kishindo katika chaguzi zijazo za dola kwa maana ya uchaguzi wa mwaka 2019 na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 na katika hilo wanataka watanzania wasikie na dunia ujue kwamba wanaDodoma wameamua kuunga mkono serikali ya CCM ya awamu ya Tano, ambayo inaongozwa na rais wao mpendwa na mwenyekiti wa CCM taifa, Dk.Magufuli.

Mkakati huo pia utawezesha viongozi wao kujenga mahusiano mazuri baina ya viongozi wa Chama na serikali, viongozi wa taasisi za kidini, wazee maarufu na makundi mbalimbali katika meneo yao.

“Utatoa msukumo wa ujenzi na ukarabati wa ofisi za chama, hasa katika ngazi za mashina na matawi na utawasaidia kuhakikisha kuwa maagizo na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na chama yanatekelezwa ipasavyo na kwa wakati katika mkoa wa Dodoma”alisema.
 
Back
Top Bottom