Katibu Mkuu Ado Shaibu ameendelea na ziara jimbo la Buhigwe

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
605
1,536
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ndugu Ado Shaibu Ado leo tarehe 21 Mei 2021 ameendelea na ziara kwenye Jimbo la Buhigwe kwa kutembelea Kata za Kibwigwa, Bukuba, Janda na Kinazi.

Katibu Mkuu amekutana na Wanachama na viongozi wa Matawi na Kata na kukagua maandalizi ya Chama kuelekea Uchaguzi wa marudio wa Jimbo la Buhigwe uliopangwa kufanyika tarehe 16 Mei 2021 sambamba na Jimbo la Muhambwe na Kata 18.

Akiwa kwenye Kata ya Kinazi Katibu Mkuu amesema ataendelea na programu ya kushuka chini kuonana na wanachama na viongozi kwenye Matawi, Kata, Jimbo na Mikoa.

"Nilipochaguliwa niliihaidi Halmashauri Kuu kuwa Ukatibu Mkuu wangu utakuwa wa field. Nitaendelea kushuka chini kukutana na wanachama na viongozi.
Miezi mitatu baada ya Uchaguzi niliwaandikia Makatibu wa Mikoa na Majimbo kuwa washuke chini kukutana na wanachama na kujenga Chama.

Ninawapongeza sana wanaolifanyia Kazi agizo hilo. Wanaosubiri kukumbushwa na waraka mwingine wa Katibu Mkuu dawa yao inachemka" alisisitiza Katibu Mkuu.

Sendwe Ibrahim,
Mwenyekiti wa Mkoa,
ACT Wazalendo,
Mkoa wa Kigoma.View attachment 1760744View attachment 1760743
IMG_20210422_193330_116.jpg
 
Back
Top Bottom