Katibu Mkuu CCM, Dr. Bashiru: Siasa za kuabudu watu ni ushirikina

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Messages
33,734
Points
2,000

Chakaza

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2007
33,734 2,000
Kama Katibu mkuu was Chama chao CCM kashtuka na kusema siasa za Kuabudu mtu badala ya chama in ushirikina nyie wengine mtashtuka lini?

Natamani sana Dr Bashiru angekuwa na verified account hapa JF na ujumbe huo akawapa waabudu sanamu waliomo humu.

Je, nini kimemtokea hadi Kuabudu mtu (obviously ni kumuabudu Magufuli) aone ni ushirikina?

Je, washabiki wa Kuabudu mtu JF wanajifunza nini?

---
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dkt Bashiru Ally, amewataka wanachama wa chama hicho kuacha siasa za kuabudu watu badala ya chama, kwani kufanya hivyo ni kutekeleza siasa za kishirikina.

Dkt Bashiru ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Mabalozi na viongozi wengine wa chama hicho, katika Manispaa ya Bukoba, mkoani Kagera.

"Kuabudu watu ni ushirikina, wanaotaka kutukuzwa na kujifanya wao ndio wanaweza mambo, wanafanya siasa za kishirikina"

Aidha amewataka kuacha kufanyiana fitina ndani ya chama kwa kuwa fitina zina malipo yake, "Siwezi kuwazuia kunywa sumu kama mmeamua kufanya hivyo, lakini siwezi kuogopa kuongea ukweli"

bashiru.jpg
 

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Messages
21,064
Points
2,000

Retired

JF-Expert Member
Joined Jul 22, 2016
21,064 2,000
Huyu Bashiru hana nia njema, yeye anasema wanaomuabudu say Membe, Makamba, Kinana etc (wale wapinzani wa CCM wenye nguvu wasiabudiwe) wasiabudiwe ila Jiwe ndiye aabudiwe! Ndicho anachomaanisha. Usidhani alikuwa na maana ya kuwa watu wasimwabudu Jiwe! Never!
 

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Messages
1,273
Points
2,000

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2019
1,273 2,000
Ungejua KM dkt.Bashiru anamtaja Mbowe na Zitto Wala usingehitimisha hivyo. Nakupa mazingira ya kuthibitisha ninachosema:

1. WanaCHADEMA kwa kauli zao wenyewe wamenukuliwa wakisema" mwamba tuvushe hakuna mwingine zaidi yako" huo ni ushahidi tosha wa siasa za kishirikina anazosema ndg.bashiru ambazo zinafanywa na CHADEMA.

2. Zitto amekuwa akijitapa kujua kila kitu na wanachama wake kuamini kuwa ni kweli anajua kila kitu mpaka kujipachika cheo Cha Ayatollah ndani ya chama Cha siasa ambacho hakihojiwi na wanachama hawajawahi kuhoji.

3. Mwingine anayesemwa na Bashiru ni Maalim Seif anayeamini Zanzibar imeumbwa kwa ajili yake na ana hati miliki ya kuongoza Zanzibar

4. Naomba niishie hapa ila niishie kusema Bashiru ni daktari na kawapiga chenga ya mwili
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2019
Messages
2,834
Points
2,000

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2019
2,834 2,000
Kinachowaponza wafuasi na wanachama wa Ccm ni njaa na unafiki! Kesho Magufuli akiondoka madarakani, wote wanamgeuka na kuanza kumsujudia yule atakayekuwepo kwa wakati huo, huku wakimnanga aliyeondoka kwa kila aina ya maneno ya kejeli, dharau, nk.

Hao ndiyo ccm. Huwa wanabadili gia angani, ndani ya dakika sifuri.
 

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Messages
33,734
Points
2,000

Chakaza

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2007
33,734 2,000
KARLO MWILAPWA,
Usigeuze maneno, akiwaambia wanachama wa chama hicho (chake) sasa hao aliokuwa akiongea nao ni Chadema?
Mnakuwa na akili kama za watoto katika kuficha jambo?
Acheni siasa za ushirikina, mmeonywa!
(Hapo kwenye ushirikina nadhani amechanganya na yale ya chumba kisicho funguliwa kule waliko likizoni)
 

Forum statistics

Threads 1,389,914
Members 528,056
Posts 34,038,496
Top