Katibu Mkuu CCM Dk Bashiru Ally ampongeza Askari aliyekataa kutoa salamu ya CCM kwenye mkutano

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
2,672
2,000
Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amempongeza askari polisi mkoani Pwani aliyegoma kutumia salamu za chama hicho tawala nchini kwa maelezo kuwa ni kinyume na maadili ya kazi yake

Amesema "Nampongeza yule askari polisi aliyekataa kupokea maagizo ya Kiongozi wa CCM, nimeshampigia simu IGP kumwambia ampe pongezi kwa sababu alisimama katika maadili ya kazi yake"
******

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Dk Bashiru Ally amempongeza askari polisi wa mkoani Pwani ambaye siku za hivi karibuni aligoma kutumia salamu ya ‘Kidumu Chama cha Mapinduzi’ inayotumiwa na chama hicho tawala nchini Tanzania.

Askari huyo aliombwa kutoa salamu hiyo na mjumbe wa halmashauri Kuu Taifa ya chama hicho, Haji Jumaa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Vianzi wilayani Mkuranga, kabla ya kueleza kero za kufungwa kituo cha polisi muda wa kazi.

Hata hivyo, askari huyo aligoma akisema maadili ya kazi yake hayaruhusu kutoa salamu hiyo, akidai ni kosa kimaadili.

Dk Bashiru ametoa kauli hiyo leo Jumanne Agosti 27, 2019 katika mkutano wa wanachama wa CCM wilaya ya Ubungo ikiwa ni sehemu ya ziara yake iliyoanza leo ya kukagua uhai wa chama, miradi ya maendeleo na kuzindua mashina.

Akitoa mfano wa tukio hilo, Dk Bashiru amesema CCM haiwezi kuwa chombo cha nidhamu kwa watumishi wa umma.

"Nampongeza yule askari aliyegoma kufuata maelekezo nataka nimjue hata IGP nilimpigia simu kuhusu tukio hilo.”

"Polisi hapokei maelekezo ya chama chochote cha siasa iwe CCM au CUF. Kama una jambo usibwatuke tu, sitaki kusikia amri au maelekezo yoyote, tukiendelea na tabia hiyo tutakuwa tunajenga nchi isiyofuata sheria,” amesema Dk Bashiru.

Amebainisha kuwa watumishi wa umma wana vyombo vyao vya kuwajibishana na wakati mwingine hupeana adhabu.


Zaidi, soma;
 

mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,562
2,000
Asihofu kwani hakuna asojua kuwa kila mfanyikazi anolipwa mshahara hulipwa na serekali ya ccm. Hivyo, ni kosa kutokukijali chama kinacho kulipa posho yako
 

lukesam

JF-Expert Member
Feb 23, 2015
10,686
2,000
Dk. Bashiru anatakiwa amkamate yule kada aliyekuwa akimlazimisha askari kukiuka maadili ya kazi yake na amtandike viboko vya makalio hadharani TBC One ikiwa live.

Hakuna sababu ya kulea makada wa hovyo hovyo wasio na hoja wanakomalia vitu vya kijinga.
 

Zionist

JF-Expert Member
Dec 5, 2017
1,601
2,000
Mimi kama mzalendo wa nchi yangu, simo kwenye siasa wala sina chama, kile kitendo kiliniuma sana, na mpaka sasa hivi nina hasira. Yaani Kumlazimisha yule afande mwenye taaluma yake, na kiapo chake cha weledi ni sawa na kumtukana hadharani.kweli yule afande anajielewa, ila kwa Bashiru: ni wakati wa kuwawekea mipaka watendaji wenu wa chama.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom