Katibu mkuu ACT Wazalendo akutana na waziri wa maendeleo wa Sweden

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
609
1,540
Leo tarehe 28 Mei 2021, Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ndugu Ado Shaibu Ado amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa wa Sweden Ndugu Janine Alm Ericson.

Mazungumzo hayo ya Waziri huyo na Vyama Vikuu vya Upinzani Tanzania yaliyofanyika Jijini Dar es salaam yalihudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa CHADEMA Ndugu Ndugu Rodrick Lutembeka na Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Ndugu Anders Sjoberg.

Mazungumzo yaliangazia hali ya kisiasa nchini Tanzania na hatua zinazochukuliwa/zinazopaswa kuchukuliwa kuimarisha demokrasia na utawala bora nchini Tanzania.

Bonifasia Mapunda, Naibu Katibu, Idara ya Mambo ya Nje.
ACT Wazalendo.

28 Mei 2021.


k0vh5m.jpg

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Inasikitisha chama kizima cha upinzani kinapotoa habari ambazo sio sahihi.Janine Alm Ericson sio Waziri wa maendeleo na ushirikiano wa kimataifa. Waziri ni Per Olsson Fridh. Janine ni statssekreterare (wadhifa sawa na katibu mkuu Tanzania).Sio Waziri.

Vyama vinapoleta habari kama hizi ziandike ukweli na sio uzushi.Kama ni kosa la bahati mbaya kwa kushindwa kutafsiri basi wafanye sahihisho kuondoa sintofahamu.
 
Back
Top Bottom