M
MegaPyne
Guest
Katibu Mkuu wa wizara ya Utalii Tanzania Bibi Blandina Nyoni juzi alikesha katika banda la Tanzania akiuza utalii na kutoa huduma kwa watu mbalimbali waliofika katika banda hilo kwa kuwafahamisha mikakati ya Serikali ya awamu ya nne kwenye sekta ya utalii.
Katibu Mkuu alikuwa akiyafanya hayo katika mkutano wa siku tatu ulianza jumatatu wa soko la wasafiri duniani World Travel Market uliofanyika katika Excel pembeni kidogo ya jiji la London.
Akionekana kama mama mwenye nyumba anayewakaribisha wageni, Mama Blandina aliuvua wadhifa wake na kuanza kututangaza utalii wa Tanzania na kuwafahamisha wale wanaotaka kukeza katika sekta hiyo faida za kufanya hivyo.
Pia alitumia nafasi hiyo kuzungumza na washiriki karibu na makala wote wanaouza utalii wa Tanzania kujua matatizo yao na kuwaeleza bayana mikakati ya Serikali ya awamu ya nne katika kupanua soko la utalii.
Akizungumza katika mahijiano maalum na jarida la Jambo Tanzania linalosambazwa katika ofisi za balozi za Tanzania huku Ulaya, Bibi Nyoni alisema mkutano huo umewafundisha mambo mengi washiriki waliotoka Tanzania, kwanza waliweza kukutana na watu kutoka nchi nyingine ambao wameendelea zaidi katika kuutangaza Utalii, na hivyo waliweza kujifunza baadhi ya mbinu ambazo zinaweza kusaidia kuutanganza zaidi utalii wa Tanzania.
Wanaofanya kazi kwenye sekta ya Utalii Tanzania kujionea ukubwa wa soko la utalii na kupata nafasi ya kutangaza vivutio na huduma zilizopo kwa makampuni ya Utalii ya dunia yanayotaka kutuma watalii Tanzania alisema Bibi Blandina.
Akiuzungumzia matatizo mbalimbali yaliyojitokeza huko nyuma katika sekta ya utalii, Bibi Blandina alisema ni miundo mbinu ikiwa ni pamoja na hoteli na huduma zinazotolewa kwenye mbuga za utalii na kudai kuwa serikali ya Tanzania imeona hali hiyo, na sasa inafanya juhudi za kuboresha miundo mbinu ya kwenye mbuga za wanyama, na tayari mahoteli yanajengwa na barabara zinaendelea kujengwa.
Akizungumzia suala la usalama wa watalii na mali zao , Bibi Nyoni alisema wizara ya Utalii ya Tanzania kwa kushirikiana na idara nyingine za serikali, wameanzsiha utaratibu wa kuwa na kikosi cha pamoja usalama kinachoshirikisha askari wa Jeshi la Polisi na askari wanaolinda wanyamapori ambayo kazi yao kubwa ni kukomesha vitendo vya uhalifu dhidi ya watalii na ujangili kwenye mbuga za wanyama .
Kweli uhalifu katika mbuga za wanyama umepungua kabisa , lakini juhudi zinaendelea ili kufanya usalama uwe mkubwa zaidi na kusiwe na malalamiko kama hayo yanatokea kani ndivyo vitu vinavyoweza kushusha soko la utalii la Tanzanua, hili tumelitilia mkazo mkubwa, alisema.
Akizungumzia mafanikio ya ziara za Rais Kikwete huku Ulaya na Marekani, Bibi Blandina alisema kweli zimewasafishia njia, kwani hata wao sasa hawapati tabu sana katika kufanya hiyo kazi kwa nchi hizo kwani katika nusu ya hutuba zake zilikuwa zinalenga kwenye utalii na wawekezaji.
Mheshimiwa Rais kuwa bega kwa bega kutangaza utalii huku Ulaya na Marekani umetujengea hamasa kubwa sisi watendaji na kweli faida yake Watanzania waiona si muda mrefu,hata wananachi nao watanufaika na hizo hutuba zake alisema.
Katibu Mkuu huyo wa Wizara alisema wananchi si watanufaika na pesa za kodi za utalii, bali pia wanapokuja kwa wingi na kwenda kwenye maneneo yao, wananzci wataweza kuuza vito vyao kama vile shanga, vinyago na vitu vingine, hivyo ni mwananchi nae ananufaika.
Alisema Wizara yake ipo katika mkakati mkubwa kuasnza kujitangaza huku ulaya baada ya kumaliza kule Marekani na China na kusema kuwa kwa mwaka wa fedha wa mwakani wanatarajia kuongeza bajeti kuona uwezekano a kujitangaza zaidi.
Mbali na Bi Blandina viongozi wengine waliambana nae ni Waziri wa Utalii, Biashara na Uwekezaji wa Zanzibar Bi Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa bodi ya Utalii Tanzania, ,Bw. Daniel Yona,Waziri wa Mkurugenzi wa hifadhi za Taifa, Bw. Gerald Bigurube, Mkurugenzi wa Utalii wa TANAPA, Bw. Allan Kijazi, Kaimu Mkurugenzi wa Ngorongor Bw. B.Mrunya,