Katibu Mkuu CCM (Chongolo) amtaka Waziri wa Maliasili na Utalii, Pindi Chana kujiuzulu

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
chongolo-pic-data.jpg
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amemtaka Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Pindi Chana kuachia nafasi hiyo na kuruhusu mamlaka za uteuzi zifanye maamuzi mbadala, iwapo ameshindwa kudhibiti changamoto ya tembo wanaoharibu mazao ya wananchi wilayani Meatu katika Mkoa wa Simiyu.

Kauli hiyo ya Chongolo imekuja baada ya miezi mitatu tangu Rais Samia Suluhu Hassan alipoiagiza Wizara hiyo kushughulikia changamoto hiyo.

Katika maelezo yake alipokuwa ziarani Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu leo Jumatano Juni Mosi, 2022, Chongolo amesema kuwapo kwa changamoto hiyo hadi sasa ni ishara kwamba Wizara husika imekaidi au kudharau maelekezo ya Rais.

"Hatuwezi kuwa na watu wanaoagizwa na Rais juu ya kuchukua hatua hawafanyi wanakaa ofisini, hii inaleta matatizo kwa wananchi na inaonyesha dharau kwa aliyekuagiza," amesema.

Amewahakikishia wananchi ndani ya mwezi mmoja uongozi wa wizara hiyo utakwenda eneo hilo kwa ajili ya kutatua changamoto hiyo.

Ameongeza kuwa CCM haitaridhia kuona wananchi wanateseka ilihali kiliomba ridhaa ya kuwaongoza vyema.
 
wao wanapiga siasa tuu, lakini vyama vingine marufuku, angekuwa mnyika ndiyo katoa hayo matamshi kesho tuu angeitwa central au kwa msajiri wa vyama kuchukuliwa maelezo!
 
Nimewaambia uzeni zile meno za tembo pesa mkenge uzio maeneo ya hifadhi na watu hamsikii..

La sivyo ua hao tembo waliozidi kwenye hifadhi..

Mtatajua wenyewe cha kufanya..

Twende kwa mwendo huu huu.
 
Back
Top Bottom