Katibu Mkuu BAVICHA amshindilia kaa la moto Mwigulu Nchemba na Nape

Mwigullu na Nape hivi sasa ndo threat kubwa kwa CDM nini? mbona watu wadogo sana hawa inakuaje wawe tishio kiasi hiki, hapo SANGARA hawajaunguruma. Hakika CDM ni dhaifu, kila siku Nchema, Nape. Siyo vipaumbele vya maendeleo.

Hapo ndo level yako ya kufikiri ilipoishia siyo??? Hebu tupatie vipaumbele vya maendeleo vya hao unaowatetea!
 
Mimi nionavyo hata wabaya wa CCM nao wamejaribu kila jambo kukichafua bila mafanikio bado CCM ni mwendo mdundo. Wananchi wangependa kusikia sera watafanyiwa nini na wapinzani kuliko hili la kuwa na lengo moja tu la kukingo'a CCM madarakani, wakishaking'oa wananchi nini kitafuatia? huu naona kama utapeli mkubwa wa wapinzani. Wananchi ni lazima tulishtukie hili.

Mkuu kwani CCM wao wanatufanyia nini vile???
Kutuua wananchi wake ili wao wabaki madarakani sio???
Au
Kuwabandikia wananchi kesi za uongo sio???
Au
Kutuibia rasilimali zetu wakishirikiana na wazungu pamoja na wahindi sio???
Au
Kuuza wanyama hai ughaibuni sio???
Orodha ni ndefu sana, give a break.
 
Mimi nionavyo hata wabaya wa CCM nao wamejaribu kila jambo kukichafua bila mafanikio bado CCM ni mwendo mdundo. Wananchi wangependa kusikia sera watafanyiwa nini na wapinzani kuliko hili la kuwa na lengo moja tu la kukingo'a CCM madarakani, wakishaking'oa wananchi nini kitafuatia? huu naona kama utapeli mkubwa wa wapinzani. Wananchi ni lazima tulishtukie hili.

We kichaa nini?Utafanyaje kitu bla kumuondoa anayehamishia resources za kufaonyia kitu mifukoni mweka...ukivamiwa na mwizi utapambana na mwizi au utang'ang'ana kurudisha alivyoviiba ndana? oviasly utahakikisha mwizi anaangamia kwanza ndipo uhakikishe usalama wa mali zako...CDM ndo sisi wananchi,tunahakikisha mwizi (CCM)anaangamia ndipo turudishe mali zetu..
 
Naona unatekeleza hilo agizo hapo chini: CHAMA CHA MAPINDUZI KUHUISHA MTANDAO WA WANA CCM KATIKA VYUO NA MASHINA YA WAKEREKETWAKumetokea na sura tofauti katika hali ya kisiasa nchini hivi karibunikufuatia propaganda za CHADEMA kutaka kujipatia umaarufu na kujitafutia uhalalikwa njia ya kuichonganisha serikali na wananchi na kupandikiza chuki dhidi yaChama cha Mapinduzi. Hali hii imedhihirishwa na juhudi za makusudi zilizofanywana chama hicho za kupotosha ukweli, kutokuona ukweli na kung’ang’ania uzushikuwa ndio mtaji wao wa kisiasa bila hata kujali masilahi ya Taifa na misingi yautu iliojengwa kwa wananchi wake. Kwa mfano kumekwepo na upotoshaji wa kuwahakuna uthubutu wa serikali ya awamu ya nne, ubunifu, kubeza mafanikio nawakati mwingine kuropoka kuwa hakuna mafanikio yaliofikiwa tangia uhuru. Piakumekwepo na lawama kuhusu kupanda kwa gharama za maisha bila hata kuzingatiachanzo cha gharama hizo kinatokana na nini badala yake lawama zinatolewa kamavile bei zimepandishwa na Chama na Serikali na viongozi wake.Hii imesababisha baadhi ya wananchi kwa kutokujua ukweli kupotoka nawengine kushabikia nadharia bila kutaka ukweli na bila kujali madhara yaushabikiaji wa vitu vya kizushi kuwa una athiri umoja, aman, utulivu nahata shughuli za uzalishaji . matokeoyake tumekuwa tukishuhudia vitendo vya uvunjifu wa taratibu maeneotofautitofauti.Baadhi ya vitu vilivyochangia kukua kwa wimbi hili katika vyuo vikuu na maeneo mengine kamailivyoelezwa katika kikao cha baadhi ya wabunge vijana na viongozi na wanachamawa vyuo vikuu vya mkoa wa Dodoma ni
  • Kudhofika kwa UVCCM na vitengo cha propaganda vya CCM kwa ngazi zote kiasi cha kupungua kwa watu wa kukitetea chama na kuelezea mafanikio yaliopatikana kutokana na jitihada za serikali yake.
  • Kupungua kwa moyo kujitolea kufanya kazi za chama kwa wa CCM wakati usio wa uchaguzi na kuyaacha baadhi ya makundi kama vijana bila mawasiliano mpaka wakati wa Uchaguzi. Kukosekana kwa mikutano na wanachama kwa viongozi wa vijana Taifa hata ile isio rasmi kiasi cha kuwafanya wafuasi wa CCM vyuoni kuwa wapweke.
  • Kutokufanyika kwa semina za mara kwa mara kwa wanafunzi zinazohusu fursa hivyo kuwafanya wakate tama na kupotoshwa kirahisi kwa kauli za vitisho za wapinzani.
  • Kutokuwafanyia semina za mara kwa mara kwa wakereketwa wa CCM walioko vyuoni ili kuimarisha uhusioano na chama na serikali na kujua undani wa chama, sera na mafanikio yaliofikiwa na serikali ili kuwa na mwelekeo wa pamoja na kauli ya pamoja wanapoitetea serikali
  • Wanafunzi walio wana CCM kukosa mawasiliano hata ya kufikisha taarifa za siri punde kunapokuwepo na vuguvugu vyuoni na pia hakuna mtandao wa kuwafikishia taarifa hata wafuasi wa CCM kuhusu hatua zinazochukuliwa na serikali kuhusu malalamiko ya wanachuo.
  • Kutokuwepo kwa udhibiti wa kauli za wahadhiri wanapoibeza serikali wanapofundisha na wakati mwingine kufanya kampeni za wazi wazi darasani kinyume na sheria za utumishi wa uma za kutokufanya siasa mahali pa kazi.
  • Kutokuwepo kwa udhibiti wa vurugu wanazofanyiwa wafuasi wa CCM na wanafunzi wasiounga mkono migomo. Wakati mwingine wanafunzi wanafanyiwa fujo kwa kuvaa sare za CCM na kuzuiwa kutoka maeneo ya vyuo kwenda katika mikutano.
Kwa upande wa Mashina ya wakereketwa kumetokea malalamiko ya vijanakutotumika kwenye shughuli za kisiasa mpaka wakati wa uchaguzi. Pia kumekwepona malalamiko ya kukosekana kwa ufafanuzi punde chama au viongozi wakuu wanapokuwawamepakwa matope hivyo kuwafanya wafuasi wa CCM kuanza kuzomewa mitaaniwanakoishi kuwa wameshindwa kujibu.
  • Hii inawavunja nguvu wakereketwa wanapoambiwa kutokujibiwa malalamiko au matope yaliorushwa ni ishara ya ukweli.
  • Pia kimekosekana kitengo cha propaganda na kutawala vyombo vya habari hata vilivyo vya serikali kiasi kwamba hata panapokuwa pameandikwa habari ya CCM, wapinzani ndio wanakuwa wameiandika hivyo kuwa na madhara kwa Chama.
Mapendekezo
  • Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu na ofisi ya mnadhimu mkuu ziongezewe nguvu ili zifanye shughuli ya kwenda hatua zaidi ya wapinzani kwa kuwa na watu wanaoshughulikia mambo haya. Vinatakiwa viwepo vitengo vya propaganda kwa kila ngazi viwezeshwe na kuratibiwa ili viende sambamba na matukio makuu katika kalenda. Kwa mfano maadhimisho ya CCM yawe na midahalo ya wana CCM, wanavyuo wetu na wananchi kwa ujumla, siku ya akina mama iwe na midahalo, sikukuu ya mungano iwe na midahalo na yafanyike maandalizi na fursa hizo zitumike kukosoa wale ambao wamekuwa wakileta lugha zenye madhara kwa hatima ya mungano nk.

  • Kuwepo na kikundi maalum katika ofisi ya umoja wa vijana na wabunge vijana kushirikiana na ofisi ya Chama taifa, ofisi ya waziri anayehusika na mahusioano na uratibu na mnadhimu mkuu kushughulikia kupangua hoja za kizushi za upinzani na kutoa mapendekezo staiki kuhusu kutengeneza mtaji wa kisiasa kwa makundi mbalimbali ya jamii.
  • Kikosi hicho kiimarishe mtandao kwa wanavyuo wanaomaliza masomo wajulikane walipo na ikibidi wawezeshwe ili wafanye kazi ya kukisemea vizuri chama popote walipo na wawe chachu pale mahali pa kazi walipo.
  • Kitengo hicho kiratibu midahalo na kutafuta wana CCM wanaoweza kuwa na majibu mazuri zaidi kulingana na uhusiano wa maada husika na utalaam na uzoefu wa msemaji anaestahili kushiriki
  • Kuhamasisha wana CCM kushiriki midahalo kwa njia za simu na wakati mwingine kuwaweka wana CCM kimkakati kushiriki mjadala hiyo tokea sehemu mbalimbali maada inapokuwa na mvuto wa kisiasa, masilahi ya kitaifa na chama chetu
  • Kupitia mwavuli wa Ofisi ya mahusiano na uratibu kitengo kiwe na uwezo wa kujibu kila hoja kwa kupata ushauri, majibu stahiki na makubaliano tokea kwa wataalam na wakuu wa wizara husika inayoguswa na agenda.
  • Kikundi kihusike na kutembelea wanavyuo na kufanya mawasiliano ya uamzi wa chama na makusudio ya serikali kutengeneza wasemaji wa agenda za serikali ndani ya jamii.

  • Kikosi hicho kishirikiane na wabunge wa kila jimbo kutembelea shule za sekondari kwani hao ndio wanavyuo wajao na wapiga kura wa uchaguzi ujao. Ni vyema pia ifanye mikutano ya hadhara nchini kote punde zinapotokea kauli za kukishambulia chama chetu. Wahusike wanachama, viongozi wa wilaya, mikoa na wabunge kukanusha na kulaani kauli za uongo. Hili liratibiwe na ofisi ya chama makao makuu, mikoa, wilaya, kata na matawi.

  • Kitengeneze utumiwaji wa wataalamu wa fani mbalimbali kufanya mawasilianao kwa njia ya SIMU NA INTERNET kueneza sera za chama na kazi za serikali.
  • Kuwepo muda maalumu na kikundi maalumu cha wabunge wa kuandaliwa kupeleka hoja au kujibu hoja watakaoweza kufanya hivyo kwa hisia za juu kuleta msisimko wa kisiasa na kuwapa moyo wana CCM pote walipowasiwe wanyonge.
  • Kutengeneza mtandao wahadhiri watakaokuwa wanakisemea vizuri chama mahali pakazi
  • Kufanya tafiti za siri kuhusu misimamo ya wateule wa nafasi mbalimbali kwa chama ili kuepuka hujuma na usaliti wakati wa uchaguzi.
  • Kukutana na viongozi wa kidini kuwaweka sawa na kutambua kuwa chama kinawajali na kujua umhimu wao katika amani ya nchi
  • Kukosi pia kitakuwa kinahusika kutengeneza mtazamo wa pamoja kuhusu jambo linalohusu nchi na kutafuta watu maeneo tofauti kulisemea jambo hilo, mfano mambo ya kuzingatiwa katika katiba mpya.
  • Kuanzisha ofisi, matawi na kuratibu upatikanaji wa wana CCM kushika uongozi kwenye serikali za wanafunzi.
  • Kuhusu vijana wa kwenye majiji na mijini na miji midogo wasio na ajira, wizara ya inayohusika na biashara na wizara inayohusika na vijana iangalie namna ya kutekeleza mpango maalumu wa kuwarudisha vijana walioasi chama kwa madai ya hali ngumu ya maisha.
  • Kwa mfano wizara husika zinaweza kufanya sensa na kupata idadi ya vijana wanaoweza kutambulika na kukopesheka halafu watafutiwe supplier maalumu aagize kwa jumla pikipiki na bajaji halafu zikopeshwe kwa vijana badala ya utaratibu wa sasa wanaoajiriwa na kupeleka hesabu kwa matajiri wao, wapeleke hesabu kwa supplier na punde deni likiisha pikipiki zinakuwa za kwao. Lakini mpango huo ufanyike kimkakati ili uweze kuleta manufaa kwa chama.
  • Mfano wa mkakati ni kwanza kufanyika kampeni ya kukaa vikao vya ndani na vijana kila miji watakao pata kwa kila awamu watakuwa chachu.
  • Mfano wa pili ni kuwakusanya vijana ambao wana ufundi wowote wawezeshwe halafu wafanye kazi na serikali. Kwa mfano wanaoweza kutengeneza madawati wajulikane watengeneze madawati ya shule zote za misingi, sekondari na vyuo kwa ushirikiano na serikali.
  • Utekelezaji wa ilani ya uchaguzi uwahusishe wananchi ili waone vinavyofanyika pamoja na wabunge kutumia fursa hiyo kuwaeleza kuwa kinachotekelezwa kilikuwepo kwenye ahadi. Kwa mfano vitabu visigawiwe kimyakimya kwa kuwatumia watendaji wa sekta ya elimu kuwakabidhi waratibu na waratibu kuvifikishia ofisini bali kuwe kunafanyika mikutano inayohusisha wanafunzi na wananchi ili wajue hatua zinazochukuliwa. Ifanyike hivyo kwa huduma za afya, kwa maabara, umeme n.k kwa kadri itakavyowezekana.
  • Hii itapunguza wananchi kudanganywa mathalani walikuwa wanaambiwa wao ndio wamejenga shule za sekondari za kata sio serikali ya CCM lakini ukweli ni kwamba mchango wa wananchi kwenye ujenzi wa madarasa, nyumba za walimu, zahanati na vituo vya afya ni maboma peke yake na mambo yote yanayosalia ni fadha za serikali. Utaona kuwa fedha ya serikali ni kubwa lakini kwa kuwa zinatoka kimya kimya kwa njia ya akaunti wananchi wakiambiwa wamejenga wanadhani ni michango yao imefanya kila kitu.
“WE STILL HAVE THE CONTROL OF THE MATCH” MUNGUIBARIKI CCMMUNGUIBARIKI TANZANIA MWIGULU LAMECK NCHEMBA (MB) JIMBO LA IRAMBA MAGHARIBI
Wanalicheza Gwaride la Chadema pasi kutaka.
 
Wanalicheza Gwaride la Chadema pasi kutaka.

wamesahau kwamba ccm hakuna mtu anayetaka wananchi wanufaike. Tulipofikia ni pabaya sana, yaani mtu anaagiza wale wahadhili wanaoisema serikali waadhibiwe aafu anataka watafutwe wa kukisemea chama mahala pa kazi!! Kuisema serikali hakujaanza juzi tena siku hizi kumepungua kuliko kawaida!! Wamefikia hatua ya kutaka kuajiri watu kwa tiketi ya chama,hii ni kuonesha wameshindwa kutekeleza yote yanayofaa kwa nchi hii!!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom