Katibu Mkuu BAVICHA amshindilia kaa la moto Mwigulu Nchemba na Nape | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katibu Mkuu BAVICHA amshindilia kaa la moto Mwigulu Nchemba na Nape

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Scolari, Jul 23, 2012.

 1. Scolari

  Scolari JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2012
  Joined: Aug 4, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kutoka Ifakara:

  Katibu Mkuu wa BAVICHA Deogratias Munishi amemshukia vikali Mwigulu Nchemba na Nape kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kata ya Mkamba.

  Munishi amedai kuwa Mwigulu alikodi vijana kutoa Manzese na kuwapeleka Iramba ili kumuwinda John Mnyika na kuvuruga mikutano ya Chadema iliyokuwa inafanyika Singida lakini hawakufanikiwa baada ya wanannchi kuwadhibiti kisawa sawa.

  Aliwaambia wananchi kuwa vijana hao ni sehemu ya vijana waliopewa mafunzo maalumu ya kudhuru watu kipindi cha uchaguzi mdogo wa Igunga mwaka jana yaliyofanyika Iramba Singida na Uyui Tabora.

  Katika mkutano huo ambao pia ulihutubiwa na mwenyekiti wa BAVICHA John Heche, Munishi amemgeuzia kibao Nape Nnauye kwa kusema kuwa CCM ndio chama cha kigaidi kwa kuwa kimekuwa kikiendesha vitendo vya kigaidi dhidi ya wananchi akitolea mifano uvurugaji wa mikutano ya Mchungaji Msigwa yenye lengo la kutaka kudhuru wananchi kule Iringa, yaliyofanyika hivi majuzi Singida, umwagaji wa tindi kali kule Igunga, na vitendo vya kigaidi vilivyofanywa na CCM kwenye uchaguzi mdogo wa Arumeru.

  Amewataadharisha wananchi kuwa CCM inaandaa mauaji ya halaiki Tanzania kwa vitendo vyake hivyo waiogope kama ukoma.
   
 2. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Nahisi kuna kesi mbili zitafunguliwa na PoliCCM hivi karibuni dhidi ya Munishi na Heche. Wameingia kwenye 18 ya CCM.

  Mpaka mwisho wa mwaka huu kila kiongozi wa CDM atakuwa na at least kesi 3 mahakamani. Zikiwa zimetawanyika kona kadhaa za nchi.

  Hili kuta la mwisho la ubabe wa CCM litamegeka hivi karibuni kwa kuzidiwa na uzito wa ngvu ya wananchi. Baada ya hapo bila shaka CCM watatumia JWTZ kulinda maslahi yao.

  JWTZ na CCM ni damu damu, moja ya triki ni kuzima kesi zote za wizi na ubadhirifu ndani ya JWTZ zilizoko mahakamani,
  kwa kisingizio cha kukosa ushaahidi, na kuamuru watuhumiwa kulipa fadhira kwa kuibeba CCM.

  Unaondoa PoliCCM mtaani unaweka askari wa JWTZ
   
 3. Advocate J

  Advocate J JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 3,880
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  wananchi fungukeni chama kinachotawala ndo kinaleta machafuko kama vp kipeni likizo ok
   
 4. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Hongera BAVICHA, kwa hiyo mikutano ya CDM sasa imekuwa narrowed to Mwigulu na Nape. Inaonekana CCM ilikuwa haijafahamu size ya CDM.
   
 5. M

  Molemo JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mkuu,size ya Nape na Mwigulu ni Bavicha tu.
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  ccm inakufa huku inajiona..
   
 7. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,959
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  jembe unafika huku! Mi nilifikiri uko jukwaa la elimu tu. Duuuh!
   
 8. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,959
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  Bavicha hebu dili na hawa wapuuzi!
   
 9. mathematics

  mathematics JF-Expert Member

  #9
  Jul 23, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 3,295
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 160
  and soon will buried!
   
 10. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Kila ccm inachojaribu kinastukiwa sasa wajaribu kutumia style ya Syria
   
 11. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mwigullu na Nape hivi sasa ndo threat kubwa kwa CDM nini? mbona watu wadogo sana hawa inakuaje wawe tishio kiasi hiki, hapo SANGARA hawajaunguruma. Hakika CDM ni dhaifu, kila siku Nchema, Nape. Siyo vipaumbele vya maendeleo.
   
 12. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #12
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  CCM ni imara ndioyo maana wana JF mliotumwa hamlali, CDM wenyewe hawalali kila siku majungu, fitina na chuki. Hiyo ndo ishara ya Uimara wa CCM kwani kisingekuwa imara wabaya wake wasingetapatapa kwa maneno matupu.
   
 13. M

  Mabala The Farmer Member

  #13
  Jul 23, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  BAVICHA kazeni mikono, tupo nyuma yenu kwani naamini nguvu ya uma ndiyo ya umoja,hakuna kuogopa.We are beleving to "CHEVEGUARA" who says that, Impacts leading to Revolution.
   
 14. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #14
  Jul 23, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,936
  Likes Received: 673
  Trophy Points: 280
  kweli wewe ni kenge

  kwa tanzania ya leo unaleta ukenge wako kwa maslahi yako na makenge wengine
   
 15. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #15
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mimi nionavyo hata wabaya wa CCM nao wamejaribu kila jambo kukichafua bila mafanikio bado CCM ni mwendo mdundo. Wananchi wangependa kusikia sera watafanyiwa nini na wapinzani kuliko hili la kuwa na lengo moja tu la kukingo'a CCM madarakani, wakishaking'oa wananchi nini kitafuatia? huu naona kama utapeli mkubwa wa wapinzani. Wananchi ni lazima tulishtukie hili.
   
 16. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #16
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Lazima utasema hivyo kwa vile umekwisha pigwa upofu wa kutotafakari mambo, na badala yake umebaki kutukana tu. Endelea hivyo lakini mwisho wa siku ukweli utajulikana.
   
 17. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #17
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Wewe ulitegemea Mwigullu awe size ya nani? SLAA au Mbowe? tehe tehe tehe CDM bwana mnajikanyaga kweli.
   
 18. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #18
  Jul 23, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwani mbona ccm imekuwa Kama Chama cha upinzani tena Mikutano ya nini badala ya kutimiza ahadi?
   
 19. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #19
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  CDM mbona mnajinadi sana kwa kukiponda CCM? waambieni wananchi nini visuion na mission yenu. AU ndo msemo wa kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza? CCM kimetulia CDM wanajiuza siyo? jiuzeni kwa bei halali basi siyo bei feki.
   
 20. P

  Pwito Senior Member

  #20
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 177
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wengine tumejiandaa na manzishi yake maana lazima yafanane na ya Mandela sababu yanasubiriwa kwa dizaini moja yaani wote ni marehemu hai
   
Loading...